Wananchi wamshukia Waziri Muhongo

Wananchi wamshukia Waziri Muhongo

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
*Ni kwenye kongamano la wazi
KONGAMANO la wazi la Wizara ya Nishati na Madini jana liligeuka kuwa mwiba kwa Waziri Profesa Sospeter Muhongo baada ya kusisitiza msimamo wa serikali kuhusu gesi ya Mtwara.

Profesa Muhongo ambaye alikuwa akiwasilisha mipango ya uhakika ya upatikanaji wa umeme nchini aliwalaumu wanasiasa kuwa kikwazo katika mradi huo kwa kuwachochea wananchi kuandamana. Alisema wananchi wa Mtwara hawana nafasi tena ya kusikilizwa kwa vile walipewa elimu mara kadhaa lakini kutokana na kulaghaiwa na wanasiasa kwa ujira wa Sh 20,000 wamekuwa wakiandamana na kupinga mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

“Maandamano ya wananchi hayawezi kuitingisha Serikali, hatuwezi kusimamisha mradi kwa sababu tumegundua ni ujinga wa baadhi ya wanasiasa kutaka taifa likubaliane na ujinga wao.

“Ni upuuzi mkubwa kudai gesi ni mali ya mikoa ya kusini, ni upuuzi kwa mtu kusema wanamtwara wanahoja eti wakasikilizwe.

“... ni upuuzi tena kwa mwanasiasa kusema ajira kwa vijana ni bomu, nasema hakuna bomu litakalolipuka labda katika familia yake.


“Pia ni upuuzi tena Serikali kuwasikiliza wanasiasa wanaopiga kelele huku hawana takwimu wala njia mbadala ya kupata umeme wa uhakika.
“Nasema kwa kuwa tumewajua wanaopinga mradi tutawashughulikia na hatutaacha kutandaza bomba na ole wao wajaribu, watajuta.

“Tunataka wananchi vijijini wapate umeme hadi asilimia 50 siyo tena leo ni asilimia saba tu wanaopata umeme. Lazima miradi saba itekelezwe ndani ya miaka 20 tuliyojipangia. “Ni jana (juzi) Rais wa Marekani, Barrack Obama ameondoka nchini ametoa dola bilioni saba kusaidia kupata umeme megawati zaidi ya 10,000 na sekta binafsi zikitoa bilioni tisa,”alisema. Baada ya kutoa kauli hiyo kulizuka malumbano kati ya washiriki Profesa Muhongo na wakati mwingne washiriki wenyewe kwa wenyewe.

Mshiriki aliyejitambulisha kwa jina la Said Mohamed Manora kutoka mikoa ya Kusini alidaiProfesa Muhongo amewatukana, amewatenga na kutowathamini wananchi wa mikoa hiyo. Manora alisema Mkoa wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa iliyotelekezwa huku barabara zikijengwa kwa kusuasua tofauti na ilivyo kwa Kanda ya Ziwa. Alisema Profesa Muhongo ameonyesha dharau kwa wanamtwara akisema anapaswa kutafuta historia yao badala ya kuendelea kuwapuuza.

Hata hivyo Profesa Muhongo aliendelea kutoa msimamo wake kwamba hakuna muda tena wa kuwasikiliza huku akisisitiza gesi ni mali ya Watanzania. “Narudia kusema itakuwa ni upuuzi gesi hiyo kudai ni yao, mbona hamuuzi korosho huko Mtwara na nani kawaelekeza kuna soko Dar es Salaam,”alisema.

Wakati anajibu ‘mapigo hayo’ kulitokea makundi mawili tofauti ambayo yalinyoosheana vidole; kundi moja likiwa upande wa Profesa Muhongo na jingine likimuunga mkono mshiriki aliyeibua hoja. Kitendo hicho kilivuruga utulivu katika chumba cha mkutano huo. Hata hivyo iligundulika kuwa washiriki wengi waliomuunga mkono Manora walikuwa ni wa kutoka mikoa ya kusini na walioungana na Waziri ni watumishi wa wizara hiyo na wale wanaomba kupatiwa miradi ya umeme.

Malumbano hayo yalisababisha washiriki wengi kutoka nje ya ukumbi huku majadiliano ya makundi yakitawala. Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliachim Maswi alimuunga mkono Waziri wake na kuema Serikali haiwezi kukubalina na kile kinachodaiwa na wanamtwara kwa vile kitaligawa taifa na ni hatari.“Kama hamfahamu naomba niwaeleze kwamba wakati wanamtwara wanadai gesi yao, tulipokea vishawishi vingi kutoka mkoani Mara, kama mnavyojua mimi natoka huko na hivo hivyo waziri.

“Wakurya wenzangu walikuwa wakisema tukubali gesi iwe ya Mtwara na wao dhahabu iwe yao, walisema tukiruhusu hivyo wawekezaji wote watachinjwa haraka hata kabla ya kutoroshwa hapo,”alisema. Kabla ya tafrani hiyo, Profesa Sospeter Muhongo alisema mipango muda mfupi iliyokuwa ikipangwa awali na Serikali ndiyo iliyosababisha kutopatikana maendeleo ya haraka.

Alisema mipango ya muda mfupi ndiyo imeleta vitendo tunavyoshuhudia hivi sasa kwa Watanzania kama kubomolewa nyumba zao au kuhamishwa katika makazi yao jambo ambalo ni hasara.“Kama taifa lazima liwe na mipango ya muda mrefu na siyo tena mipango ya miaka michache ambayo inaleta hasara kutokana na mabadiliko. “Suala la mipango ya muda mfupi halipo katika wizara moja la hasha, karibu wizara zote, hii ni tatizo kwa viongozi wengi, tunapaswa kuiga mipango ya mataifa mengine.

Tanzania itapiga hatua tu tutakapopanga mipango ya muda mrefu kwa kuangalia dunia inakwendaje na kuweka vipaumbele kwani ifikapo 2030 nishati na maji vitakuwa bidhaa adimu maradufu,”alisema. Profesa muhongo alisema muda umekwisha wa maneno na kilichobaki ni vitendo kwa kuwaajibisha viongozi katika wizara yake kama hawawezi kufanya kazi kwa kiwango cha kimataifa.

Alisema kwa muda aliokaa ndani ya wizara hiyo ameweza kuwafukuza kazi watumishi waliogundulika kujihusisha na rushwa, wizi, utendaji mbovu na ubabaishaji na bado wengine wanafuatiliwa kwa ukaribu.“Ndani ya wizara ya yangu nasema watumishi wengi watapukutika, siwezi kukaa na watu ambao hawafanyi kazi kwa uadilifu na kiwango cha kimataifa, binafsi najiamini na ninaweza,” alisema.

Profesa Muhongo alisema Tanzania haiwezi kutegemea mabawa ya kizamani yanayosubiria mvua na badala yake tunapaswa kuwa na njia mbadala ya kupata nishati ya uhakika. Alisema kuwa tayari wizara imeweka kipaumbele ya umeme ni kutumia gesi asilia, makaa ya mawe, maji, jua, upepo na joto ardhi. Ifikapo Julai 2014 bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam litakuwa limekamilika, alisema.

My: Take Sospeter Muhongo Ni Hatari Kwa Usalama Wa NCHI. Atimuliwe Mara Moja
 
Ni mwendelezo wa uvunjaji wa katiba yetu ibara ya tisa.
 
Huyu na yule wa wapigwe tu ni sawa sawa tu... wanaleta upumbavu, hao wa Mara Mbona mashine za kuchimba dhahabu zimejengwa Mara..?? Je wangekubali mitambo iliyojengwa Mara ingejengwa Dar halafu wasafirishe udongo wenye dhahabu (ORE) kuja Dar..??
 
huyu jamaa si mwanasiasa -- nimeamini kabisa, na ndiyo maana position kama hizi (za uwaziri) huwa hawapewi watu wasio wanasiasa.
 
Huyu waziri ana ubabe wa kijinga sana.....yeye anaona kuwasikiliza watu wa mtwara ni upuuzi? yeye mbona anataka kusikilizwa,kila mtu ana haki ya kusikilizwa na sio kubaguana kwa staili hii,binafsi ningependa kuona mikoa ya kusini inanufaika na hiyo gesi,ningependa kuona Nchi inapanuka katika maendeleo na sio dar peke yake.
 
Duh...Muhongo 'kichwa ngumu' aisee, yaani anakutukana kwa jina la 'serikali', ina maana serikali siku hizi inawaita waTanzania wote wenye hoja au mtazamo tofauti kuwa ni 'wapuuzi'!? And to top it off, hata kuwasikiliza tu (na si kukubali maoni yao) ni upuuzi! Kama hivyo basi wapuuzi tupo wengi kweli kwa kuwa na mtazamo tofdauti na serikali yetu hii fisadi, kiziwi, kipofu, na ya kibeberu!
 
Ni binadamu wachache sana wanaoamini kuwa anachokiamini ni tatizo kwa watu wengine na hii ndio sababu kubwa ya vita duniani. Busara ya Muhongo inamuongoza hivyo hawezi kuliona tatioz la Mtwara kwa uhalisia wake, anayoyasema Muhongo ni maneno ya zamani zote ambazo watanzania huwa wanaambiwa kuwa hiki ni chetu wote lakini Dar na Kaskazini ndio zinafaidika. Inataka tafakari ngumu kupata ufumbuzi wa busaara mbili hizi
 
Duh...Muhongo 'kichwa ngumu' aisee, yaani anakutukana kwa jina la 'serikali', ina maana serikali siku hizi inawaita waTanzania wote wenye hoja au mtazamo tofauti kuwa ni 'wapuuzi'!? And to top it off, hata kuwasikiliza tu (na si kukubali maoni yao) ni upuuzi! Kama hivyo basi wapuuzi tupo wengi kweli kwa kuwa na mtazamo tofdauti na serikali yetu hii fisadi, kiziwi, kipofu, na ya kibeberu!

Muhongo amelwa madaraka. Huyu mtu ni hatari kwa taifa hili. Kauli zake zitaleta umwagikaji wa damu. Ajifunze kutoka kwa wakina Kagasheki. Wataalam na wana diplomasia. Juzi tumesikia anataka kugomea urais,
 
Madhara ya msimamo wake ni kuchochea hujuma za chini kwa chini dhidi ya miundombino ya gesi. Haitashangaza kuona miundombinu hiyo ikilipuliwa na baruti za wavuvi!.. Ni vizuri saana kuwasikiliza wanamtwara kuliko kutumia ubabe kwa namna yoyote ile.
 
Madhara ya msimamo wake ni kuchochea hujuma za chini kwa chini dhidi ya miundombino ya gesi. Haitashangaza kuona miundombinu hiyo ikilipuliwa na baruti za wavuvi!.. Ni vizuri saana kuwasikiliza wanamtwara kuliko kutumia ubabe kwa namna yoyote ile.

Sasa hivi tukiwaambia haya hawawezi kutuelewa kwani wanaamini wana jeshi litakalotumika kulinda miradi pamoja na kuulinda mfumo wao wa kinyonyaji.
 
Huyu waziri ana ubabe wa kijinga sana.....yeye anaona kuwasikiliza watu wa mtwara ni upuuzi? yeye mbona anataka kusikilizwa,kila mtu ana haki ya kusikilizwa na sio kubaguana kwa staili hii,binafsi ningependa kuona mikoa ya kusini inanufaika na hiyo gesi,ningependa kuona Nchi inapanuka katika maendeleo na sio dar peke yake.
Kumbuka huyu bwana aliteuliwa na rais. Hajawahi kugombea ubunge akauza maneno kwa wananchi ndiyo maana ana lugha za kibabe. Kweli gesi ni ya wote lakini siyo upuuzi kuwasikiliza wananchi. Sasa dempkrasia iko wapi kama hakuna kusikilizana. Ni jeshini tu ndiko kwenye amri.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom