Wananchi Mbeya Wamukata DC Balama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Mbeya Wamukata DC Balama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Nov 22, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Tuesday, November 22, 2011[/h] [h=3] WANANCHI WAMKATAA DC WA JK, NI KUHUSU UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA NA NHC MBEYA
  [/h]
  [​IMG]
  KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA MBEYA EVANCE BALAMA AKIWA NA MKURUGENZI WA WILAYA HIYO JULIANA MALANGE.

  WANANCHI wa kijiji cha Ikumbi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya leo walimweleza Mkuu wa wilaya hiyo Evance Balama na ujumbe wake uliokuwa umefika Kijijini hapo kuwa wanamtaka Rais Jakaya Kikwete kuzungumza nae na wala si yeye.


  Hali hiyo ambayo ilishangaza vigogo wa Serikali waliokuwa wamefika katika eneo hilo ilianza na wananchi kukataa salamu za viongozi hao akiwemo mwakilishi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Juliana Malange.

  Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ackson Mwanjoka ambaye alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na agenda moja ya kujengwa kwa mji wa kisasa katika Kijiji hicho kilichopo karibu na kiwanja kipya cha ndege cha Songwe mahala ambapo walihamishwa awali bila kulipwa vema stahiki zao.

  Mwenyekiti huyo alipojaribu kumkaribisha Mkuu wa wilaya, wananchi walikataa kwa kunyosha vidole wakiashiria kuwa hawakuwa tayari kusikiliza agenda hiyo ambapo Mkuu wa wilaya aliinuka na kuwaambia kuwa waanze wao kusema.

  Baada ya Mkuu wa wilaya kuwataka waseme hoja zao ndipo wananchi wakanyosha kidole na Mwenyekiti wa Kijiji hicho akampa nafasi mwananchi Meshack Job.

  Mwananchi huyo alisema kuwa wananchi walikuwa wamebaini mbinu ya Serikali ya kuwahamisha hivyo kutokana na hali iyo na kwasababu awali hawakupewa fidia stahiki katika eneo ulipojengwa uwanja wa ndege hawakuwa tayari kuusikiliza ujumbe huo bali wanameitaji Rais Kikwete ili wazungumze nae.

  ‘’Niweke wazi kuwa agenda iliyopo mezani ni kama zilizowahi kujitokeza hapo nyuma mwanzoni mwa mwaka huu na wananchi hatuhitaji kuwasikiliza na kuzungumza chochote na nyinyi ambaye tunamwitaji ni Rais Jakaya Kikwete na si mtu mwingine yeyote’’ alisema Job huku akiondoka na wananchi wenzake wakishangilia kwa kusambaratika.

  Kitendo hicho kiliwaacha midomo wazi huku wakitazamana kwa zaidi ya dakika tatu viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu huyo wa wilaya huku wakianza kumtupia lawama Mwenyekiti wa Kijiji hicho kuwa alikuwa anaufahamu mpango huo wa kuwadhalilisha viongozi wa Serikali.

  Mkuu wa wilaya alipoulizwa mtazamo wake juu ya hali hiyo iliyokuwa imejitokeza alisema kuwa wananchi walipaswa kusikiliza kwasababu Serikali ina mpango mzuri wa kuwajengea makazi ya kisasa katika maeneo yao kupitia Shirika la Nyumba la Taifa NHC.

  Mwenyekiti Wa Kijiji hicho Ackson Mwanjoka alisema kuwa shutuma zilizotolewa dhidi yake ya kuwadhalilisha vigogo hao kupitia wananchi alisema kuwa hakutendewa haki kwasababu hata taarifa za mkutano huo alipewa Novemba 18, mwaka huu hivyo hasingeweza kujua lolote ingawa alikiri kuwa wananchi wana hasira na Serikali katika masuala ya Ardhi katika eneo hilo.

  Hali hiyo imejitokeza ikiwa ni siku chache wananchi wa Kijiji cha Mbalizi wilayani humo kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumwondoa wilayani humo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Juliana Malange kwa madai kuwa analinda genge la waporaji wa miradi ya wananchi ukiwemo mradi wa maji wa Kijiji hicho.

  Viongozi wa Shirika la nyumba la Taifa waliokuwa wameongozana na Mkuu huyo wa wilaya ili kutoa elimu juu ya uwekezaji huo wa nyumba za kisasa ni pamoja na Meneja wa Shirika hilo mkoa wa Mbeya Charles Kessy, Frola Luvanda, Gidion Mgaya na Raymond Mdolwa ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Shirika hilo.
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=3]NGUVU YAUMMA YA CCM YAWANG'OA MTENDAJI NA MWENYEKITI WA KIJIJI MBARALI [/h]
  [​IMG]

  BAADHI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA ISUNURA WAKIPA KATIKA PICHA YA PAMOJA HIVI KARIBUNI. (Picha na Maktaba ya mtandao huu)

  [​IMG]
  KATIKATYI NI KAIMU AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA ISUNURA BRUNO MPALILE AKIWA AMEZINGIRWA NA WANANCHI WAKIMSHINIKIZA KWENDA NYUMBANI KWAKE HAPO YUPO KILABUNI.


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Isunura wilayani Mbarali mkoani Mbeya, kimetumia nguvu ya Umma kumnyanganya mihuri Kaimu Ofisa Mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji hicho kutokana na viongozi hao kutowatendea haki wananchi.

  Tukio hilo ambalo lililazimu Kikosi cha jeshi la Polisi kufika kijijini hapo lilitokea mwishoni mwa wiki ambapo wananchi hao wanamtuhumu Mwenyekiti wa Kijiji hicho Silvio Mbishila(CCM) kuwa ni moja ya vikwazo vya maendeleo ya Kijiji chao.


  Walisema kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa mstari wa mbele kula rushwa kutoka kwa wafugaji wa vijiji jirani na kupelekea wafugaji hao kuchungia mifugi yao katika maeneo ya kijiji hicho licha ya kuwepo sheria ndogondogo walizojiwekea huku baadhi ya vigogo wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali wakimkingia kifua.

  Akizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo, Mwenyekiti wa CCM tawi la Isunura Chesco Mduba alisema kuwa chama chake kimejitoa udhamini kwa Mwenyekiti huyo na kupeleka mihtasari ya maazimio hayo ngazi ya chama wilaya na Serikali tangu Februari mwaka huu lakini wanashangaa kuona anaendelea kulindwa.

  ''Huyu Mwenyekiti sisi wanachama ambao ni wadhamini wake, tulipokea malalamiko kutoka kwa wananchi na sisi wenyewe tunajionea kushindwa kazi kwa mtu huyu ndipo tukaandika mihtasari kwa viongozi wa juu na kutamka wazi kuwa tunajitoa udhamini lakini tunashangaa tunapuuzwa'' alisema Mduba.

  Alisema kuwa tangu barua na mihtasari hiyo iandikwa hakuna kiongozi yeyeote ambaye amefika katika kijiji hicho kuangalia hali halisi ya malalamiko ya wananchi ambapo kiongozi huyo kwa kushirikiana na Kaimu ofisa mtendaji wa Kijiji hicho Bruno Mpalile wakiendelea kufanya mambo watakavyo na taarifa zikipelekwa Halmashauri hazifanyiwi kazi.


  Mwenyekiti huyo wa Kijiji ambaye alipobaini kuwa wananchi wa Kijiji hicho walikuwa wamejikusanya kwa ajili ya kwenda nyumbani kwake kuchukua mihuri ya Kijiji chao alikimbilia katika kituo cha Polisi cha mjini Rujewa kwa ajili ya usalama wake ambapo vyombo mbalimbali vya usalama vilihusika katika kutaka suluhu ya suala hilo ambavyo viliamua Mwenyekiti huyo kurejeshwa kijijini hapo na kukabidhi mihuri kama walivyokuwa wakitaka wananchi hao.

  Alipofika Kijijini hapo akiwa ndani ya gari ya Polisi lenye namba za usajili PT 1960 wananchi wakaaza kushangilia na kudai mihuri yao ambapo Mwenyekiti huyo pamoja na askari polisi waliwaomba wananchi hao kuwa mihuri hiyo ikakabidhiwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo George Kagomba au kwa diwani wa kata ambayo hawakuitaja kwasababu mpaka sasa kijiji hicho hakijulikana kipo katika kata gani.

  Baada ya ombi hilo wananchi walikataa na kuwaeleza askari polisi hao kuwa kama walikuwa wamepanga hivyo ili kuendelea kuwanyanyasa wananchi basi hawakuwa tayari kuondoka katika eneo la makazi ya Mwenyekiti huyo hivyo walishauri kuwa endapo watakaidi kuwapatia mihuri yao wakamwite Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ili akatolee ufafanuzi juu ya kumlinda Mwenyekiti huyo na watendaji wengine katika Kijiji hicho.

  Mvutano huo ulizaa matunda kwa wananchi kukabidhiwa mihuri ya Kijiji chao ambapo mihuri hiyo ilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa CCM wa tawi hilo Chesco Mduba ndipo Polisi wakawaambia wananchi kuwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ungefika kijijini hapo kwa ajili ya ufafanuzi zaidi lakini mpaka kufikia jana hakuna kiongozi yeyote wa Serikali ya wilaya hiyo aliyefika kijijini hapo/

  Waandishi wa habari walipofika ofisini kwa Mkurugenzi wa wilaya hiyo ya Mbarali kwa ajili ya kuhoji juu ya suala hilo walizuiliwa na katibu muhtasi wa Mkurugeniz huyo kwa kile alichodai kuwa Mkurugenzi huyo hakuwepo ofisini kwake.
   
 3. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sijui watasema tena kuna mkono wa chadema au ni nani kasababisha kama sio magamba wenyewe na ahadi zao zisizo timizwa.Na hapo pia walitaka kutoa ahadi za owongo kama kawaida yao.
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hongera wananchi wa Mbeya na hii ndo dawa ya hawa viongozi wa magamba,ni kukataa kuongea nao wala kuwasikiliza hizo taarabu zao ambazo wamekuwa wakizitoa siku zote kwa muda miaka 50 ya uhuru.
   
Loading...