Wananilazimisha nimpe jina Jezebeli

Wananilazimisha nimpe jina Jezebeli

Status
Not open for further replies.

IamMrLiverpool

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
4,738
Reaction score
7,083
Wana MMU habarini,

Iam very dissapointed nimezaa na girlfriend wangu anaitwa Yveti wazazi wake mmoja ni,mtanzania ila mama ake ni mnyarwanda na wazazi wake wote wanaishi rwanda(wana biashara zao) nilikutana,nae school of medicine sasa nimezaa,nae cha ajabu wazazi wake wanataka nimuite jina Jezebeli mtoto ana siku 14 bado tunazozana maana mimi sitaki hilo jina.

Maana lina mreflect mtu hatari sana kwenye bible ambaye alikua mwanamke katili muuaji anaejipenda for sure sijawai kuona mtu anamuita mwanae Jezebel kwa sasa hivi tumeamua kumpa jina baby kwa muda hadi tuafikiane ila wao hawataki kuchange mawazo.

Sasa naombeni mnishauri hivi ni mindset yangu tu kuhusu jina ama nipo sahihi nikubali hilo jina.
 
Aisaee... Samahani sana !! Mwanamke kabeba 9 months na kakuzalia kwa salama!! umeshindwa kuridhia ka jina tu !! kumradhi UKATILI siyo wa jina ila ni wako binafsi huo !! Badala ya kumzawadi G/F wako !! THINK...
 
Kiroho majina yana impact kubwa.

Nitakupa mifano miwili tu kutoka kwenye biblia:

1. Kumbuka namna Yakobo alipomkatalia mkewe Raheli kuhusu jina Benoni na badala yake akamwita Benyamini (Soma Mwanzo 35:18). Benoni ilimaanisha "Mwana wa huzuni/son of sorrow" wakati Benyamini ina maana "Mwana wa furaha/son of happiness."

2. Kumbuka pia mtu mmoja alibatizwa jina la Yabeshi na mama yake, kwa kuwa huyu mama alimzaa mtoto huyu kwa maumivu. Yabeshi ilimaanisha "Mwana wa maumivu." Hivyo huyu jamaa alipokuwa mtu mzima maisha yake yakawa ya huzuni na maumivu mpaka alipoutafuta uso wa Mungu, kumbe hakujua vilisababishwa na jina. (Soma 1 Mambo ya Nyakati 4:9-11).

Sasa, tukija kwa jina Yezebeli lina maana "binti wa baali/mungu sanamu" & ukienda kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana utaona lina reflect ukahaba. Ndio maana Yezebeli mke wa mfalme Ahabu alipenda kuabudu sanamu, kumbe jina lake lilimaanisha "binti wa baali."

Je! Wewe una amini katika nini? Chaguo ni lako.
 
Aisaee... Samahani sana !! Mwanamke kabeba 9 months na kakuzalia kwa salama!! umeshindwa kuridhia ka jina tu !! kumradhi UKATILI siyo wa jina ila ni wako binafsi huo !! Badala ya kumzawadi G/F wako !! THINK...

jina linabeba hitma ya MTU. Jezebel ni jina LA kishetani na kumpa mtoto jina hilo utakuwa umemuunganisha moja kwa moja na madhabahu za kuzimu
 
Wana Mmu habarini iam very dissapointed nimezaa na girlfriend wangu ni mnyarwanda anaitwa Yveti wazazi wake mmoja ni,mtanzania ila mama ake ni mnyarwanda na wazazi wake wote wanaishi rwanda(wana biashara zao) nilikutana,nae school of medicine sasa nimezaa,nae cha ajabu wazazi wake wanataka nimuite jina jezebeli mtoto ana siku 14 bado tunazozana maana mimi sitaki hilo jina maana lina mreflect mtu hatari sana kwenye bible ambaye alikua mwanamke katili muuaji anaejipenda for sure sijawai kuona mtu anamuita mwanae jezebel kwa sasa hv tumeamua kumpa jina baby kwa muda hadi tuafikiane ila wao hawataki kuchange mawazo sasa naombeni mnishauri hv ni mindset yangu tu kuhusu jina ama nipo sahihi nikubali hilo jina
Wewe ndiyo baba, hakuna maelezo Mengi, mpe jina linaloanzia na M kwani ni herufi yenye bahati na pia utakuwa kwenye historia ya kukumbukwa juu ya ushindi wa Dr Magufuli.
 
kwa kifupi tu. kaa na mama mtoto umweleze madhara ya kumwita mtoto jina ambalo lina maana mbaya. akikuelewa nivrahisi yeye kuwaelimisha wazaxi wake. usithubutu kumwita mtt jina usilojua maana yake. itamgharimu maisha yake. siku hizi kuna vitabu vingi vyenye majina na maana zake. tafuta kitakupa mwanga.
 
mwanamke hana mamlaka yoyote ya kutoa jina la mtoto mwenye mamlaka hayo ni mwanaume...rejea adam na eva pale eden adam ndo alipewa dhamana ya kutoa majina kwa viumbe vyote na si mkewe
 
Wasikurostishe shem watu wa kwetu ni wababe ww tia ngumu mpe hata jina la mama yako
 
Tatizo lako umemzalisha na hujamuoa, hapo ndio shida ilipo.

Ingekuwa umemuoa mamlaka yote yangekuwa juu yako ila kwa kuwa bado hujamuoa wazazi wake wanajiona bado wana mamlaka.

Kaeni chini mshauriane tu
 
Tatizo lako umemzalisha na hujamuoa, hapo ndio shida ilipo.

Ingekuwa umemuoa mamlaka yote yangekuwa juu yako ila kwa kuwa bado hujamuoa wazazi wake wanajiona bado wana mamlaka.

Kaeni chini mshauriane tu
Couldn't have said it better. So much wisdom right there.
 
Wewe ndiyo baba, hakuna maelezo Mengi, mpe jina linaloanzia na M kwani ni herufi yenye bahati na pia utakuwa kwenye historia ya kukumbukwa juu ya ushindi wa Dr Magufuli.

Mfyuuuuu jinga sana ww
 
Baba na mama ndo wanaamua jina la mtoto wao!!
Sasa wakwe zako wanakuwaje na nguvu zaid yenu!!!
Muite mwanao jina taaaaamu, soft na sweet
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom