Wananchi hawezi kuishitaki Serikali yao kwa kosa hili?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,317
12,617
Inafamika kuwa Serikali inakusanya Kodi kutoka kwa wananchi, na inakopa kwa niaba ya wananchi wake, inafahamika pia kuwa serikali inapanga na kutekeleza mipango kwa kutumia fedha za wananchi. Je, wananchi hawezi kuishitaki serikali Yao kwa kupangiwa mipango mibaya iliyowatia hasara wananchi mmojammoja, kundi au taifa?

Serikali yetu inawatia hasara wananchi mmojammoja, kama kundi au taifa kwa kupanga mipango isiyosomana hivyo kutia hasara kwa wananchi na taifa.

Mfano, wizara ya nishati, wizara ya maji, wizara ya ujenzi na wizara ya mawasiliano hazisomani kabisa. Watu wa umeme wanaweka na kupitisha umeme kwenye majengo yaliyoko kwenye hifadhi ya barabara, watu wa barabara wanahamisha nguzo za umeme na nyanya za mawasiliano ili kujenga barabara, watu wa barabara za mabasi yaendayo haraka wanabomoa barabara ambazo bado ni nzima za magari ya kawaida ili kujenga njia zao, watu wa maji wanavunja barabara kupitisha mabomba ya maji na watu wa mawaziliano wanapitisha nyaya zao kwenye eneo ambalo siku chache TU zijazo zinahamishwa au kukatwa na ujenzi wa barabara na sehemu inayofaa kwa kilimo inageuzwa kuwa makazi, kiwanda au mgodi.

Mipango na matumizi yote ya aina hii ama yanawatia hasara wananchi mmojammoja au wananchi kama taifa. Hii ni kuonyesha kuwa ama serikali inaajili watu wasiokuwa na uwezo au wananchi wanachangua viongozi wasiokuwa na uwezo na upeovkabisaa. Tunapoteza hela za Kodi na mikopo kugharamia kitu kilekile kwa muda mfupi. Hakuna wataalamu na viongozi wenye uwezo wa kuiona nchi miaka 100 ijayo, bali tuna wataalamu na viongozi wa leoleo na miaka 5 hadi 10 TU ya awamu Yao baasi, wajao watajijua.

Swali ni je, sisi wananchi hatuwezi kuishitaki serikali kwa mipango mibovu inayotuingiza hasara? Je, wananchi tunamjua kiongozi anaetufaa au ni oya oya TU za fulana na kofia wakati wa chaguzi?

Mara zote huwa ninawasifu kwa mipango kanisa katoliki. Hawa jamaa wanapotaka kujenga kanisa huwa wanaenda kutafuta eneo kuuubwa kabisa mbali kabisa na mji kiasi kwamba hakuna mtu anashituka Wala kuwaambia acha kwakuwa ni kama porini kabisa kwa fikira za watu wajinga. Tena wanaweza kwenda kuchukua eneo ambako Kuna fisi, mawe, mabonde na kusikofaa kuishi kwa akili za watu wajinga. Lakini wao wanawaza kuanzia miaka 20, 50, 100, na zaidi. Watu wetu sisi wanawaza matumbo Yao leoleo na uchaguzi ujao itakuwaje.

Mwl Nyerere alikuwa anaiona nchi miaka zaidi ya 100.
 
Back
Top Bottom