Kwa ujumla wake lengo la raisa wetu Katika hii Dhana ya KUTUMBUWA MAJIPU linaonekana ni zuri machoni mwa watanzania lakini kilicho nyuma ya pazia ni sumu mbaya.
Kuna minongono kuwa utumbuaji majipu ni wa visasi na huwafika waliodhaniwa kukihujumu chama kuelekea uchaguzi wa 2015.
Utumbuaji unasemwa haufuati sheria za utumishi wa umma na umekuwa wa kukurupuka na badhi ya wakati unadhalilisha.
Athari zimekuwa nyingi katika maeneo tofauti.
Kwa mfano licha ya kukusanya mapato kupitia mianya iliyokiukwa hapo nyuma watu wamekosa ajira kwa kuachishwa kazi kutokana na makampuni kulipia madeni waliyotozwa ama kwa kukosa kazi kutokana na maofisi mbali mbali kubomolewa wakati ule wa bomoa bomoa hasa Dar.
Mzunguko wa fedha katika uzalishaji na soko kupunguwa kutokana na sehemu ya mamilioni ya fedha zilizokuwa kwenye mzunguko kulipwa fidia na hivyo kuathiri mzunguko wa pesa .
Vitu vimepanda bei mno kutokana na sehemu ya pesa hizo kuwa mikononi mwa serikali ambapo hutumika kwa mambo ya mipango ya serikali na haiingii sokoni moja kwa moja hatimae wanaNCHI KULALAMIKIA MAISHA MAGUMU.
Athari nyengine ni mjengeko wa maamuzi ya kukurupuka. Hii inajenga woga kwa watendaji na kusababisha kutojiamini kwa watendaji wadogo vile vile Tanzania sasa inapita katika kipindi cha kujengeka tabaka la kidikiteta katika mfumo rasmi ( An Organized chaos) ambapo hapo mbele utaleta shida kwa watanzania.
Watu wanameza machungu na kujenga visasi visivyo maana kwa kutofuatwa taratibu za maamuzi na kuaibishana. Hapa tatizo sio kosa au sababu za kufanya maamuzi tatizo ni UTARATIBU usiofuata sheria au hekima. Tanzania ya sasa inaonja hilo.
Ushauri wangu.
Katika azma njema ya kufanya mageuzi sheria na taratibu zifuatwe ili kutumbuwa majipu kwa maslahi ya watanzania lakini bila kuwaonea watu na kujenga visasi zaidi.
Hekima itumike bila kufanya ajizi au kupinda sheria
Wanaoshabikia wachaguwe mambo ya kushabikia na pale Rais anapokosea au kuteleza wawe tayari kukosoa.
Utumbuaji uwe wa nia njema na usiwe bias kwa lengo la kuijenga nchi.
Nguvu kubwa itumike kujenga MFUMO kwa kufanya mageuzi ya sheria zetu na taratibu zijengwe ili majipu yasiote tena.
Ni hayo. wanaomsifia rais Magufuli wasijisahau.
Nawasilisha