Shughuli ya upigaji kura inaendelea katika Kata ya Malangali Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo wananchi wameendelea kujitokeza kupiga kura ya udiwani katika uchaguzi wa marudio unaoendelea leo Januari 22, 2026.
Wananchi wameendelea kujitokeza katika vituo mbalimbali vya kupigia kura.
Ushiriki wa wananchi umeonekana kuwa na mwamko, huku wakiendelea kujitokeza kupiga kura katika vituo vya kupigia kura wakitumia haki yao ya msingi ya kidemokrasia.
Pius Moses ambaye ni mkazi wa kata hiyo, amesema amepiga kura katika hali ya utulivu.
Shughuli hiyo ya upigaji kura ya marudio inafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa udiwani wa kata hiyo marehemu Peter Choma kilichotokea Oktoba 29 mwaka 2025.
Mgombea wa sasa wa nafasi hiyo ya udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Andrea Matanila amesema ameridhishwa na mwenendo wa upigaji kura.