Wananchi wavamia mali za watuhumiwa

Huduma

Member
Jan 26, 2008
68
1
Hebu thibitisheni habari kama hizi ni kweli. Inaelezwa ya kwamba wananchi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Pwani na Dar es salaam wanavamia mashamba, viwanja, nyumba na mali nyingine za watuhumiwa wa Ufisadi na wale wa EPA?


Je, haya ni kweli au uzushi tu?
 
Hebu thibitisheni habari kama hizi ni kweli. Inaelezwa ya kwamba wananchi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Pwani na Dar es salaam wanavamia mashamba, viwanja, nyumba na mali nyingine za watuhumiwa wa Ufisadi na wale wa EPA?


Je, haya ni kweli au uzushi tu?

Si kweli. Labda kama ndio una hamasisha basi ngoja tuje tuvamie.
Unajua sasa hivi kila mtu anazungumza lake kuhusiana na hawa mafisadi maana watu wamewachoka sana. Sijui kama wao mafisadi na familia zao wanafahamu hili!
 
Naona tunaelekea Thailand. Kama hili likianza hakuna wa kulizima. Jamani thibitisheni kama ni kweli.
 
Unajua ni rahisi sana watu kuvamia shamba na kuvuna kilichopo kisha kuingia mtini. Hii inawezekana
 
Kuhamasisha watu kuvunja sheria ni kosa.Kesi ziko mahakamani si vizuri kufanya vurugu.Ustahamilivu unatakiwa katika masuala haya.
 
Ukiangalia wananchi walivyokuwa wanawazomea Mramba na Yona ,sitashangaa kusikia wanavamia mali za hawa mafisadi waliopelekwa mahakamani; watu wanahasira sana kwani wanaumia na ugumu wa maisha na wamezinduka nakujua kuwa moja ya vyanzo vya taabu zao ni huu ufisadi ulioshamili; nakumbuka wakati wa sakata la Richmond kushuhudia mtoto wa Lowassa akinyang'anywa trolley na vijana lililojaa bidhaa akitoka nalo supermarket!! Wananchi wanahasira sana.
 
Wamekwiba sana hao,kama kweli waendelee kupora na kuwatia hasara
 
Back
Top Bottom