mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,050
- 4,904
Moshi. Baadhi ya wananchi wamejitokeza kwenye ziara ya Rais Samia Hassani Suluhu, wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali, ikiwamo migogoro ya ardhi na kuomba msitu wa nusu maili urejeshwe kwa wananchi.
Wananchi hao wamejitokeza katika Daraja la Rau wakati Rais Samia alipokuwa akiweka jiwe la msingi la katika daraja hilo lililosombwa na mafuriko mwaka jana.
Baadhi ya mabango hao yalikuwa na jumbe mbalimbali, za kuomba msitu wa nusu maili urejeshwe kwa wananchi kama ilivyo Serengeti na Ngorongoro.
Ujumbe mwingine, ni “kuchukuliwa kwa msitu wa nusu maili ni umaskini kwa vijijini 62 vinavyozunguka Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro."
Akiweka jiwe la msingi katika katika barabara ya Sanya Juu -Elerai wilayani Siha, Rais amesema changamoto zote ambazo ameziona kwenye mabango yenye jumbe mbalimbali atazichukua na kwenda kuzifanyia kazi.
Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.