Wanaokejeli anayofanya Rais Magufuli wanaacha maswali

K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,067
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,067 280
TANGU Rais John Magufuli aingie madarakani, wapo watu ambao wamekuwa wakiendelea na kampeni ya kubeza juhudi anazofanya kusimamia utendaji, uwajibikaji serikalini, udhibiti wa matumizi ya serikali na usimamizi wa shughuli za maendeleo.

Wengine wamekuwa wakinyoosha kidole moja kwa moja kwa Rais na kukosoa baadhi ya juhudi zake zikiwemo za kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma kwa kutumbua majipu. Wakosoaji wamekuwa wakijizuia kurejea historia ya Magufuli kabla ya kushika urais inayomwonesha namna ambavyo tangu mwanzo alikuwa kiongozi anayetekeleza majukumu yake serikalini kwa kujituma zaidi.

Tangu akiwa katika Awamu ya Tatu ya uongozi wa Serikali chini ya Rais Benjamin Mkapa, Magufuli ana mengi ya kujivunia ambayo umma wa Watanzania ulishuhudia akiyatekeleza. Kwa kifupi Magufuli wa sasa ni yuleyule ambaye alisemekana ndiye waziri asiye na doa na kila wizara iliyokuwa haionekani kutenda mambo ipasavyo watu wakapendeleza Magufuli apelekwe huko! Akiwa Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, kwa mfano, anakumbukwa alivyosimamia kidete sakata la samaki waliovuliwa bila kibali katika bahari ya Hindi.

‘Samaki wa Magufuli’ ni jina lililotokana na samaki waliokamatwa mwaka 2009 katika meli ya Tawaliq 1 ikiwa na wafanyabiashara wa nje ya nchi waliokuwa wakiendesha uvuvi haramu. Meli hiyo ilikamatwa ikiwa na tani 293 za samaki aina ya jodari waliovuliwa kwenye ukanda wa kiuchumi bila ya kuwa na kibali. Hata hivyo, kesi dhidi ya raia hao wa nje ilitupwa na serikali ikaamuriwa iwalipe sanjari na kuwapatia hati zao za kusafiria. Mjadala kuhusu sakata hili nitauendeleza siku nyingine.

Lakini mbali na hilo, Magufuli anakumbukwa alivyosimama kidete katika kupambana na uvuvi haramu kiasi cha samaki nchini kuongezeka kwa kasi. Wavuvi wengi bado wanamkumbuka namna alivyosaidia ongezeko la samaki na bila shaka wanakumbuka namna hali ilivyokuwa mbaya katika siku za karibuni kabla ya serikali kuchukua hatua za sasa za kukomesha uvuzi haramu nchini. Nirudi kwenye hoja ya watu wanaokejeli juhudi za Rais Magufuli.

Katika hali ya kawaida, nchi ilikokuwa imefikia kwa sasa Rais anastahili kufanya uamuzi unaoakisi wakati wa sasa uliogubikwa na kero mbalimbali. Mfano, afya ni miongoni mwa sekta zilizokabiliwa na malalamiko mengi. Utendaji na nidhamu isiyoridhisha miongoni mwa watumishi ni moja ya malalamiko ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeanza kuyafanyia kazi kwa kasi.

Miongoni mwa mifano, ni mabadiliko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo kwa namna moja au nyingine, huduma zake zilikuwa zimedorora lakini kwa sasa zinavutia. Magufuli amewezesha kununuliwa kwa baadhi ya vitendea kazi muhimu katika kipindi kifupi cha uongozi wake. Aidha bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Sh bilioni 41 za mwaka wa fedha uliopita hadi Sh bilioni 251 kwa mwaka huu. Eneo lingine ambalo Rais Magufuli amelifanyia kazi, ni udhibiti wa mapato na watumishi hewa.

Maelfu ya watumishi hewa wamebainika. Uwajibikaji kwa watumishi wa karibu kada zote umeimarika katika kada zote. Wananchi sasa wanashuhudia mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na watumishi wengine hadi ngazi ya chini, wakishughulika na wananchi tofauti na mazoea yaliyojengeka ya kukaa ofisini. Uwajibishaji wa viongozi wa ngazi za juu (vigogo) waliokuwa wamekalia kufuja mali za umma na wale ambao hawaoneshi utendaji uliotukuka, ni ishara tosha ya uongozi thabiti wa Magufuli.

Taasisi na idara mbalimbali za serikali zimeguswa na utumbuaji majipu wa Rais Magufuli alioufanya ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Hata sasa anaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo, kuwashusha au kuwaondoa madarakani wale anaoona uwajibikaji wao una walakini. Baadhi ya taasisi ambazo zilionja chungu ya utendaji wa rais ndani ya siku 100 za uongozi wake, ni pamoja na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo baadhi ya vigogo walisimamishwa kazi kwa tuhuma za kuwapo uozo bandarini.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pia ilikumbwa na utumbuaji majipu uliokwenda sanjari na kutengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu na watumishi kadhaa kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Itakumbukwa pia Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli nchini (RAHCO), ilikumbwa pale mkurugenzi mkuu wake aliposimamishwa kazi. Hadi sasa ambapo Rais Magufuli ametimiza mwaka madarakani, idadi ya taasisi zilizoguswa; kwa maana ya watendaji wake kuwajibishwa, hazihesabiki.

Pamoja na mabadiliko haya katika sekta mbalimbali, bado wapo watu ambao hawataki kuyaona badala yake, wamegeuka mahiri wa kukosoa kila jambo. Kinachosikitisha ni kwamba, baadhi ya wanayosema kama ukosoaji ni yale yale waliokuwa wakipigia kelele miaka ya nyuma kuwa yamekithiri serikalini, mintarafu suala zima la uwajibakaji na ufisadi. Bahati mbaya, baadhi ya wakosoaji, hawaoneshi njia, kwa maana ya wao kuwajibika katika kuleta maendeleo. Hapo ndipo wakosoaji hawa wanapoacha maswali mengi ya kujiuliza.

Ingawa katika hali ya kawaida, hakuna binadamu asiye na upungufu, pia hilo halikosekani pia kwa Rais Magufuli. Lakini upungufu huo usifunike mambo mema anayofanya kiasi cha kuuaminisha umma kwamba hakuna la maana linalotendeka.

Wanaobeza juhudi hizi za Rais hawaitakii mema nchi. Ingawa kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake, wakati mwingine demokrasia hii inatumika vibaya pale ambapo baadhi ya watu hupotosha na hata kutumia lugha zisizo na staha kwa kiongozi mkuu wa nchi. Ifike wakati, Watanzania hususan wanasiasa, waitendee haki nchi kwa ukosoaji wenye tija.
 
kidamva

kidamva

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,581
Likes
1,671
Points
280
kidamva

kidamva

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,581 1,671 280
Mnaomtetea Rais Magufuli ndio mnaacha maswali zaidi. Mwaka mmoja tangu aingie madarakani wananchi wanalia umasikini, fedha hazipo kwenye mzunguko, benki zinafilisika, biashara nyingi zinafungwa, wafanyakazi wanafukuzwa, huko Serikalini watumishi wa umma wanahakikiwa kama wafungwa. Yaani kwa ujumla nchi haina raha.
Afadhali basi angekuwa anabana matumizi halafu kuwe na unafuu wa maisha, lakini nchi imekuwa shubiri
 
kibwenzi

kibwenzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
2,498
Likes
1,327
Points
280
kibwenzi

kibwenzi

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
2,498 1,327 280
Hayo ni maoni yako ..usitulishe maneno na sisi
 
kmbwembwe

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
6,747
Likes
1,608
Points
280
kmbwembwe

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
6,747 1,608 280
Mnaomtetea Rais Magufuli ndio mnaacha maswali zaidi. Mwaka mmoja tangu aingie madarakani wananchi wanalia umasikini, fedha hazipo kwenye mzunguko, benki zinafilisika, biashara nyingi zinafungwa, wafanyakazi wanafukuzwa, huko Serikalini watumishi wa umma wanahakikiwa kama wafungwa. Yaani kwa ujumla nchi haina raha.
Afadhali basi angekuwa anabana matumizi halafu kuwe na unafuu wa maisha, lakini nchi imekuwa shubiri
yaani ni his master's voice. hii kanda tangu irekodiwe na wapinzani wa jpm imeshachuja. kama mazuzu mnaendelea kuicheza. wasomi nchini na nje ya nchi wamesema uchumi wa nchi ni mzuri tena unakua. uchumi mbaya ni wa wapiga dili. kwao ni kweli hela hakuna.
 
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Messages
9,257
Likes
1,966
Points
280
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined May 1, 2009
9,257 1,966 280
TANGU Rais John Magufuli aingie madarakani, wapo watu ambao wamekuwa wakiendelea na kampeni ya kubeza juhudi anazofanya kusimamia utendaji, uwajibikaji serikalini, udhibiti wa matumizi ya serikali na usimamizi wa shughuli za maendeleo.

Wengine wamekuwa wakinyoosha kidole moja kwa moja kwa Rais na kukosoa baadhi ya juhudi zake zikiwemo za kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma kwa kutumbua majipu. Wakosoaji wamekuwa wakijizuia kurejea historia ya Magufuli kabla ya kushika urais inayomwonesha namna ambavyo tangu mwanzo alikuwa kiongozi anayetekeleza majukumu yake serikalini kwa kujituma zaidi.

Tangu akiwa katika Awamu ya Tatu ya uongozi wa Serikali chini ya Rais Benjamin Mkapa, Magufuli ana mengi ya kujivunia ambayo umma wa Watanzania ulishuhudia akiyatekeleza. Kwa kifupi Magufuli wa sasa ni yuleyule ambaye alisemekana ndiye waziri asiye na doa na kila wizara iliyokuwa haionekani kutenda mambo ipasavyo watu wakapendeleza Magufuli apelekwe huko! Akiwa Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, kwa mfano, anakumbukwa alivyosimamia kidete sakata la samaki waliovuliwa bila kibali katika bahari ya Hindi.

‘Samaki wa Magufuli’ ni jina lililotokana na samaki waliokamatwa mwaka 2009 katika meli ya Tawaliq 1 ikiwa na wafanyabiashara wa nje ya nchi waliokuwa wakiendesha uvuvi haramu. Meli hiyo ilikamatwa ikiwa na tani 293 za samaki aina ya jodari waliovuliwa kwenye ukanda wa kiuchumi bila ya kuwa na kibali. Hata hivyo, kesi dhidi ya raia hao wa nje ilitupwa na serikali ikaamuriwa iwalipe sanjari na kuwapatia hati zao za kusafiria. Mjadala kuhusu sakata hili nitauendeleza siku nyingine.

Lakini mbali na hilo, Magufuli anakumbukwa alivyosimama kidete katika kupambana na uvuvi haramu kiasi cha samaki nchini kuongezeka kwa kasi. Wavuvi wengi bado wanamkumbuka namna alivyosaidia ongezeko la samaki na bila shaka wanakumbuka namna hali ilivyokuwa mbaya katika siku za karibuni kabla ya serikali kuchukua hatua za sasa za kukomesha uvuzi haramu nchini. Nirudi kwenye hoja ya watu wanaokejeli juhudi za Rais Magufuli.

Katika hali ya kawaida, nchi ilikokuwa imefikia kwa sasa Rais anastahili kufanya uamuzi unaoakisi wakati wa sasa uliogubikwa na kero mbalimbali. Mfano, afya ni miongoni mwa sekta zilizokabiliwa na malalamiko mengi. Utendaji na nidhamu isiyoridhisha miongoni mwa watumishi ni moja ya malalamiko ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeanza kuyafanyia kazi kwa kasi.

Miongoni mwa mifano, ni mabadiliko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo kwa namna moja au nyingine, huduma zake zilikuwa zimedorora lakini kwa sasa zinavutia. Magufuli amewezesha kununuliwa kwa baadhi ya vitendea kazi muhimu katika kipindi kifupi cha uongozi wake. Aidha bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Sh bilioni 41 za mwaka wa fedha uliopita hadi Sh bilioni 251 kwa mwaka huu. Eneo lingine ambalo Rais Magufuli amelifanyia kazi, ni udhibiti wa mapato na watumishi hewa.

Maelfu ya watumishi hewa wamebainika. Uwajibikaji kwa watumishi wa karibu kada zote umeimarika katika kada zote. Wananchi sasa wanashuhudia mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na watumishi wengine hadi ngazi ya chini, wakishughulika na wananchi tofauti na mazoea yaliyojengeka ya kukaa ofisini. Uwajibishaji wa viongozi wa ngazi za juu (vigogo) waliokuwa wamekalia kufuja mali za umma na wale ambao hawaoneshi utendaji uliotukuka, ni ishara tosha ya uongozi thabiti wa Magufuli.

Taasisi na idara mbalimbali za serikali zimeguswa na utumbuaji majipu wa Rais Magufuli alioufanya ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Hata sasa anaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo, kuwashusha au kuwaondoa madarakani wale anaoona uwajibikaji wao una walakini. Baadhi ya taasisi ambazo zilionja chungu ya utendaji wa rais ndani ya siku 100 za uongozi wake, ni pamoja na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo baadhi ya vigogo walisimamishwa kazi kwa tuhuma za kuwapo uozo bandarini.

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pia ilikumbwa na utumbuaji majipu uliokwenda sanjari na kutengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu na watumishi kadhaa kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Itakumbukwa pia Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli nchini (RAHCO), ilikumbwa pale mkurugenzi mkuu wake aliposimamishwa kazi. Hadi sasa ambapo Rais Magufuli ametimiza mwaka madarakani, idadi ya taasisi zilizoguswa; kwa maana ya watendaji wake kuwajibishwa, hazihesabiki.

Pamoja na mabadiliko haya katika sekta mbalimbali, bado wapo watu ambao hawataki kuyaona badala yake, wamegeuka mahiri wa kukosoa kila jambo. Kinachosikitisha ni kwamba, baadhi ya wanayosema kama ukosoaji ni yale yale waliokuwa wakipigia kelele miaka ya nyuma kuwa yamekithiri serikalini, mintarafu suala zima la uwajibakaji na ufisadi. Bahati mbaya, baadhi ya wakosoaji, hawaoneshi njia, kwa maana ya wao kuwajibika katika kuleta maendeleo. Hapo ndipo wakosoaji hawa wanapoacha maswali mengi ya kujiuliza.

Ingawa katika hali ya kawaida, hakuna binadamu asiye na upungufu, pia hilo halikosekani pia kwa Rais Magufuli. Lakini upungufu huo usifunike mambo mema anayofanya kiasi cha kuuaminisha umma kwamba hakuna la maana linalotendeka.

Wanaobeza juhudi hizi za Rais hawaitakii mema nchi. Ingawa kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni yake, wakati mwingine demokrasia hii inatumika vibaya pale ambapo baadhi ya watu hupotosha na hata kutumia lugha zisizo na staha kwa kiongozi mkuu wa nchi. Ifike wakati, Watanzania hususan wanasiasa, waitendee haki nchi kwa ukosoaji wenye tija.
Mengi anayofanya ni ya kawaida sana tatizo mbwembwe na kelele ndo nyingi
 
kidamva

kidamva

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,581
Likes
1,671
Points
280
kidamva

kidamva

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,581 1,671 280
yaani ni his master's voice. hii kanda tangu irekodiwe na wapinzani wa jpm imeshachuja. kama mazuzu mnaendelea kuicheza. wasomi nchini na nje ya nchi wamesema uchumi wa nchi ni mzuri tena unakua. uchumi mbaya ni wa wapiga dili. kwao ni kweli hela hakuna.
Hivi wale watoto wa masikini waliokosa mikopo wakiwa na sifa ni wapiga deal? Wale wagonjwa wanaokosa dawa hospitalini ni wapiga deal? Wafanyakazi walioajiriwa halafu ajira zao zikasitishwa nao ni wapiga deal? Yaani CCM mmeifukarisha nchi halafu mnatukana watu wapiga deal? Lazima mtu aambiwe anapopoteza mwelekeo.
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
46,231
Likes
33,393
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
46,231 33,393 280
Wanaoleta mada kama hizi wapo Tanzania kweli au wapo KEnya?
Au hawa ni ndugu zake JP wanaishi naye nyumba moja?
Najiuliza ni watu wa aina gani?
Au ni wale maded wateuliwa?
Kuna anayefahamu atusaidie...?
 
Wong Fei

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2016
Messages
3,757
Likes
4,150
Points
280
Wong Fei

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2016
3,757 4,150 280
Hivi wale watoto wa masikini waliokosa mikopo wakiwa na sifa ni wapiga deal? Wale wagonjwa wanaokosa dawa hospitalini ni wapiga deal? Wafanyakazi walioajiriwa halafu ajira zao zikasitishwa nao ni wapiga deal? Yaani CCM mmeifukarisha nchi halafu mnatukana watu wapiga deal? Lazima mtu aambiwe anapopoteza mwelekeo.
Mkuu achana nao. Wamekaririshwa na mkuu wao. Siku zote hawa jamaa wana akili za kushikiwa. Sidhani km hata darasani walikuwa wanafanya vizuri. Nalifikiri ni wale wanafunzi wa dvn 5
 
Forum statistics

Threads 1,274,988
Members 490,865
Posts 30,529,728