Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,972
- 22,933
Wanandoa wenye furaha katika ndoa yao ni watu wanaoishi kwa ukaribu sana. Hapa sizungumzii kuhusu wale wa 'piga makalio kisha tufanye ngono.' Bali namaanisha wale wa kugusana kimwili mara kwa mara - kupigana mabusu shavuni, kugusana kidogo begani na kupeana raha zote pasipo masharti.
Wanandoa wenye furaha hupongezana kila siku. Hupeana mahaba kwa kutamkiana maneno rahisi kama vile.... "Wewe ni mtamu sana," au "Unaonekana mzuri," au "Chakula cha jioni kilikuwa kitamu sana" kiukweli , hufanya tofauti kubwa katika ndoa kwa kufurahishana wakati wote.
Wanandoa wenye furaha huombana msamaha wanapokosea. Wanaendelea kusameheana. Na wanaonyesha shukrani. Wanathaminiana. Hawachukuliani kawaida.
Wanandoa wenye furaha hupanga bajeti ya mapato yao pamoja. Wanandoa salama hawana siri za pesa kati yao. Na hawaruhusu mtu wa tatu wakiwemo wakwe zao kuingilia ndoa yao ili kuwagawanya.
Wanandoa wenye furaha hutumia wakati wa mapumziko pamoja. Wanatoana out kupata vinywaji ama chakula pamoja. Pia wanaruhusu wenzi wao kukaa na marafiki zao. Mtu aliye salama hamtengi mwenza wake kutoka kwa jamii.
Jitahidi uwe wanandoa mwenye furaha.
Ubarikiwe.