Wananchi tufanye nini kama hatuna imani na Spika wa Bunge?

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,126
725
Jamani wanajf ninaomba niileta hii theory hapa tujadiliane kama linawezekana. Bunge lililopita halikuwa nzuri sana kwa sababu kulikuwa na udikter ndani yake. Je kama bunge la mwezi wa nne litakuwa kama hili la juzi tufanye nini kwa sababu spika anatupotezea muda kwa maslahi anayoyajua mwenyewe wakati sisi tunaumia. Tunajua kuna wabunge walikuwa na uchungu sana na hasa masuala yanayogusa jamii lakini walinyimwa fursa hiyo. Tunaomba kama kanuni na sheria za bunge zinaruhusu wananchi kushinikiza kuondolewa kwa spika japo kuwa ni chaguo la wabunge.
 
Kazi ya spika ni kuweka masingira muafaka kuwezesha bunge kutekeleza jukumu lake ambalo pamoja na mambo mengine, ni kusimamia utendaji wa serikali kwa niaba ya wananchi. kilichojitokeza katika kikao cha bunge lililopita, spika alitenda kinyume na wajibu wake huo, na hivyo badala ya kulisaidia bunge kutimiza wajibu wake, yeye ndiye akawa kikwazo kikubwa. Katika hali hiyo wananchi tunayo kila sababu kuandamana nchi nzima kumtaka ajihengue kwenye nafasi hiyo; kwani katiba yetu ya sasa inatamka wazi kuwa madaraka yote yanatoka kwa wananchi.
 
Wenye akili walisha jua bunge la chama kimoja lime rudi baada ya makinda kuwa spika...........
 
Ni afadhali tuwavamie huko mjengoni kabisa kama, ataendelea kuchemsha kama juzi. Yaani ni afadhali angetafuta muafaka wa kitu kimoja kitakacho msaidia huyu mtanzania kutokana na mazingira aliyonayo sasa hivi. Tunaendelea kulundika tu haya matatizo yakisha jaa yatapanguliwa vipi, sasa hivi yameshaanza kuwashinda.
 
Hivi yule ndo speaker wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania? I can imagine why we are still poor!
 
Back
Top Bottom