Wananchi wajitokeza na mabango ziara ya Rais

Moshi. Baadhi ya wananchi wamejitokeza kwenye ziara ya Rais Samia Hassani Suluhu, wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali, ikiwamo migogoro ya ardhi na kuomba msitu wa nusu maili urejeshwe kwa wananchi.

Wananchi hao wamejitokeza katika Daraja la Rau wakati Rais Samia alipokuwa akiweka jiwe la msingi la katika daraja hilo lililosombwa na mafuriko mwaka jana.

Baadhi ya mabango hao yalikuwa na jumbe mbalimbali, za kuomba msitu wa nusu maili urejeshwe kwa wananchi kama ilivyo Serengeti na Ngorongoro.

Ujumbe mwingine, ni “kuchukuliwa kwa msitu wa nusu maili ni umaskini kwa vijijini 62 vinavyozunguka Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro."

Akiweka jiwe la msingi katika katika barabara ya Sanya Juu -Elerai wilayani Siha, Rais amesema changamoto zote ambazo ameziona kwenye mabango yenye jumbe mbalimbali atazichukua na kwenda kuzifanyia kazi.

Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.
Huyu ndio raisi wetu watanzania.. wanaojaribu kutuchonganisha sisi wana kilimanjaro na raisi Samia kwa sababu za kisiasa, mwenyezi Mungu awalani wao na vizazi vyao.
 
Moshi. Baadhi ya wananchi wamejitokeza kwenye ziara ya Rais Samia Hassani Suluhu, wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali, ikiwamo migogoro ya ardhi na kuomba msitu wa nusu maili urejeshwe kwa wananchi.

Wananchi hao wamejitokeza katika Daraja la Rau wakati Rais Samia alipokuwa akiweka jiwe la msingi la katika daraja hilo lililosombwa na mafuriko mwaka jana.

Baadhi ya mabango hao yalikuwa na jumbe mbalimbali, za kuomba msitu wa nusu maili urejeshwe kwa wananchi kama ilivyo Serengeti na Ngorongoro.

Ujumbe mwingine, ni “kuchukuliwa kwa msitu wa nusu maili ni umaskini kwa vijijini 62 vinavyozunguka Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro."

Akiweka jiwe la msingi katika katika barabara ya Sanya Juu -Elerai wilayani Siha, Rais amesema changamoto zote ambazo ameziona kwenye mabango yenye jumbe mbalimbali atazichukua na kwenda kuzifanyia kazi.

Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.
Migogoro ya ardhi na matumizi ya maji Msohi vijijini, stendi kuu ya mabasi yenye uwezo na hadhi ya kuhudumia abiria kwa wingi zaidi bila kutegemea mabasi yanayoanzia safari zake Arusha, ujenzi wa Soko kuu, kuchakaa kwa miundo mbinu ya barabara, umeme na maji wilaya ya Mwanga nk ni changamoto kwa wakazi wa Kilimanjaro,
 
..Chalamila alisema ktk ziara ya Rais SSH wananchi waende na mabango hata yenye MATUSI.

..Tuna Raisi mwanamama, tena mtu mzima, kwa hiyo tunahitaji kuwa na nidhamu zaidi kuliko wakati ule tulipokuwa na Maraisi wanaume.
Ndio anapokosea hapa tu
 
Back
Top Bottom