Wananchi Mbeya wachoma basi

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Wakazi 30 wa Kijiji cha Ihanda wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya juzi walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi kujibu shitaka la kuchoma moto basi la abiria aina ya Toyota Coaster lililokuwa likifanya safari zake kati ya Tunduma na Mbeya.

Ilidaiwa juzi na Mwendesha Mashitaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Charles Makunja kuwa, Januari 19 mwaka huu saa 12.50 jioni katika barabara ya Tunduma - Mbeya, watuhumiwa hao kwa pamoja bila uhalali wowote walichoma moto basi lenye namba za usajili T 196 ADC mali ya Tusubile Mwampamba mkazi wa Mbeya.

Aliwataja watu hao kuwa ni pamoja na Frank Mlungu (16), Emmanuel Mlungu (20), Jophrey Simyota(19), Masha Sichone(20), Joshua Kyando(20), Fadhiri Nzowa(15) na Peter Mwashiuya(16)

Wengine ni Hezron Mbalwa(32), Joseph Mwatusubila (26), Michael Mnkondya(19), Christina Mshani (18), Steven Simon (19), Jophrey Kibona (19), Erasto Mwamlima (28), Alex Mgalla(25), Franksoni Sichinga(30), Michael Mlungu(18) na Teteka Simfukwe(18)

Makunja aliendelea kuwataja wengine kuwa ni Jotson Mbwaga(23), Gabriel Mwailima(39), Madilu Haonga(17), Mateo Kitta(19), Msenga Sichone(38), Bahati Sichinga (32), Jemsi Simfukwe (26), Ally Wibson(20), Michael Sichinga (20), Isaya Kabuka (26), Jailosi Simkonda na Watson Kibona (16).

Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na hakimu wa mahakama hiyo, Nyasige Kajanja aliamuru washitakiwa hao wapelekwe rumande hadi Februari 3mwaka huu badaa ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa kila mmoja kuwa na mdhamini mwenye fungu la dhamana la Sh 12 milioni.

Basi hilo lilokuwa likiendeshwa na Dankeni Masika (33) lilimgonga mtembea kwa miguu Charles Sikanyika (25) aliyefariki dunia papo hapo.

Kufuatia hatua hiyo washtakiwa walidaiwa kulichoma moto wakiwa wamechukua sheria mikononi mwao ya kufanya uhalibifu huo.
 
Back
Top Bottom