Wananchi Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!

Nimelipenda sana hilo bango lililoandikwa 'UKITUUA TUNAKUPELEKA THE HAGUE' safi sana hiyo ni salaam kwa JK na shemeji yake Said Mwema!
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

Umeambiwa wapo wabunge kama Hawa Ghasia, George Mkuchika sasa wewe unataka wawakilishi wapi tena???
 
Mtwara KOMAENI tu. Hiki kiwanda cha kusafisha GAS na kufua umeme kikijengwa Mtwara, mtapata wafanyakazi wengi sana watakaokuja kuishi huko. Kwa kuwa wengine kipato chao kitakuwa kikubwa, basi wataanza kupeleka watoto wao shule, kufanya shopping, kujenga nk.

Na nyie hata kama hamna shule, basi mtapata kazi za ulinzi, kupanda mauwa kiwandani na kwenye majumba yao, kufagia na kila aina ya usafi. Watataka huduma bora za afya, elimu, usafiri nk.

Kwa ufupi ni kuwa mzunguko wa hela utakuwa mkubwa sana kwenye kiwanda cha Gas na ikiwezekana mitambo ya kuzalisha umeme viwepo pia hapohapo Mtwara. Dar ije Gas iliyo tayari kutumika moja kwa moja.

KOMAENI WATANI ZANGU HADI KIELEWEKE. Nyie ndiyo mmeweka msingi mpya wa kulinda rasilimali zetu.


Mkuu Sikonge.
Asante kwa Ujumbe huu murua.Hawa waandamanaji baadhi ya mabango yao yalifaa yawe na haya maneno ya busara na ya kweli tu
.
Dar ije Gas iliyo tayari kutumika moja kwa moja.

Wana Mtwara katika kipindi hiki au jambo hili wanatakiwa kusahau uvyama/Siasa na kuwa wamoja kudai haki.
 
Mpaka wameandamana ujue hao wawakilishi wameshindwa kazi yao ya kuwatetea wananchi.
ndugu zangu wa mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na chadema, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu
 
Mie mkuu naona watu wamekata tamaa.

Wameona wanapuuzwa na watawala, hayo mengine yanakuja baada ya hilo. Watu wa Mtwara huko nyuma walikuwa na msimamo imara kisiasa wakiunga mkono serikali kwa kila kitu. Umaskini ndio umewafanya wakate tamaa.

Ni point ya kufanyia kazi bila hata kujali nani yuko behind.

Mchami haya ni ya ukweli. Tanzania haitakuwa ya kwanza kuingia katika matatizo ya uvunjifu wa amani kutokana na matatizo yasiyolinganifu ya maliasili/ raslimali hasa kwa sehemu zinapopatikana maliasili/raslimali hizo. Ndiyo maana tunapaswa kubadilisha muundo na mfumo wetu wa utawala na uchumi ili wananchi wawe na maamuzi.
 
Gesi iliyopo Mtwara ni nyingi sana na haiwezi kwisha hata ikipelekwa Dar es Salaam kwa faida ya Tanzania nzima kwa miaka 50 ijayo. Kitu cha msingi siyo kuzuia gesi isiondoke Mtwara bali fursa zipelekwe kule kama vile hivi sasa kuna ujenzi wa kiwanda cha saruji unataka kuanza pale Mikindani. Wananchi wawezeshwe katika kujiajiri kwa viwanda vidogo kwa kutumia umeme utakaozalishwa na gesi. Kushabikia suala hili (la kukataa gesi isiondoke Mtwara) ni ujinga kwa sababu ikifika Dar es Salaam itaisaidia Tanzania nzima ikiwemo kuongeza mapato ya wafanyabiashara wakubwa ambao watafikiria kwenda kuwekeza pia Mtwara na Lindi
 
Nasubiri mchango wako wa pili ....................... kama utarudia maneno yanayofanana na haya!!

Nadhani leo ameokoka kifikra. Nasikitika kazi imeninyima nafasi ya kushiriki maandamano hayo. Bt tupo pamoja na wanamtwara wote na wadai haki za msingi za maendeleo ya kila mahala.
Miaka 51 imepita barabara haijakamilika kutuonyesha sisi ni mazuzu bomba halimalizi mika miwili limekamilika.
Tumechoka.

Rise up Mtwara and all southern zone rise voices hadi wasikie.
God help us from this evil acts frm MAGAMBATUNATAKA GAS IWANUFAISHE WA MTWARA NA SIO BAGAMOYO.
 
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu

Acha unafiki wewe. Ukiangalia hapo kwenye maandamano, unaona bendera ya ADC nadhani na NCCR/CUF. Uliona kukaa kimya kuitaja CHADEMA ungepungukiwa na kitu?
 
ccm ni wakoloni weusi,sisi mtwara kuhusu ishu ya bara bara tumehangaika miaka nenda rudi,wao wametufanya sisi kuwa ni mtaji wao na kufanya kila wanaloamua wao kufanya,,sasa waamue tuone

jiulize kwa nini bomba la mafuta lijengwe kwa miezi 18 tuh wakati bara bara ile imesota ndani ya miaka 51 hadi leo hii wanasua sua kuimaliza,do they think that we are such dumb enough and dull to recognise our rights and fight for our development??
Waache waendelee kufikiria namna hiyo,picha linaendelea na huo ni mwanzao tuh
 
Whether they are right or wrong, it is a message and a sign. The so called "Wananchi" at the Ultimacy of its meaning! think, think, think....!
 
Nnauye Jr, na wana CCM wenzako.

Hapa hatuoni mnachangia ila kwenye issues za mipasho kama Slaa kumiliki kadi.

Hapa ndipo kwenye siasa zenye maslahi kweli. Hapa tunazungumzia maisha ya mtanzania na maslahi yake.

Karibu Nnauye Jr.

cc. masopakyindi
 
Last edited by a moderator:
Pasco upo hapo? nilikuwa naitafuta ile thread yako, sasa na hawa sijui ni Wachaga au ni watu wa Kaskazini? Muoneshe hii thread Boss wako Lowasa kwamba nchi anayotaka kutawala mpaka mandondocha yaliokuwa ndio strong hold ya CCM yameshtuka.

Sasa hii treni ni mbele kwa mbele na hizi ni salamu za uchaguzi wa 2015 utakavyokuwa utawaduwaza wengi na uchambuzi wenu feki. Kimya sasa kinaongea, hawa ndio wabaya kuliko wale ambao walishaamka siku nyingi. Wait n see.
 
Last edited by a moderator:
Washavaa sana khanga t shirt na kofia za maisha bora leo ndio wanashituka sio?wacheni sisiem ipumuwe
 
Ilikwisha kuandikwa kuwa vipofu watapata kuona,viziwi watapata kusikia na viwete watatembea.Ni faraja kubwa kuona waliokuwa wamelala kwa mda mrefu hapa nchini(kwa mujibu wa historia) sasa wanaamka tena kwa kasi.Ntwara juuu,juuu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom