Wanaomsifia rais Magufuli wasijisahau

Wanaomsifia rais Magufuli wasijisahau

We mwana ngurumo uteule wa israel ni upi?unajua ya kwamba kuwa waisrael waliua mitume na manabii wengi sana waliotumwa na Mungu?unajua hadi leo waisrael hawamuamini Yesu? Na wana dini yao inaitwa dini ya wayahudi?Ina maaba unaweza kuwa muovu namna hii still ukawa bado mteule? Dont be brainwashed, zinduka!
 
Ndugu wananchi itakuwa vigumu kunielewa lakini ukitulia na kusoma kwa umakini utanielewa. usiwe na jazba tafakari utaelewa hiki nilichokiandika.

Magufuli ni mwanadamu kama wanadamu wengine, na ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine. siri moja ya wanasiasa ni kutaka kuvuta usikivu wa watu ( to attract population) ila mwisho wa siku ataishia kufanya baadhi ya mambo fulani mazuri na mengi mabaya kama mwanadamu.

Hivi sasa Watanzania wengi wameinua macho kumwangalia Magufuli kama mleta neema na atakaye sababisha nchi kuwa ya maziwa na asali. Pasipo kumung'unya maneno napenda kuwaambia hapana Magufuli hatoweza kamwe kuifanya Tanzania kuwa nchi ya maziwa na asali, ila yupo mmoja tu ambaye Watanzania wanatakiwa kumwinulia macho na kumwambia aiponye nchi yetu ni MUNGU WA MBINGUNI MUUMBA WA MBINGU NA DUNIA

Neno la Mungu linasema amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu
Wewe hufai bure kabisa. Wachina hawana dini, hawatambui uwepo wa Mungu na wanapaa kimaendeleo unasemaje. Wewe unasali kwa mzee wa upako, lwakatare, and the like.
 
Huu ni ushauri wa kiimani au kisiasa? Kwa hiyo tukifanya uchaguzi kwenye karatasi ya kura na Mungu awepo.Swali-tukimchagua Mungu ,tutaweza sheria zake maana hata waisrael walishindwa wakaomba watawaliwe na mwanadamu.
 
Yuko sawa KABISA kwan hta Mungu alifika sehemu ikamlazmu atumbue majipu pale sodoma walipozid,nchi yetu ilikua imefkia pabaya,kwan wao wakat wanafanya ,hyo madudu hawakujua km Sheria haziruhusu kufanya ivyo! Ifike sehemu hata upinzin uwe wenye tija,anyofanya sasaiv ndo ayo walokua wanatwambia mpaka tukawakubali SS Rais anatenda wanalalamika tena tuwaeleweje sasa! Rais endelea kutumbua tu
ko na WW.
 
Mungu huwa anatumia wanadam hata wakati mwingine kuiponya nchi. Daudi alikuwa mwanadamu kama Magufuli lakini Mungu alitenda kazi ndani yake ili kumwangamiza Goliath yule mfilisti aliyekuwa akimtukana Mungu.

Kwa thread yako hii, inaonesha kuwa Magufuli hatotumika kuifanya nchi hii kuwa ya maziwa na asali kwa sababu kuu mbili;
1. Magufuli kama wanasiasa wengine yote anayofanya ni ili kuvuta usikivu wa watu
2. Kwa kuwa watu wameacha kumtegemea Mungu bali magufuli hivyo nchi ya Tanzania imelaniwa

Maoni yangu katika hili ni haya;
1. Katika kila analofanya mwanadamu, anaongozwa na dhamira ambayo huweza kuwa njema au mbaya. Kwa kuwa dhamira hupimwa kwa matokea ya jambo alilofanya mtu basi ikiwa matokeo ya kile kitu ni mema kwa waliowengi, tena waliowanyonge basi utajua dhamira ya mtu ilikuwa njema. Mungu anatabia ya kuangalia wanyonge, wanaoonewa na kudhulumiwa na kwa kuwa magufuli anania hiyo ya kuona waliochini wanainuka iwe kwa sababu za kisiasa au la, basi Mungu yu pamoja naye. Mtume Paulo anasema, ikiwa ni kwa nia njema au kwa hila, kristo anahubiriwa.
2. Tanzania haina Mungu, bali watu wake nao ni wachache wana Mungu. Na kwa kuwa taifa hili si teule kwa Mungu kama ilivyo Israel, basi nchi haitahukumiwa kutokuendelea kiuchumi kwa sbb ya kosa la kumtegemea Magufuli. Marekani, China, Uingereza n,k zina wachawi, wazizi, mashoga, walevi, washirikina tena wengi tu, lakini zimeendelea kiuchumi na hazikuadhibiwa kiuchumi kwa sababu ya dhambi hizo. Hivyo, Tanzania haitaadhibiwa kwa sababu watu wamemtegemea magufuli. Wewe mwenye ufahamu wa kumtegemea Mungu, unapaswa kumwangalia Mungu na kumwomba na si Magufuli.

Nilimwomba Mungu atupe raisi mwenye nia njema na nchi hii, na kwa kuwa ananisikia na kunijibu kama atendavyo katika mengi nimwombayo, katika hili naamini Mungu alinijibu.
Mbona umekuwa mtu aliyekata tamaa, usiye na imani?. Maana ikiwa Mungu alifanya njia kwa wana Israel katika bahari ya shamu, huoni kama hili la Mungu kumtumia Magufuli kuifanya nchi hii kuwa ya maziwa na asali ni dogo sana kwa Mungu. Ni nani aliyekuloga hata usilione hili?
Unapaswa kuomba, kuomba kuomba, wewe ndo utaiponya nchi hii kwa maombi, Magufuli atatumika tu. Mimi nanaendelea kuomba

Mwana wa ngurumo
Hayo mambo ya kutumia Wanadam, Mungu alisha acha muda mrefu. Kwa Islam kwa mfano, baada ya Issa(Read Yesu/Jesus) alikuja Muhammad na baada ya hapo hakuna mwanadam mwingine, kwa kuwa maagizo yalishatumia kwenye vitabu, kilichobaki ni kufuata maagizo hayo tu! Kwa wenzetu Wakristo sina hakika sana, ila nadhan ni Scenario hiyo hiyo!
 
Back
Top Bottom