Wanaoandama na viongozi wanaopokea maandamano siku na nyakati za kazi ni wahujumu uchumi

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,969
Nchi yetu haiishi vituko na mambo ya kijinga bahati mbaya vyote vikifanywa na watu wanaoitwa wasomi ambao jamii ingewategea wawe mfano bora wa maamuzi na vitendo.

Muda si mrefu uliopita nchi ilikumbwa na upepo mbaya wa ujinga ambapo baadhi ya madiwani na wabunge waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi mkuu kwa gharama kubwa walijiuzulu nafasi zao kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi na kisha kurudi kugombea tena nafasi zile zile walizojiuzulu kupitia chama kingine kwa gharama kubwa ya mabilioni ya kodi za wananchi ambazo zingeweza kutumika kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba na madawati katika shule za sekondari ambapo sehemu nyingi utasikia taarifa za wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kukosa masomo na halmashauri husika kuanza kywageukia wananchi kwa michango ya ujenzi wa vyumba.

Walicho kifanya wabunge na madiwani hao ni hujuma kwa uchumi wa nchi ingawa kwa ujinga wa wanasiasa wanasherehekea kuwa eti ndiyo gharama ya demokrasia.

Sasa hivi kumeibuka wimbi la wafanyakazi wa umma kufanya maandamano siku na saa za kazi kwa madai ya kupongeza kikokotoo ambapo katika hali ya kushangaza maandamano yao yamekuwa yakipokelelewa na viongozi wa serikali ambao walipaswa kuhakikisha wafanyakazi hao wanakuwa katika sehemu zao za kazi ili kutimiza wajibu wao katika kujenga uchumi wa nchi. Hawa nao wanafanya hujuma kwa kutumia muda wa kuzalisha mali na kuhudumia wananchi kwenda barabarani na mabango kuandamana. Ni jambo la kushangaza hata kiongozi mkubwa aliyepiga marufuku maandamano na mikutano kakaa kimya simply because anasifiwa yeye. Je kesho yakitokea maandamano ya kupinga au kulalamika mfano wakulima waliokosa masoko na kulipwa mazao yao, wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu, vijana waliosoma lakini hawana ajira, wafanyakazi hao hao lakini sasa wakidai nyongeza za mishahara za kila mwaka na kuongezwa mishahara, mashoga nk atakaa kimya?! Utashangaa siku hiyo ndiyo itakuwa siku kuu ya kulipua mabomu na virungu huku madai.yakiwa wanaoandamana wanatumiwa na wanasiasa.

Mimi nawashauri hao wafanyakazi na viongozi wanaojipendekeza kwa kisingizio cha kuunga mkono kikokotoo waache kulihujumu taifa hili kwa kuacha kazi zao na kuingia mabarabarani siku na nyakati za kazi kwani hiyo ni hujuma ya wazi kabisa kwa uchumi wa nchi. Muda ni mali na kama tungepiga mahesabu kila dakika na saa ambazo kila mfanyakazi amepoteza kwenye maandamano hayo tutakuta ni mabilioni ya shilingi ambayo tungeyatumia kujenga madarasa lakini sasa tutawalipa wafanyakazi ambao hawakufanya kazi badala yake walikuwa wanazunguka na mabango barabarani huku viongozi nao wakitumia gharama kubwa ya misafara, posho, magari na mafuta kwenda kuyapokea maandamano hayo.

Nawashauri viongozi wanaooandaa maandamano hayo kupanga yafanyike baada ya saa za kazi yaani kuanzia saa 10.30 jioni au siku za mapumziko. Wakiona hiyo haifai waandike risala zao za pongezi na kumpekekea mhusika, kwa gharama zao walipie matangazo ya kupongeza kwenye redio na Tv, kwa pesa zao walipie matangazo ya kupongeza kwenye magazeti, watunge mashairi na nyimbo za kupongeza kisha warekodi na kumpelekea. Lakini kuchezea muda wetu wa kazi ambao tunawalipa ni marufukuuu!!! Tumesha ambiwa HAPA NI KAZI TU tuchape kazi laa sivyo kama hawana kazi za kufanya wapelekwe kusini kubangua korosho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom