Wananchi wa Jimbo la Fuoni lililopo wilaya ya Magharibi B mkoa wa Mjini Mgaharibi, Zanzibar wameendelea kujitokeza kushiriki katika uchaguzi mdogo wa Mbunge katika jimbo hilo.
Uchaguzi huo unafanyika hii leo Desemba 30, 2025 kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Abbas Ali Hassan Mwinyi aliyefariki mwezi Septemba mwaka huu.
Msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya hiyo, Miraji Mwadin Haji ameeleza kuwa hali ya kiusalama katika vituo vyote 36 vya uchaguzi ni shwari na wananchi wameendelea kujitokeza kushiriki uchaguzi huo.