Wanaoishi Jana Wanatusumbua Leo; Tutaiokoaje Kesho?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,739
40,864
majaliwa-3-jpg.322619
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Rais J.P. Magufuli inapozidi kujipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo na kifikra katika kuimarisha utendaji wa utumishi wa umma kuelekea 2020 ni watendaji na viongozi ambao bado wanaishi jana wakati nchi iko leo na hivyo wanatishia hatima ya taifa letu kesho.

Jana yetu ni miaka ya nyuma ambapo watendaji waliweza kufanya lolote bila kujali sana matokeo (with impunity) na wafanyakazi walijua watendaji wao walikuwa "hivi na vile" kiasi wkamba watumishi wa chini nao baadhi yao walianza kufanya mambo bila kujali matokeo. Mtu alipopata nafasi ya ajira au kupandishwa cheo fikra za kwanza ambazo inaonekana watu walikuwa nazo ni vipi katika nafasi hizo watachuma kwa haraka haraka kabla mambo hayajabadilika.

Taratibu za ajira na utendaji kazi zilifuatwa kama vipe ni jambo la hiari (optional) kiasi kwamba ulazima wa kusimamia sheria na taratibu ulionekana ni usumbufu mkubwa. Mwananchi alipoamua kwenda kupata huduma fulani kwenye taasisi ya serikali ni lazima afikirie mara mbili na kujiandaa kiakili (pyschologically) na usumbufu wowote ambao ataupata. Mwingine inabidi aulize kwanza kama kuna mtu yeyote anayemfahamu huku au kama anafahamu mtu anayeweza kuwa anafahamiana na mtu mwingine huko anakotaka kwenda. Sehemu nyingine katika kutafuta mtu wa kufahamiana naye mtu aliweza kwenda hata kipeo cha tatu na cha nne cha marafiki. Akipatikana anayejuana na fulani huko basi mtu anaweza kua na imani kuwa anaweza angalau kusikilizwa; akikosekana bajeti ya kulainisha mifumo inabidi ifikiriwe tena.

Maisha haya ya jana yamejionesha kwa kiasi kikubwa katika utendaji wa uzembe na usiojali fedha za wnaanchi kama ambavyo ripoti mbalimbali za CAG zimekuwa zikituonesha tangu 2006. Hii jana watu walikuwa wameizoea kiasi kwamba leo haikuruhusiwa ifike kamwe; watu waliipenda jana sana kiasi kwamba hata wakati wa kampeni za uchaguzi bado lilikuwepo kundi la watu ambao waliitamani leo lakini hawakuwa tayari kuiachilia jana.

Matukio karibu matatu yaliyotokea Alhamisi iliyopita yametudokeza kuwa bado tuna tatizo la watu wanaoishi jana. Muhimbli ilitarajiwa uongozi mpya kuanza kuondoa kero ambazo si za lazima; hii siyo tu uongozi wa Muhimbili bali pia Wizara ya Afya; lakini inaonekana mazoea magumu. Bado watu wamekutwa tena wamejazana wodini kama vile wako kwenye behewa la Daraja la tatu wakielekea Bara. Hivi kweli bado hakuna mtu mwenye akili za 'kawaida' tu kuwa watu wanaohitaji huduma safi, salama na mazingira mazuri kabisa ya tiba ni kina mama na watoto - kwa sababu ya udhaifu (vulnerability) yao? Kama watu hawa wanashindwa kuliweka hili kama ajenda yao nambari 1 hivi huko kwingine watapanga nini? Kama inabidi kufuta posho na mishahara ya viongozi wote ili kina mama na watoto wetu wapatiwe huduma sahihi na bora basi na liwe hivyo; lakini hili halieleweki?

Kabla hatujatulia Mwigulu Nchemba naye kazukia huko Pugu (kwa mara nyingine) kufuatilia machinjio. Akakuta kati ya ng'ombe 200 waliokuwa wanaenda kuchinjwa (au sijui wameshachinjwa) ni 20 ambao walikuwa na vibali; huku wale wengine wote kama wamelipiwa basi wamelipiwa kwenye mifuko ya mtu na labda kwa kiasi cha chini kidogo na hivyo kuikosesha serikali mapato; na hilo ni siku moja tu! Hawa watu wa machinjioni walikuwa wanaamini basi ile ya kwanza ni nguvu ya soda basi wacha waendelee kama ilivyokuwa (status quo was maintained). Hawakuwa tayari kuamini kuwa mtu atarudi tena na inawezekana hata watakaoingia bado watafikiria Mwigulu hatawazukia tena na hivyo wataanza na wao kutafuta 'mitkasi' ya hapa na pale. Warudi jana.

Na kabla hata hatujatulia Waziri Mkuu Kassim "Tabasamu" Majaliwa (nimempa jina la 'tasabamu' kwa sababu tabasamu lake linadanganya watu) karudi tena Bandari ambako nako akakuta madudu mengine yale yale na tena safari hii ikitisha zaidi. Kwamba, mpango wake wa kwenda huko kwa kushtukizwa baada ya kutoshwa na watumishi safi ukatibuliwa na 'mbeya' mmoja kiongozi wajuu tu ambaye aliamua kuwadokeza na hivyo kutaka kusaidia kuficha madudu huko.

Nakubaliana na wengine wote kuwa Waziri huyo akithibitika kweli ametuma ujumbe wa kumtonya mama Chuwa ili ajaribu kuvuruga ushahidi basi Magufuli hana jinsi; ni lazima amuondoe Waziri huyo bila kujali uwezo wake, ujiko wake, au sifa zake. Serikali hii haipaswi na haitakiwi hata kuuliza "mwenzetu ilikuwaje ukavuruga mipango ya waziri Mkuu". Hii ni hujuma ya ndani (internal sabotage). Tena hili inapaswa lifanyiwe kazi mapema sana ili kuleta heshima na woga kwa viongozi wengine. Magufuli akipepesa macho tu na kujikwaa tu atajitengeneza udhaifu usio wa lazima.

Nina uhakika wapo viongozi wengine na watumishi wengine ambao bado na wenyewe wanaombea kuwa safisha safisha hii haitowafikia na kwamba, hizi zote zilikuwa nguvu za soda. Siku 100 baadaye nguvu za soda bado zinachemka na kama tulisikia dokezo kidogo Bandari ni mojatu ambako kunahitaji kusafishwa ili safisha hii iendelee maeneo mengine. Hawa wa sehemu nyingine kama wana akili timamu wanapaswa ama kuanza kujiondoa wenyewe au wasubiri shoka la Magufuli liwekwe kwenye mashina yao!

Jana imepita; waliotumikia fikra za wa jana wajue kuwa siku mpya imefka. Hili nililisema mwanzoni lakini bado watu hawaamini kuwa kuna siku mpya. Hawaamini kuwa kiongozi huyu siyo yule na fikra zinazomuongoza siyo zile. Waliozoea kubebana, kufichiana na kusaidiana kufika hujuma, rushwa, magendo na hujuma za kila namna wakati wao uliishia jana.

Ni lazima washughulikiwe leo kama tunataka kesho iliyo bora; kama tunataka watoto wetu na vijana wetu wanafikiria kutumikia umma kuwa na misingi mizuri, ni lazima uchafu wa jana usafishwe. Usafishwe na kila mtu ajue kuwa tunahitaji utumishi wa umma ulio msafi na ambao uchafu kidogo tu ukitokea hauchelewi kushughulikiwa. Na katika kushughulikia ni lazima tuwatoe mfano wale wenzetu wote ambao tulidhani wanaijua leo lakini bado kifikra wametiwa pingu za jana na bado hawajaziachilia; kwani hawa ni hatari kwa kesho yetu na ya keshokutwa ya watoto wetu na mtondogoo wa watoto wa watoto wetu.

Siku mia zimepita lakini siku mamia bado zinakuja. Mwendo wa kurudisha heshima katika utumishi wa umma na weledi wa watumishi unapaswa kuongeza kasi. Mpaka Watanzania tuheshimiane na tuheshimu utumishi wa umma.

Hadi hivi sasa hakuna majuto.

MMM
 
Jana yetu ni miaka ya nyuma ambapo watendaji waliweza kufanya lolote bila kujali sana matokeo (with impunity) na wafanyakazi walijua watendaji wao walikuwa "hivi na vile" kiasi wkamba watumishi wa chini nao baadhi yao walianza kufanya mambo bila kujali matokeo. Mtu alipopata nafasi ya ajira au kupandishwa cheo fikra za kwanza ambazo inaonekana watu walikuwa nazo ni vipi katika nafasi hizo watachuma kwa haraka haraka kabla mambo hayajabadilika.

Naona leo ukwenye mada husika!
Ni pale tu impunity itakapo kuwa siyo ya njia mmoja!.
njia na hatua ya JP na Pm wake ni one man show! Leo hii ni aibu kuwaona Yona na Mramba wakifagia barabara huku 11 bilioni zimeliwa na hawajaturudhishia hata senti.

Raisi mwenye Impunity kufanikiwa ni kazi! Ni pale tu uwanja wa kuwajibishana unapokuwa sawa mbele ya Haki ndipo nidhamu na imani inapojengeka! Ni kweli Raisi msafi anaweza kupunguza tatizo la ufisadi lakini kwa kiwango ndogo sana!
 
Hii nchi ilikuwa imeoza kabisa.

Na huu uozo ambao sasa unaanza kujitokeza ni indictment kubwa sana dhidi ya CCM na serikali zake.

Wasiwasi wangu ni kuna watu ambao ndo wamechangia kuuleta huo uozo ambao hawataguswa kabisa.

Hii in hofu ya kweli; na ni kweli haya yote ni mashtaka yasiyopingika dhidi ya utawala wa CCM. Ubaya ni kuwa badala ya wapinzani ambao tulitarajia wangekuja na kusafisha leo wanaosafisha ni wana CCM wenyewe. Hili linapaswa kutufunza kitu. Hata hivyo naamini - na ushahidi unazidi kuendelea - hakuna yeyote ambaye alikuwa ni tatizo atadumu. Kuguswa kwa Hosea ilipaswa kuwa somo la kutosha; kugushwa kwa Mkuu wa Uhamiaji ilikuwa somo kwa wengine na wengine wataguswa vizuri tu. Hili likutoe shaka. Hakuna mti mtakatifu tena wala ng'ombe mtakatifu. Leo si jana.
 
Mwambie Magu atumbue majipu ya kivuko cha bagamoyo na vingine ambavyo vinaota kutu bila kufanya kazi ilhali vilinunuliwa kwa gharama kubwa....

Hii nchi imeoza kiasi kwamba kama kweli huo utumbuaji wa majipu utakuwa ni wa haki basi kuna watu nao itabidi wajitumbue wenyewe hayo majipu yao.

Swali ibuka; je, watajitumbua?
 
Kama ulivyoainisha, old/bad habits die hard... tulifikia pabaya sana..people commited crime with impunity!
Overhauling culture/utamaduni mzima wa corruption si kitu ya siku moja na Magufuli pekeyake hawezi...anahitaji msaada wetu sote... when it comes to fighting corruption, everyone is a stakeholder.
 
Hii in hofu ya kweli; na ni kweli haya yote ni mashtaka yasiyopingika dhidi ya utawala wa CCM. Ubaya ni kuwa badala ya wapinzani ambao tulitarajia wangekuja na kusafisha leo wanaosafisha ni wana CCM wenyewe. Hili linapaswa kutufunza kitu. Hata hivyo naamini - na ushahidi unazidi kuendelea - hakuna yeyote ambaye alikuwa ni tatizo atadumu. Kuguswa kwa Hosea ilipaswa kuwa somo la kutosha; kugushwa kwa Mkuu wa Uhamiaji ilikuwa somo kwa wengine na wengine wataguswa vizuri tu. Hili likutoe shaka. Hakuna mti mtakatifu tena wala ng'ombe mtakatifu. Leo si jana.

Mimi huko kwenye vyama nishatoka.

Haijalishi ni nani anasafisha huo uozo.

Kikubwa kinachoogopesha zaidi ni kuona ni jinsi gani ambavyo tulikaribia kuwa 'a failed state'.

Inavyoonekana ni kana kwamba kila mtu mwenye mamlaka fulani alikuwa anajifanyia tu mambo atakavyo utadhani hakuna serikali na dola.

Tunapenda kujisifia kuwa sijui tuna amani na blah blah zingine kama hizo....hiyo amani ina faida gani kama nchi ilikuwa imeoza hivi?

Shaking my head!!!!
 
Naona leo ukwenye mada husika!
Ni pale tu impunity itakapo kuwa siyo ya njia mmoja!.
njia na hatua ya JP na Pm wake ni one man show! Leo hii ni aibu kuwaona Yona na Mramba wakifagia barabara huku 11 bilioni zimeliwa na hawajaturudhishia hata senti.

Raisi mwenye Impunity kufanikiwa ni kazi! Ni pale tu uwanja wa kuwajibishana unapokuwa sawa mbele ya Haki ndipo nidhamu na imani inapojengeka! Ni kweli Raisi msafi anaweza kupunguza tatizo la ufisadi lakini kwa kiwango ndogo sana!

Si wanasema sheria imetekelezwa; Magufuli angeingilia kati na kutaka waendelee kifungoni au alazimishe watu warudishe fedha (ambayo haikuwa hukumu ya mahakama) unajua mngesema nini? ' anaingilia mahakama'. Sasa, binafsi sijapenda kabisa hili la kina Yona lakini bado linathibitisha tu bado kuna watu wanaishi jana. Suala hili ni la Jaji Mkuu na wenzake kuangalia kama kuna favors fulani zilipita huko.. siyo suala la Magufuli.
 
Hii nchi ilikuwa imeoza kabisa.

Na huu uozo ambao sasa unaanza kujitokeza ni indictment kubwa sana dhidi ya CCM na serikali zake.

Wasiwasi wangu ni kuna watu ambao ndo wamechangia kuuleta huo uozo lakini hawataguswa kabisa.
Tulisema, tukaonya, tukakataa kuwa Jakaya Mrisho Halfani Kikwete hafai kuwa Rais. Benjamin Mkapa alikuwa na misimamo thabiti ya kutotaka Jakaya awe Rais. Watanzania walipofuka macho. Ikawa kila ukitaja uovu wa Jakaya na udhaifu wake hueleweki na unaonekana adui. 89% ya Watanzania wakampa kura. Pale ndipo tulipoiangusha nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe. Hatuna wa kumlaumu. Ujinga na upumbavu wetu umetufikisha hapa. Haya maisha tuliyachagua wenyewe
 
Naona leo ukwenye mada husika!
Ni pale tu impunity itakapo kuwa siyo ya njia mmoja!.
njia na hatua ya JP na Pm wake ni one man show! Leo hii ni aibu kuwaona Yona na Mramba wakifagia barabara huku 11 bilioni zimeliwa na hawajaturudhishia hata senti.

Raisi mwenye Impunity kufanikiwa ni kazi! Ni pale tu uwanja wa kuwajibishana unapokuwa sawa mbele ya Haki ndipo nidhamu na imani inapojengeka! Ni kweli Raisi msafi anaweza kupunguza tatizo la ufisadi lakini kwa kiwango ndogo sana!

Na inategemea huyo rais ameingizwa na akina nani na hao waliomshabikia wana mikono misafi kiasi gani!!!!

Ndio maana juhudi hizi baada ya siku mbili zinaonekana ni usanii....

Huyo Magu aliyelipiwa mabango nchi nzima na akina HSC leo imejifilisi na kufungua kampuni mpya hakuna kinachoendelea!!!

Zaidi ya chuki... Visasi hakuna jipya....
 
Ina maana huu uozo umeanzia wakati wa Kikwete?

Nasita kuamini aisee....
 
Mimi huko kwenye vyama nishatoka.

Haijalishi ni nani anasafisha huo uozo.

Kikubwa kinachoogopesha zaidi ni kuona ni jinsi gani ambavyo tulikaribia kuwa 'a failed state'.

Inavyoonekana ni kana kwamba kila mtu mwenye mamlaka fulani alikuwa anajifanyia tu mambo atakavyo utadhani hakuna serikali na dola.

Tunapenda kujisifia kuwa sijui tuna amani na blah blah zingine kama hizo....hiyo amani ina faida gani kama nchi ilikuwa imeoza hivi?

Shaking my head!!!!

You are very right; na hicho ndio kinanisumbua hata mimi. Hivi, nchi ilikuwa inafanyaje kazi? Kwa mfano, kama ile taarifa ya kuwa mtoto wa Kova ni miongoni mwa watu waliotumbuliwa kule kwenye makontena ni lazima ujiulize alikuwaje Mkuu wa Polisi wa Dar. Binafsi mojawapo ya mabadiliko ambayo ningependa sana yaje ni kuwa na chombo kama FBI hivi... I hope tunaelekea huko. NN, amani kwa mwenye njaa inamsaidia nini? Binafsi sijawahi kuamini kuwa tuna amani ya kweli; kukosekana kwa vita haina maana ni uwepo wa amani.
 
Kuna wana ccm waliochukulia hilo swala la Waziri kutuma SMS kama jambo la kitoto na kuishia kulitetea kwa Nguvu zote na pia Muhongo katoa taarifa kama Manyerere alivyolifikisha hapa jukwaani kwamba hilo swala halina uhusiano na wizara yake

Magufuli alikua sahihi alipomwambia Jk pale Lumumba siku alipokabidhiwa cheti cha ushindi kwamba ccm wamejaa wanafki
 
Kama ulivyoainisha, old/bad habits die hard... tulifikia pabaya sana..people commited crime with impunity!
Overhauling culture/utamaduni mzima wa corruption si kitu ya siku moja na Magufuli pekeyake hawezi...anahitaji msaada wetu sote... when it comes to fighting corruption, everyone is a stakeholder.

Absolutely; lakini mara zote watu wanafuata viongozi wao. Binafsi naamini kuna watu wataanza kuelewa tu kuwa sasa 'there is a new sherrif in town'. Bado wengine hawaamini hili; hata baadhi ya Mawaziri, so it seems.
 
Mwambie Magu atumbue majipu ya kivuko cha bagamoyo na vingine ambavyo vinaota kutu bila kufanya kazi ilhali vilinunuliwa kwa gharama kubwa....

Unafikiri hata akitumbua huko utakubali kuwa kumetumbuliwa; si utahamisha goli jingine. Magufuli anafanya kazi kwa kufuata vipaumbele vyake na bado zipo siku zinakuja wataguswa hata ambao hawakuwahi kufikiriwa kuguswa.
 
Naona leo ukwenye mada husika!
Ni pale tu impunity itakapo kuwa siyo ya njia mmoja!.
njia na hatua ya JP na Pm wake ni one man show! Leo hii ni aibu kuwaona Yona na Mramba wakifagia barabara huku 11 bilioni zimeliwa na hawajaturudhishia hata senti.

Raisi mwenye Impunity kufanikiwa ni kazi! Ni pale tu uwanja wa kuwajibishana unapokuwa sawa mbele ya Haki ndipo nidhamu na imani inapojengeka! Ni kweli Raisi msafi anaweza kupunguza tatizo la ufisadi lakini kwa kiwango ndogo sana!

Na inategemea huyo rais ameingizwa na akina nani na hao waliomshabikia wana mikono misafi kiasi gani!!!!

Ndio maana juhudi hizi baada ya siku mbili zinaonekana ni usanii....

Huyo Magu aliyelipiwa mabango nchi nzima na akina HSC leo imejifilisi na kufungua kampuni mpya hakuna kinachoendelea!!!

Zaidi ya chuki... Visasi hakuna jipya....
 
1. Mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya Rais J.P. Magufuli inapozidi kujipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kimfumo

2. Muhimbli ilitarajiwa uongozi mpya kuanza kuondoa kero ambazo si za lazima; hii siyo tu uongozi wa Muhimbili bali pia Wizara ya Afya; lakini inaonekana mazoea magumu. Bado watu wamekutwa tena wamejazana wodini kama vile wako kwenye behewa la Daraja la tatu wakielekea Bara. Hivi kweli bado hakuna mtu mwenye akili za 'kawaida' tu kuwa watu wanaohitaji huduma safi, salama na mazingira mazuri kabisa ya tiba ni kina mama na watoto - kwa sababu ya udhaifu (vulnerability) yao? Kama watu hawa wanashindwa kuliweka hili kama ajenda yao nambari 1 hivi huko kwingine watapanga nini? Kama inabidi kufuta posho na mishahara ya viongozi wote ili kina mama na watoto wetu wapatiwe huduma sahihi na bora basi na liwe hivyo; lakini hili halieleweki?

3.Waziri Mkuu Kassima "Tabasamu" Majaliwa ... karudi tena Bandari ambako nako akakuta madudu mengine 'mbeya' mmoja kiongozi wajuu tu ambaye aliamua kuwadokeza na hivyo kutaka kusaidia kuficha madudu huko.

Nakubaliana na wengine wote kuwa Waziri huyo akithibitika kweli ametuma ujumbe wa kumtonya mama Chuwa ili ajaribu kuvuruga ushahidi basi Magufuli hana jinsi; ni lazima amuondoe Waziri huyo bila kujali uwezo wake, ujiko wake, au sifa zake. Serikali hii haipaswi na haitakiwi hata kuuliza "mwenzetu ilikuwaje ukavuruga mipango ya waziri Mkuu".

4, Hii ni hujuma ya ndani (internal sabotage). Tena hili inapaswa lifanyiwe kazi mapema sana ili kuleta heshima na woga kwa viongozi wengine. Magufuli akipepesa macho tu na kujikwaa tu atajitengeneza udhaifu usio wa lazima.

5.Na katika kushughulikia ni lazima tuwatoe mfano wale wenzetu wote ambao tulidhani wanaijua leo lakini bado kifikra wametiwa pingu za jana na bado hawajaziachilia; k

Hadi hivi sasa hakuna majuto. MMM
Mkuu MMM nimeziweka hoja zako katika namba ili niweze kuchangia vema

Nianze na ulipomalizia, hakika kuna majuto. Kama Rais anaweza kwenda kusimamia 'ununuzi wa vitanda' siku 100 baadaye hakuna anayemwelewa, alipo anajuta! Na wananchi wanajuta.

Pili,nashukuru hoja namba 1 umetamka mfumo. Ni mfumo huo ndio unasababisha majuto nilivyoeleza. Niliwahi kusema, mkurugenzi si tatizo, lmfumo mzima uangaliwe kila mtu awajibike kuanzia wizara ya afya, hazina na ofisi nyingine zinazohusiana.

Leo hoja yangu inasimama wima licha ya kubezwa 'mfumo' ni dude gani.

Nilionekana hayawani, nilisimama na ninasimama na hoja 'watanielewa siku moja'

Tatu, hoja namba 3 ya 'mbeya' kuwajibishwa inaonyesha uhalifu katika mfumo wa kihalifu

Hao watu wa vipimo ni wa wizara ya biashara na viwanda, wanafanya kazi wizara ya uchukuzi na mawasiliano, hapa ni kitu gani kama si mfumo?

'Mbeya' alitumia nafasi ya mfumo wa kihalifu kumnusuru mwenzake

Katika hali ya kawaida, uchunguzi ungeshakamilika asubuhi na 'Mbeya' angebaki hadithi. Kwavile hili ni la 'sisi kwa sisi' litafumbiwa macho.

Ninakuhakikishia hakuna ''Mbeya'' atakayewajibishwa kwasababu ile ile ya kulindana.

Siku 100 zimeisha, kulindana 'sera ya chama' ipo pale pale. Hapa ndipo utaona Felia

Nne, hoja ya 'internal sabotage' ni ya kujitakia.
Huwezi kuwa na genge lililoachia vipimo kwa vijiti kisha ukalirudisha madarakani ukidhani ifisi akiondolewa mbugani na kuwekwa kwenye zizi anaweza kuwa kondoo mzuuri

Tuliona 'recycling ya viongozi' mvinyo wa zamani katika chupa mpya.Source ya Felia

Wenzetu wakasema ni kikosi cha 'infantry kikisaidiwa na Seal six' Tulikataa kata kata.
Leo yanaanza kudhihiri, ndani ya kikosi kilichosemwa ni mahiri wapo wasaliti

Tano, kama mheshimiwa hatatoa mfano mbele ya safari itakuwaje? Majuto au Felia !
Wapi 'walk the talk'
 
Unafikiri hata akitumbua huko utakubali kuwa kumetumbuliwa; si utahamisha goli jingine. Magufuli anafanya kazi kwa kufuata vipaumbele vyake na bado zipo siku zinakuja wataguswa hata ambao hawakuwahi kufikiriwa kuguswa.

Hahahahahaaa aibu yako we kizee kinafiki ona ulivyojibú kwa aibu!!!

Ktk wizara iliyoongoza kwa uzembe ni ujenzi na unajua hii inareflect nn

This time needs smart people na hao smart people hakuna zaidi ya kutafuta sifa tu!!!

Huko muhimbili mbona ni yale yale?

Walugaluga mnaamini mabadiliko ni kufukuza na kubadilisha sura!!

Na mabadiliko inategemea yanaletwa na nani si hawa waliokuwa sehemu ya uchafu!!!

Mwambie msukuma mwenzio atumbue na jibu la uuzaji wa nyumba za serikali!!!

Huu ndo mwisho wa unafiki wako
 
Back
Top Bottom