Wanaohama Vyama Wataendelea kuhama

Wanaohama Vyama Wataendelea kuhama

Hizzo

New Member
Joined
May 22, 2020
Posts
1
Reaction score
3
Nimekuwa nikifuatilia hamahama ya wanasiasa na kila anayehama amekuwa akitoa sababu mbalimbali. Kila mtu ana haki ya msingi ya kujiunga na chama chochote cha siasa anapovutiwa sera, katiba na Itikadi!!

Ukifuatilia wanasiasa wengi Tanzania waliohama vyama mara Nyingi wamekuwa hawana hoja au sababu za msingi za kufanya hivyo!

Historia inaonesha kuwa wanasiasa wengi waliohama vyama hawakufuata itikadi ya chama husika zaidi ya maslahi binafsi! Itikadi ni IMANI! Na ukiona mtu anakana Imani yake kwa vipande vya pesa hawezi kuwa kiongozi bora!!

Wanasiasa waanze kupambana kubadilisha mfumo au kama kitu hakiendi Sawa kwenye vyama vyao Ndio maana wako humo ndani! Wanawajibika moja kwa moja kubadilisha au koboresha mfumo uliopo hasa kwa kujenga ushawishi, hoja na kuandika mpaka ueleweke! Kuhama chama sio suluhisho! Maana hata huko unapohamia kuna mapungufu Mengi mno! Je ukiyakuta hayo mapungufu Utahama tena? The best way kama haujaona chama Chenye Itikadi ya mlengo wako ni kuanzisha chama chako halafu uangalie utakavyoshangaa!

Mfano mzuri ni Zitto Kabwe, alikuwa na ushawishi ndani ya Chadema, wafuasi wake akiwemo Prof. Kitila Mkumba, Samson Mwigamba, Anna Mghwira, Alberto Msando, leo hii wamemuacha Zitto peke yake na ACT wazalendo.

Leo tunaambiwa ndani ya vyama kuna unyanyasaji wa kijinsia na kingono tena na sio watoto! Walikuwa wapi kuwa mfano miaka yate minne wakiwa wabunge hawakutoa taarifa mbaya hivyo!

Wengi wanasema kuna matumizi mabaya ya fedha! Lkn CAG hakuainisha hayo kwenye taarifa yake! Unasema Mwenyekiti anaongeza chama kibabe! Tujiulize Kauli za Mwenyekiti wa Ccm kwa wanachama wake kuwa walioshangilia wanaimani na Lowasa (2015) angekuwa yeye Mwenyekiti nusu ya wajumbe wasingerudi! Mwenyekiti anafuatilia hata simu za wanachama wake! Leo atleast wewe unapewa ujasiri wa kumsema vibaya Mbowe hadharani! Huwezi kufanya hivyo ndani ya CCM.

Mwisho, lazima tukubaliane kuwa ndani ya Chama au any institution lazima kuwe na Nidhamu kwa wanachama! Hata kama haukubaliani na wajumbe walio wengi ndani ya kikao halali!! Collective responsibility ni lazima uunge Mkono na kuadvocate maamuzi yaliyopitishwa na chama!
 
Akina nani jamani waliohama chama kwa sababu za kunyanyaswa kingono? Msaada please!
 
Demokrrasia iliyopo CDM hata ndani ya CCM haipo kamwe...jaribu kufikiri MTU anatoa kashfa za Uongo kwa Mwenyekiti wake bila bughudha yoyote ile hali ambayo ndani ya CCM huwezi ona kitu kama hicho....

Wanajidai wanataarifa za matumizi mabaya ya fedha kumshinda hata CAG...

Wanataarifa za Unyanywasaji wa Kijinsia wakati Madawati ya Jinsia yako kila mahali...

Kwanini wanakubali kujidhalilisha na kulishwa matango pori na hao wanaojidai wema kwao huku wakisahau walivyowatesa toka 2015?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo yashatokea tokea kurudi kwa vyama vingi vitakuwepo na kuendelea kuwepo. Kwasababu wapinzani wa ccm sio chama bali ni wananchi walio ichoka ccm.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Nimekuwa nikifuatilia hamahama ya wanasiasa na kila anayehama amekuwa akitoa sababu mbalimbali. Kila mtu ana haki ya msingi ya kujiunga na chama chochote cha siasa anapovutiwa sera, katiba na Itikadi!!

Ukifuatilia wanasiasa wengi Tanzania waliohama vyama mara Nyingi wamekuwa hawana hoja au sababu za msingi za kufanya hivyo!

Historia inaonesha kuwa wanasiasa wengi waliohama vyama hawakufuata itikadi ya chama husika zaidi ya maslahi binafsi! Itikadi ni IMANI! Na ukiona mtu anakana Imani yake kwa vipande vya pesa hawezi kuwa kiongozi bora!!

Wanasiasa waanze kupambana kubadilisha mfumo au kama kitu hakiendi Sawa kwenye vyama vyao Ndio maana wako humo ndani! Wanawajibika moja kwa moja kubadilisha au koboresha mfumo uliopo hasa kwa kujenga ushawishi, hoja na kuandika mpaka ueleweke! Kuhama chama sio suluhisho! Maana hata huko unapohamia kuna mapungufu Mengi mno! Je ukiyakuta hayo mapungufu Utahama tena? The best way kama haujaona chama Chenye Itikadi ya mlengo wako ni kuanzisha chama chako halafu uangalie utakavyoshangaa!

Mfano mzuri ni Zitto Kabwe, alikuwa na ushawishi ndani ya Chadema, wafuasi wake akiwemo Prof. Kitila Mkumba, Samson Mwigamba, Anna Mghwira, Alberto Msando, leo hii wamemuacha Zitto peke yake na ACT wazalendo.

Leo tunaambiwa ndani ya vyama kuna unyanyasaji wa kijinsia na kingono tena na sio watoto! Walikuwa wapi kuwa mfano miaka yate minne wakiwa wabunge hawakutoa taarifa mbaya hivyo!

Wengi wanasema kuna matumizi mabaya ya fedha! Lkn CAG hakuainisha hayo kwenye taarifa yake! Unasema Mwenyekiti anaongeza chama kibabe! Tujiulize Kauli za Mwenyekiti wa Ccm kwa wanachama wake kuwa walioshangilia wanaimani na Lowasa (2015) angekuwa yeye Mwenyekiti nusu ya wajumbe wasingerudi! Mwenyekiti anafuatilia hata simu za wanachama wake! Leo atleast wewe unapewa ujasiri wa kumsema vibaya Mbowe hadharani! Huwezi kufanya hivyo ndani ya CCM.

Mwisho, lazima tukubaliane kuwa ndani ya Chama au any institution lazima kuwe na Nidhamu kwa wanachama! Hata kama haukubaliani na wajumbe walio wengi ndani ya kikao halali!! Collective responsibility ni lazima uunge Mkono na kuadvocate maamuzi yaliyopitishwa na chama!
Wachumia tumbo ni wengi

Its not over until its over...
 
Shida hapa ni jinsi Mh m/kiti alivyotaka kutumia janga la corona kukiua chama ...kwa kulilia lockdown..!!!
 
Dunia mzima lockdown ipo jiulize Tanzania ni special.

Chunga afya yako,Corona ipo mpaka sasa hakuna dawa.Bahati mbaya corona ikikupata utaangaika mwenyewe na familia yako.

Usisikilize matamko ya wanasiasa ambao wapo zaidi kisiasa si kwaajili yako wewe na Mimi.
 
Back
Top Bottom