Wanaomponda Rais Samia hawamaanishi

LAPSE RATE

Member
Oct 18, 2015
59
76
WANAOMSIFU HAYATI MAGUFULI NA KUMPONDA SSH SIYO KWAMBA WANAMANISHA

Na mwalimu Frolian Rwegoshora Julius


Habari ndugu wanajukwaa, kabla ya yote nimeona niwape salamu na pia nimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehehema kwa kutujalia amani na utulivu ambao hauna kifani na nchi nyingine za Afrika na duniani kiujumla zinamezea mate. Haya yote ni matunda ya viongozi bora tulio nao kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kilichotuongoza kwa mda mrefu pasipo umwagaji damu.

Turudi kwenye hoja yangu ya msingi, hivi karibuni kuna kundi kubwa limeibuka likijinasibu kutetea sana serikali ya awamu ya tano chini ya hayati JPM na kuonesha kuwa yeye ndiye alikuwa Rais bora kuliko utawala wa sasa. Naomba niwakumbushe kwamba hawa watu wana choyo na walitamani kupata mamlaka au ni wale waliokuwa kwa namna moja au nyingine wanafaidi matunda ya JPM. Uongozi wa JPM hauna tofauti na wa mrithi wake SSH kwani tunashuhudia uendelezaji wa miradi yote ya maendeleo aliyoiacha JPM kama ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa la umeme wa nguvu za maji kule Rufiji (Stiegler's Gorge) maarufu kama (Mwl. Nyerere Rufiji Hydro Power), utoaji elimu bila malipo kuanzia awali mpaka kidato cha nne, kakamilisha ujenzi wa daraja la Kigongo-- Busisi, n.k.

Binafsi, suala la chanjo naona watu wanalitumia kuwa mtaji wa kisiasa na kujipaisha lakini tukubali kuwa ni sera ya ulimwengu. Hata JPM alishasema chanjo hatutazikubali hadi tujiridhishe kupitia watalaam wetu wa kiafya jambo ambalo Rais SSH hajakurupuka hadi alipopewa majibu yasiyo na shaka kutoka kwa wataalam wa afya. Hii ina maana kuwa hata mtangulizi wake angekuwa hai angekubali chanjo baada ya kujiridhisha kuwa ziko salama.

Shida inatoka wapi? Shida ni uchu wa madaraka na manufaa binafsi ya baadhi ya watu waliodhani kuwa wanufaika wa Serikali ya awamu ya tano ambao wamejikuta njia panda katika awamu ya sita. Hili ni tatizo sugu kwa nchi za kiafrika kuunga mkono juhudi pale watu wanapoona manufaa ya moja kwa moja kwa familia zao na si kwa manufaa ya Taifa. Chanjo inawasaidia watanzania wenzetu kufanya yafuatayo:

1. Kufanya biashara ya kimataifa.
2. Kupata fursa ya kielimu kwenye mataifa ya nje.
3. Safari za rufaa za kimatibabu nje ya nchi.
4. Safari za kimadhehebu ya dini (hija).
5. Wanamichezo kuweza kusafiri kimataifa bila vikwazo.
6. Ukuaji wa shughuli za utalii wa kimataifa hasa ktk hifadhi zetu za taifa.

⏺️Sasa inakuwaje hatuoni hizi faida kama taifa? Hakuna Serikali yoyote duniani inayoweza kufurahi watu wake waangamie. Tuamini serikali yetu na vyombo vyake, tusiwe watu wa kupinga kila jambo.

Wanaompinga SSH hawamaanishi bali wamekosa fursa

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Kazi iendelee
 
Back
Top Bottom