Wananchi wanyunyuziwa sumu na ndege mbeya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wanyunyuziwa sumu na ndege mbeya.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kwame Nkrumah, Feb 4, 2012.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  [h=3]MRADI WA KAPUNGA HALI NI TETE[/h]  Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
  Hali ya wakazi wa Kijiji cha Kapunga, wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya imeendelea kuwa tete, baada ya mwekezaji wa mashamba ya Kapunga rice project kumwaga sumu ya kuua mimea, kwa kutumia ndege.
  Mnamo Januari 12 hadi 14, mwekezaji kwa kutumia ndege ya kunyunyizia dawa alimwaga sumu hiyo katika mashamba yake, pia na katika mashamba ya wananchi katika eneo linalofahamika kwa jina la Mpunga mmoja, na kusababisha wakulima zaidi ya 140, wanaomiliki zaidi ya hekari 4,000 ya mimea kuathiriwa na sumu hiyo.  Tukio hilo limethibitishwa na Meneja Mkuu wa shirika la Kapunga Rice Project Bwana Wally Vermaak, ambaye amesema huyo ni mwanzo tu na wataendelea kumwaga sumu hiyo.  Mwekezaji wakati anamwaga sumu hiyo hakutoa tahadhari wala matangazo kwa wakazi wanaozunguka eneo hilo, hali iliyopelekea sumu hiyo kuwaathiri watu waliokuwa mashambani ambapo mpaka sasa afya zao ni tete kutokana miili na miguu yao kuathiriwa na sumu hiyo na kusababisha baadhi yao kushindwa kutembea.  Baadhi ya wananchi walioathiriwa na sumu hiyo wakati ndege ikimwaga mashambani na kushuhudiwa na mwandishi wa mtandao huu ni pamoja na Bwana Gaidon Peter Ngogo (54), Jailo Esau (22), Jackson Mwandemange (52), Catherina Shipela (50), Edda Ngosha (35), Julius Isega(50), Ramadhan Nyoni (52) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho na Raphael Moreli (44) ambaye ni Afisa mtendaji wa kijiji hicho.  Hata hivyo Wizara ya Kilimo ilituma Tume ya uchunguzi na utafiti wa udongo na kutoka mikoa ya Arusha na Dar es salaam, ikiwa na wajumbe wafuateao Bwana Geophrey Mwamengo, kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mbarali na Kidemi Peter, Julius Emily Paulo Tarimo, E. Macha, Alex Mlowe ( kutoka TPRI - ARUSHA) na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbarali B. J Chatanda, ambapo walianza kazi Januari 24 mwaka huu, kwa kuchukua sampuli za udongo na mimea kwa ajili ya kufanyia uchunguzi.  Katika kikao hicho mwekezaji aliendelea kudharau na kutamka kuwa ataendelea kumwaga sumu katika mashamba mengine na kwamba maeneo hayo mengine ni mali yake.  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro amekiri kupokea malalamiko ya wakulima hao na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na Serikali kuu, hivyo wakulima waendelee kuwa na subira mpaka pale serikali itakapotoa tamko.  Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Ramadhan Nyoni, amesema kuwa kijiji chake kimeendelea kupokea vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa mwekezaji huyo vikiwemo vya kuua mifugo, kuteka nyara magari ya wanakijiji kama vile gari namba T 994 AJB aina ya Canter mali ya Bwana Osward Mbeyale (39), Janauri 26, mwaka huu na hivyo wananchi wa kijiji hicho kulazimika kutumia nguvu na kulikomboa gari hilo.  Wakati huo huo wanakijiji wameshindwa kufanyashughuli za maendeleo ya kijiji hicho kutokana na mwekezaji huyo kufunga barabara za kutoka na kuingia kijijini hapo, hali inayosababisha kudhoretesha maendeleo na wakati mwingine wanawake wajawazito kujifungulia njiani kabla ya kufika hospitali.  Wananchi hao wameiomba Serikali kulishughulikia suala hilo haraka ili kuwawezesha kufanya shughuli zao maendeleo ya kijiji na yao vile vile kuepukana na manyanyaso


  source: MBEYA YETU BLOG.
   
 2. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCM= Ally Chemical wa Iraq enzi za Sadam Hussein:pole sana Filikunjombe
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  nasikia doria one ameenda kuswali swala ya maulidi mbeya......wakimuacha bila kumpopoa nitawashangaa sana.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Uwekezaji ni ukoloni tu. Ukoloni huu ni mbaya kuliko ule ukoloni wa zamani. Zamani wakoloni walikuja na wakakumbana na resistance ya mababu zetu wakitumia mikuki na mundu. Bahati mbaya babu zetu wakashindwa lakini wakoloni hawakupewa nchi kwenye sahani ya dhahabu. Leo hii ni sisi tunaenda kuwaomba waje. Nakumbuka maneno yasemayo " kuna utumwa wa kutumwa na utumwa wa kujituma; utumwa mbaya ni ule wa kujituma"
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sasa naona sumu imehamia kwa wananchi
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Hainijii akilini mtu mmoja tena mgeni kuwahangaisha maelfu kwenye nchi yao. Ni lazima wenyeji watakuwa na tatizo kubwa sana. Unyanyasaji wa aina hii una njia zake za dhararua za kushughulikia....
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hivi ni sumu kama sumu proper au ni dawa ya kuuwa magugu? Tunahitaji clarification
   
 8. P

  Percival JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,566
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Acheni upuuzi , Jembe la mkono haliwezi kulisha taifa na kutoa mazao ya biashara ya kutosha. Ni muhimu kupata na kukaribisha wawekezaji sababu wanazo raslimali na ufundi. Karibuni sana wawekezaji lakini maslahi yawe yetu sote .
   
Loading...