"Alijuwaye joto la jiwe ni Mjusi".Nabwada uwe mkweli; hivi gesi ikisafirishwa hadi DSM, nyie watu wa Mtwara mtashindwa kuendelea na shughuli zenu za uzalishaji mali. Mie nafikiri mnatumia pasipo wenyewe kujitambua.
Manufaa ya kuwepo kwa gesi yameshafika Mtwara kama vile kuwepo kwa shughuli nyingi za kuingiza kipato tofauti na kabla ya gesi kama vile radio fm ziko nyingi, nyumba za kulala wageni zina soko, biashara kwa ujumla zinalipa siku hizi.
Muelewe gesi inayopangwa kupelekwa DSM ni ziada.
Kiwanda cha cementi kinachojengwa Mtwara hakitaweza kumaliza matumizi ya gesi iliyoko Mtwara hivyo haitakuwa rahisi kurudisha gharama za uzalishaji
Shida imeanzia kwenye kuelimisha wananchi nini kinafanyika na wao wanafaidikaje.
Kwa mfano mitambo ya kufua umeme wa gesi imejengwa Dar, kwa nini isingejengwa Mtwara?
Hii inakuwa political issue mkuu. Kama watu hawaelewi waelimishwe na si kulaumiwa. Watu wa Mtwara wanaona wamebaguliwa katika maendeleo ya nchi. Wanataka waone hatua za wao kushiriki maendeleo hayo.
Ndugu zangu wa Mtwara nyie ni watu makini, msiponzwe na CHADEMA, maandamano si njia bora ya kudai haki zenu, tumieni wawakilishi wenu kuanzia madiwani hadi wabunge watafanyia kazi kupitia serikali yetu sikivu
Urusi ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa gesi duniani na wamejenga bomba la kusafirishia gesi hiyo hadi Bahari Nyeusi (Black Sea) ili waweze kuisafirisha kwenda Ulaya ambako ndiko kuliko na soko!
Itakuwa ajabu kwa gesi ya Mtwara kubaki huko ambako hakuna watumiaji wala soko!
Nadhani kuna upotoshaji mkubwa umefanywa, jitihada zifanyike kutoa elimu sahihi kuhusu gesi na hasa matumizi yake!
Ni kweli kuwa mitambo ya kuzalisha umeme na viwanda vya mbolea vitakavyotumia mali ghafi ya gesi vijengwe Mtwara na Lindi lakini pia bomba la kusafirisha gesi hadi Dar es Salaam, Tanga, Morogoro nk kwa matumizi ya nyumbani na kuendesha magari nk linapaswa kujengwa!
Naomba na ajitokeze mtu na
aeleze faida ya Gesi ya Mtwara kubaki Mtwara...
Pia aeleze hasara za gesi ile kupelekwa katika miji mingine kama
Darisalama....Kwa watu wa Darisalama, kwa watu wa Mtwara na Kwa
Watanzania wote....
nipo hapa pande za bima watu ni wengi mno, foleni ni kubwa sijawahi ona, waandamanaji/wapigananji..wanazunguka barabara kuu huku jeshi la posilisi likiwa nyuma yao lengo kubwa ni kupinga utoaji wa gas ielekee daslam...nyimbo nyiingi wanazoimba ni kwamba hawamtaki hasa ghasia wala mkuchika na gas isiwafate bali wao waifate ilipo....
nb: Kwa hali hii naona watu wa mtwara tumeanza/wameanza kujitambua!! Impact yake gas ikihamishwa itakuwa kubwa kuliko maelezo...we still keep in watching...gas kwanza, vyama baadae!!
More photos to come soon!!stay tuned!!
photoz: Update
Hizi NGOs na vyama vinavyoshabikia maandamano ya watu wachache wa Mtwara watueleze yafuatayo:-
1. Uzalishaji wa gesi unaofanyika Mtwara
2. Watumiaji wa gesi mkoani Mtwara
Wananchi wasikubali kutumiwa na watu wanaotaka kupata maslahi yao kupitia maandamano