Asante sana,
Hayo maua - maua halisi, this is no mere figure of speech- mimi tayari nina pink rose bush hapa nyumbani ninapoishi, linachanua vizuri in the spring. Pia nina red rose bush kubwa sana in Bronx, New York. Nilipanda kwenye nyumba yangu ya Bronx miaka mingi sana iliyopita.
Mimi kila nikijenga au kununua nyumba kitu cha kwanza najipa ni maua au mti wa matunda, kwa hivyo, ukiniongezea nashukuru, lakini, usiponipa, nishapanda maua mwenyewe kwenye nyumba zangu.
Moja ya vitu nilivyojifunza katika maisha ni ku appreciate vitu kama flora and fauna, huu ni utajiri kuliko pesa.
Umenifanya kufikiria kuanzisha thread ya vitabu ninavyosoma, kuvifanyia review, na kusikiliza wengine walisoma wanavifikiriaje.
Nafikiri thread hiyo, tukiwa na inclusivity nzuri, na kuondoa obvious troll, tunaweza kuwa na mazungumzo mazuri.
Wiki hii nilikaa na wachumi fulani, wakanipa mrejesho wao kuhusu kitabu fulani nilichokuwa nakiona kizuri sana kuhusu uchumi, halafu, kutokana na mrejesho wao, nikakiona tofauti kabisa, nikajifunza mambo mengi kutoka kwao.
Kwa hivyo, kama utapenda tuwe na threads fulani za kujadili vitabu na articles fulani, ambazo naona ni muhimu, naweza kuanzisha series hiyo.