Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,641
- 47,664
Wakati dingi anatwambia hii kauli mimi na mdogo wangu, hapo alikuwa amevimba kwa hasira akiwa hana cha kufanya.
Nakumbuka enzi hizo na mdogo wangu, mimi nikiwa kidato cha nne, mdogo wangu akiwa cha 3. Tulikuwa watundu japo sio watukutu. Kuna siku tuliondoka home bila kuaga, alaf kuna kazi tuliambiwa na mshua tuifanye ila tukasahau.
Tulirejea nyumbani majira ya saa kumi na moja kosoro jioni, njaa kali hatukuwa tumekula kitu tokea asubuhi. Kufika home, mzee alitugombeza sana, alafu akasema kwavile tumeona tumeshakua basi hataki tena kutuona nyumbani, akatusukumizia nje kisha akafunga mlango. (Hapo kumbuka tuna njaa ya hatari na home hawakutuwekea chakula siku hiyo).
Tulikaa pale nje, njaa kali. Nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na midizi, na uzuri kulikuwa na ndizi mbivu zimeiva, faza alisema angezitoa jioni. Tulipoona mkungu bado upo, tukakubaliana na dogo tule zile ndizi. Dogo akaenda kufunga ule ule mlango ambao baba alitufungia kwa ndani, dogo akaufunga kwa nje ili kumdhibiti mzee endapo atataka kutoka.
Tulijitahidi sana kuukata taratibu ule mgomba walau usitoe kishindo chochote, ila dingi kwavile alizijua akili zetu, naona machale yakamcheza, ghafla akaja. Kufika mlango anakuta mlango umefungwa kwa nje, kuja kuchungulia kwenye dirisha la jikoni anatukuta vidume tunaushambulia ule mkungu bila wasiwasi.
Alitwangalia pale dirishani, mwishowe akatwambia "Na nyie mtazaa tu"
Siku ikaisha, miaka mingi ikasogea. Sasa hivi nina mtoto wa kiume mkubwa tu, umri miaka 5 anaishi kwa babu na bibi yake (wazazi wangu). Kwavile mimi niko mbali, huwa nina kawaida ya kumpigia simu na kuongea nae mara kwa mara.
Last week nimekaa sehemu na rafiki zangu, nikaona ngoja nimpigie baba ili niongee na mwanangu, nikaongea nae vizuri tu huku nikijaribu kumuuliza mambo kadhaa kadhaa ya shule.
Katika kuendelea kuuliza, ghafla dogo akaniambia "BABA UNAMASWALI SANA , PUMBAVU WEE" kasauti kake kalisikika na wote waliokuwa karibu na mimi pale, na upande wa pili nikasikia bibi yake anakachapa. Nikakata simu.
Baadae faza akanipigia simu, akaniambia "mwanangu nilikwambia na wewe utazaa tu". Sikumjibu,nilikaa kimya tu, then tukaendelea na story zingine.
Dah, haya mambo aisee.
Analyse.