Wanaomiliki silaha na hawajazihakiki wazisalimishe polisi haraka, database wanayo, msako unaanza

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969
Jeshi la polisi mkoani Lindi limewataka wote ambao hawajahakiki silaha zao wazisalimishe haraka kwa jeshi la polisi kabla hawajazifuata huko ziliko
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata Mzinga amesema jeshi la polisi limeshatoa muda wa kutosha wa kuhakiki silaha na kama hujahakiki na bado unamiliki silaha hiyo ni vema ukaisalimisha
ameongezea wao wana database ya silaha zote na wataanza kuzifuata huko ziliko ambazo hazijahakikiwa
Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa wakimuona yoyote anayemiliki silaha isivyo kihalali
 
Natumaini operation hii itafanyika nchi nzima. Hii itasaidia katika kuhakikisha watanzania na mali zao wanakuwa salama zaidi.
 
Hii nayo ni aina ya ujinga mpya hapa nchini!!!
Kama database mnayo yanini kutishatisha watu?? Ambao hawajaja kuhakiki tumieni taarifa zenu kwenye hiyo database muwafikie na kuwatia adabu.
Kelele zitasaidia kipindi cha kulinda mtama usiliwe na kwelea kwelea.
 
Back
Top Bottom