Wananchi na zigo la matatizo viongozi na posho lukuki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi na zigo la matatizo viongozi na posho lukuki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Jan 21, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tanzania ni nchi ya Watanzania wote,hata kama kasungura ni kadogo basi tugawane wote sawa,hayo ndo makuzi na malezi tuliyolelewa.Viongozi walikuwa na dhamira ya kweli katika kuwatumikia wananchi walio waweke madarakani.Mtu alichaguliwa kwa uwezo wake kiuongozi.Siasa haikuwa kimbilio la kila wafanyabiashara,wahalifu na wachumia tumbo.ALiyekuwa nacho na asiyekuwa nacho wote walikuwa sawa mbele ya sheria.Waasisi wa taifa walipinga udini,ukabila na ubaguzi wa kila aina.Tanzania tuliyokuwa nayo miaka hamsini iliyopita si ya sasa.Tanzania ya sasa imepoteza uhalisia na heshima iliyojijengea miaka dahari iliyopita.Taifa limegeuka omba omba kama vile tumetoka vitani,maisha duni kwa kila Mtanzania yanawezekana na wateule wachache waliopewa dhamana ya uongozi wanazidi kuneemeka siku hadi siku.

  Wananchi wamekumbwa na woga juu ya maisha yao,wamepoteza mwelekeo hawajui leo yao itakuwa vipi.Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ili tuendelee tunahitaji watu,ardhi,siasa safi na uongozi bora.Watu wameongezeka tofauti na wakati tunadai uhuru,ardhi ni kubwa kiasi tumeshindwa kuitumia na kuwapa wakoloni wawekezaji,uongozi bora huo ni msamiati,kwani ndo imekuwa njia pekee ya kujinufaisha na kupata utajiri mkubwa kupindukia.Japokuwa ninaamini hakuna marefu yasiyo na mwisho lakini mwisho wa yote haya ni balaa ndani ya nchi yetu tukufu tuliyopewa na mwenyezi Mungu.Wananchi wamekumbwa na hofu kubwa kila mmoja yuko radhi kufanya lolote ili mradi mkono uende kinywani.Maadili ya kazi na uongozi yamepotea,kila anayepewa nafasi amekuwa chinja chinja wa mali ya umma.

  Mfumuko wa bei unazidi kuongezeka bila kupata suluhisho hilo,waatalamu wa uchumi wameishiwa uwezo na hata wenye kuonyesha uhai , hoja zao kiushauri wamebezwa na kupuuzwa.Pengo la umasikini na utajiri linaongezeka siku hadi huku serikali ikiridhia mwananchi kuongezewa zigo zito la kupanda kwa gharama za umeme kwa asilimia 40%.Watawala wanazidi kudhihirisha ombwe la uongozi ndani ya nchi hii na chama tawala.Ile kejeli liyokuwa ikisemwa zamani Chukua Chako Mapema nayo imeshika kasi.Chama chenye serikali iliyoko madarakani kimekuwa bubu na serikali yake imekuwa kiziwi.
  Ajabu na kweli hata rais hajui ni kwanini wananchi wake ni masikini wa kutupwa wakati nchi imezungukwa na rasilimali za
  kutosha.Uholanzi ni nchi inayopata pato lake la taifa kwa kutegemea bandari,lakini nchi iko mbali sana kimaendeleo.Gabon ni moja ya nchi tulizokuwa nazo sawa kiuchumi, lakini leo imekuwa ni mfano mzuri katika kukuza uchumi wa nchi yao, sisi tunashindwa nini?Kwanini tunashindwa kutumia wataalamu tuliwasomesha kwa gharama kubwa.Kile kiapo cha nitatumia elimu yangu kwa faida yangu na wote kwa manufaa ya umma kimefutwa katika katiba ya CCM.Kwanini chama kinashindwa kuisimamia serikali yake!

  EWURA kazi yake ni nini,kama imeshindwa kuwatetea wadau wake.Mbaya sana tunawalipa asilimia moja 1% katika ankara tunazolipa kwenye maji na umeme wakati wameonyesha ni moja ya chombo kilichoshindwa kumtetea mwananchi.Mashirika ya huduma za kijamii kama TANESCO na mashirika ya maji yamegeuka kuwa taasisi za kibiashara,kweli tutabaki salama?Kodi kila kukicha ,mpaka service charge kwa upande wa TANESCO na mashirika ya maji nazo tunalipia kodi ya ongezeko la thamani(VAT).Huu ni uwizi mkubwa!Mbona posho wanazo lipana kila kukicha hazina kodi au dhamana tuliyowapa ni kutunyonya na kutuangamiza kabisa!Hatujui hata hizo service charge tunazo lipia zinafanya kazi gani kama serikali inawalipa mishara na posho.Ikiwa ni hivyo basi tusistaajabu ipo siku hata hospitalini,mahakamani na taasisi zote za kijamii tutalipia service charge.

  Serikali haina pesa,inajaribu kudhibiti vyanzo vyake vya mapato.Hilo hatukatai mbona kodi hizo hazina tija kwa wananchi ikiwa hata soko la ajira nchini hakuna.Madawa hospitalini hakuna,shule zenye kutoa elimu bora hakuna,nchi hii inakwenda wapi.Kila mtu yupo busy kusaka nafasi ya ulaji mwaka 2015.Wazee wetu waliotutumikia na kumpuzika wamekaa kimya kisa nao wanaogopa kusema wakisema wataguswa madhambi yao walipokuwa madarakani.Mwalimu alithubutu tena kwa ukali bila kung'ata maneno mbona yeye hakuogopa mabaya yake kuguswa?Wazee wetu hawa wamekuwa wanalalamika badala ya kukemea.Mh Mkapa kama wewe uliweza ndani aserikali hiyo mwenzio ulimpasia kijiti ana shindwa nini wakati chama na serikali ni ile ile!

  Hali halisi kwa sasa ni viongozi kuhangaikia posho na marupurupu na wananchi wanahangaikia mlo angalau wa siku moja.Hivi sereikali hii haioni bomu inalolifuga mlipuko wake utasababisha amani bandia tuliyonayo kupotea kabisa.Tunisia nao walipuuzwa kama tunavyopuzwa leo hii,Misri halikadhalika.Ni watanzania wangapi leo hii wameamua kujiajiri kwa kuendesha boda boda.Biashara hii imekuwa kama vile biashara ya kuuza bangi,hawana amani katika biashara yao,usumbufu wa kila aina mara wakamatwe na polisi mara wapigwe marufuku,hivi jeshi hili siku likiingia barabarani kuna atayesalimika.Wananchi wapo katika ukombozi wa kujikomboa na hali ngumu ya maisha, lakini vikwazo vinavyowekwa na watawala ni kichocheo cha uvunjifu wa amani hii japokuwa ni amani bandia.

  Mwisho wa uzalendo na uvumilivu ndani ya taifa hili umefika kikomo,mwenye macho na atazame saa ya walalahoi kujikomboa toka ndani ya tabaka la unyonywaji umefika mwisho.Leo hii kila kijana utakayeongea naye anaombea nchi ingie machafukoni angalau heshima tuliyoipoteza ilirudi.Hatuombei hali hiyo itokee na Mungu hainusuru isijitokeze lakini ukweli utabaki palepale wananchi wamekata tamaa kwa serikali yao na watawala wake.Serikali itafute njia mbadala kuhakikisha uchumi huu unakuwa si kwa watu wachache waliopewa dhamana pekee yao.Kila mtu anataka kuona uchumi unakuwa kwa pamoja na umma wote kufaidi keki ya taifa pamoja.Naomba kuwakilisha
   
Loading...