mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,610
- 1,602
Nimefatilia hoja mbalimbali humu JF zinazohusu COVID19, nikagundua kuna mkumbo wa watu wengi kulaumu serikali hasa Raisi Magufuli.
Wengi wanalaumu wakiwa na hoja kwamba Rais ajafanya lockdown kama walivyofanya nchi jirani kama Uganda, Rwanda, partial lockdown ya Kenya n.k wakihoji asipofanya lockdown maambukizi yatakua makubwa zaidi.
Pili wengi wanalaumu wakiwa na hoja kwamba serikali haitoi takwimu za wagonjwa na vifo vinavyotokana na Corona kwa wakati, wakihoji kama takwimu zikitolewa sahihi itasaidia watu kuchukua tahadhali zaidi.
Tatu wanalaumu wakiwa na hoja kwamba Hotuba ya Rais aliyotoa haikua na msaada kwa mapambano ya corona hasa wakibeza mbinu alizoshauri Rais, mbinu ambazo ni kusali, Kujifukiza, kutumia vitu vya asili kama vitunguu, limao, tangawizi n.k wakihoji kwamba kwanini serikali isiagize Ventilator na vifaa vingine vya kujikinga na Corona pia wakishauri serikali kutumia mbinu za kisayansi kupambana na corona n.k
Nne wanalaumu wakiwa na hoja kwamba Rais anakimbia mapambano ya corona kwa kukaa kwao Chato badala ya kukaa ikulu Dar es salaam au Dodoma wakihoji kwamba kwanini Rais asikae katika ofisi zinazotambulika na wananchi, kuliko akikaa Chato.
Wakihoji Rais akiwa ikulu Dar es salaam au Dodoma ataongeza nguvu kwenye mapambano zidi ya ugonjwa wa corona.
Tano wapo wanalaumu utaratibu unaotumiwa na serikali katika kuzika waliofariki na Corona, hasa wanalaumu mda wa kuzika, kwani imeonekana baadhi ya watu waliokufa kwa Corona wakizikwa usiku na serikali .
Wanahoji maziko yafanyike mchana kweupe ili watu waweze kuchukua tahadhali zaidi na pia vyombo vya habari viweze kuandika habari vizuri.
Wapo wanaolalamika kwamba vituo vya afya, zahanati, na hospital za serikali zinakataa kupokea wagonjwa wa Corona na kupelekea wagonjwa kufariki kwa kukosa huduma za afya pindi wakizidiwa na ugonjwa wa corona.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo asilimia kubwa ya watu wanalaumu au kuhoji serikali hasa Raisi Magufuli kwa kushindwa kuwajibika kuhusu mlipuko wa ugonjwa unaoambukiza haraka wa Corona
Sasa ningependa kuyatolea ufafanuzi na pia ushauri haya mambo ila kabla sijayatolea ufafanuzi au ushauri ni vizuri kama kuna mwingine mwenye malalamiko au hoja kwa serikali aelezee ili nijumuishe katika maelezo au ushauri wangu
Lengo la hii mada ni kushirikiana pamoja ili tuweze kujikinga na hili gonjwa na pia kuachana na lawama nyingi kwa serikali hasa Raisi Magufuli
Sent using Jamii Forums mobile app