Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
Taifa la Tanzania limekumbwa na hali ya ukame ambayo imesababisha taarifa za kuyumba kwa hali ya chakula nchini. Maeneo kadhaa yaliripotiwa kuwa na uhaba wa chakula na matamko mbalimbali yalitolewa na serikali kuhusu hali hiyo.
Taasisi ya TWAWEZA kupitia Sauti za Wananchi, ambao hukusanya maoni ya wananchi kupitia simu za mkononi kuhusu kinachoendelea nchini katika nyanja zote za maisha, inakuletea Ripoti ya maoni ya wananchi kuhusu hali ya uhakika wa chakula nchini.
Ripoti hiyo ambayo itazinduliwa kesho tarehe 01.03.2017 kuanzia saa 5 asubuhi hadi 7 mchana pale Makumbusho ya Taifa (Posta, Mkabala na chuo cha IFM), itabainisha maoni ya wananchi. Je wananchi wana maoni gani kuhusu hali ya chakula nchini? Je wana uhakika wa kuwa na chakula kulingana na mahitaji yao?
Unataka kujua Wananchi wanasema nini na utafiti umebaini nini? Majibu tutayapata kesho.
Ungana nasi hapo kesho kwani JamiiForums itakuletea moja kwa moja 'LIVE' yanayojiri kwenye uzinduzi huo.