Wananchi tujipange kulazimisha utekelezaji wa Hukumu ya Mahakama Kuu Kuhusu Wabunge batili

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Nchi hii kwanini tumekuwa mazuzu kiasi hiki?

Katiba yetu inatamka wazi kuwa ni jukumu la msingi kuhakikisha katiba na sheria zinalindwa.

Mahakama ilitoa hukumu kuwa wabunge wote waliotangazwa kuwa walikuwa wamepita bila kupingwa, siyo wabunge.

Na chochote walichofanya ikiwa ni pamoja na mishahara na posho walizopokea kutokana na nafasi ya ubunge, ni batili, wanatakiwa kuzirejesha.

Wabunge hawa wanatakiwa kurudisha pesa zote walizozipata kama mshahara na posho ambazo ni stahili ya wabunge.

Mmoja wa hao ambao ni wabunge batili na wanaotakiwa kurudisha pesa waliyouibia umma, ni pamoja na Majaliwa Majaliwa na Nape. Idadi yao ni 28.

Tangu hukumu ya Mahakama itolewe, Bunge halijafanya chochote.

Ushauri kwa viongozi wa CHADEMA, tunaomba andaeni maandamano ya amani kuelekea Bungeni na mahakama kuu. Maandamano yaelekee Bungeni kumlazimisha Tulia kuwafukuza hao wabunge batili bungeni.

Maandamano mengine yaelekee mahakama kuu, kuitaka mahakama itoa arrest warrant, ya kumkamata Spika na uongozi mzima wa Bunge kwa kudharau hukumu ya mahakama.

Maandamano mengine yaelekee ofisi ya Rais Mwungano kuoinga Zanzibar kuvunja katiba ya Mwungano kwa kyziondoa bandari za Zanzivar kwenye muungano.
 
Back
Top Bottom