Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,045
- 38,952
Wakuu, kumekuwa na dhana inayoendelea kushikiwa bando na watu wengi na sasa hata baadhi ya viongozi wamekumbwa na dhana hii na kuihalalisha.
Mfano, Juzi Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba, akiongea na wapiga kura wake alimwelezea Mh. Dr. John Pombe Magufuli kama Rais wa wanyonge.
Ninachojiuliza na kuomba ufafanuzi wa wajuzi wa haya mambo ya siasa na jamii ni kina nani hawa wanyonge? Je, kama hali iko hivyo ina maana nchi hii kuna watu ambao Magufuli siyo Rais wao kwa vile wao siyo wanyonge? Ni vigezo gani vinavyotumiwa na viongozi wa Serikali kama Waziri Mwigulu kupembua wapi wanyonge na wapi wenye nguvu?
Tafadhali naomba ufafanuzi wenu.