Wananilazimisha nimpe jina Jezebeli

Wananilazimisha nimpe jina Jezebeli

Status
Not open for further replies.
Wana MMU habarini,

Iam very dissapointed nimezaa na girlfriend wangu anaitwa Yveti wazazi wake mmoja ni,mtanzania ila mama ake ni mnyarwanda na wazazi wake wote wanaishi rwanda(wana biashara zao) nilikutana,nae school of medicine sasa nimezaa,nae cha ajabu wazazi wake wanataka nimuite jina Jezebeli mtoto ana siku 14 bado tunazozana maana mimi sitaki hilo jina.

Maana lina mreflect mtu hatari sana kwenye bible ambaye alikua mwanamke katili muuaji anaejipenda for sure sijawai kuona mtu anamuita mwanae Jezebel kwa sasa hivi tumeamua kumpa jina baby kwa muda hadi tuafikiane ila wao hawataki kuchange mawazo.

Sasa naombeni mnishauri hivi ni mindset yangu tu kuhusu jina ama nipo sahihi nikubali hilo jina.

asije akawa Yveti Basso aisee.

Jesebel ni jina baya sana, mwanamke huyo alikuwa analala na kila mwanamme. akimpenda anamuita kufanya mambo.

tafta kifungu cha biblia uwape wasome
 
Wazazi wake wafanyabiashara...
Wanataka mtoto aitwe Jezebel...
Jezebel ni jina la kishetani...
Mtoto anatolewa kwa shetani...

Stuka!!!!!!!!!
 
Kama shida ni jina la kwenye Biblia mwite mtoto jina kama Rahel, Sara n.k kwani yapo mengi binafsi nalipenda sana jina la Abigail, mwite ABIGAIL
 
asije akawa Yveti Basso aisee.

Jesebel ni jina baya sana, mwanamke huyo alikuwa analala na kila mwanamme. akimpenda anamuita kufanya mambo.

tafta kifungu cha biblia uwape wasome

Yveti basso?????
 
Majina yana maana kubwa katika maisha yetu hapa duniani.Nimeshihudia watu wenye majina kama Shida,Mashaka,Masumbuko na kadhalika wamekuwa ana maisha yanayofanana na majina yao.

Mtazame Masumbuko Lamwai mpaka leo anasumbuka na maisha pamoja na kuwa na elimu kubwa,ujuzi mkubwa .....
 
Frederiko Unachokiamini Ndio Hicho, Zaidi Ameeleza Chosen Generation.
Kama Wewe Ungekuwa Mimi, Ningefanya Utaratibu Wa Kuongea Na Wazee Hao Kwa Azima Ya Kuwasadikisha Kile Ninachoamini Juu Ya Majina, Hususani Sifa Na Tabia Za Watu Wenye Jina La Jezebeli. Hali Hiyo Inaonesha Jinsi Hao Waze Walivyo Na Imani Tofauti. Waendee Kwa Imani Ya Kuwahubiri Na Kuwaonesha Kuwa Umekataa Mapenzi Yao Hayo, Kwa Ustaarabu Huo Na Ufanye Maombi Kwa Ajili Yao.
 
Au isije kuwa hao wanaopenda mtoto apewe hilo jina ni washabiki wakubwa wa kundi la muziki la Boyz II Men na ule wimbo wao wa Jezebel.
 
Wazazi wake wafanyabiashara...
Wanataka mtoto aitwe Jezebel...
Jezebel ni jina la kishetani...
Mtoto anatolewa kwa shetani...

Stuka!!!!!!!!!

Mimi pia nimewaza Kaunga yawezakana wanatumia nguvu ya ziada katika kufanya biashara maana mtu yeyoto anayeijua historia ya hilo jina hawezi kumpa mtoto hata mkimwombea bado nguvu ya jina itatenda kazi maana wamemmilikisha kwa shetani tayari
 
Last edited by a moderator:
inatia hasira sana pale wazazi wanapoingilia mahusiano ya watoto wao bila kualikwa kushiriki.hebu wawaache nyie na mwenzio mfanye maamuzi yenu wawili
 
Wewe na girlfriend wako chagueni jina zuri mwiteni Mtoto mi napendekeza mmwite Blessing kadi ya klinick na cheti cha kuzaliwa liandikwe hilo jina mlipendalo msiwaambie watakua wanasikia tu Mtoto anaitwa jina mlipendalo nyie over
 
Kataa, hata kulingana na mila nyingi za kiafrika jina la mtoto wa kwanza hutolewa na upande wa baba, Over!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom