Wananchi hatuitaki CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi hatuitaki CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Mar 19, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kuna upotoshaji mkubwa sana unafanyika hivi sasa ambao unafanyika katika namna ya hatari sana, naiweza kuifafanisha namna hiyo sawa sawa na mtu anaesema moto ni joto au upofu ni usingizi. Wanasiasa waliomadarakani wanajaribu kuyawekea mahitaji ya wananchi dhana ya kisiasa.

  Wakati wananchi wanasema tunataka Mfumo bora wa elimu watawala wanasema CHADEMA haiwezi kuuleta, sababu DR SLAA Aliiba pesa kanisani.

  Wananchi wanasema tunataka mfumuko wa bei udhibitiwe, watawala wanasema CHADEMA haiwezi kudhiti mfumuko wa bei sababu MBOWE ni DJ

  Wananchi wanasema tunataka huduma bora za afya, watawala wanasema, DR Slaa anampenda sana Josephine.

  Wananchi walia wanakufa njaa, watawala wanasema, CHADEMA ni chama cha Kichaga.

  Wananchi wanapiga kelele wanalalamika mariasiri za Taifa letu zinanufaisha wachache na nyingi zinaibiwa na wageni, watawala wetu wanasema Ushindi ni Lazima.

  Naomba tukumbushane historia mbichi kabisa, waliomfurumusha Hussein Mubarak kutoka Madarakani sio wanasiasa, Kijana aliyejichoma moto tunisia na kuacha laana nyuma yake hakuwa analalamikia wizi wa kura, waliomkamata Gadafi kwenye mtaro wa daraja walikuwa hawajebaba bendera ya chama chochote kile cha siasa, Hata sasa huko Siria wananchi hawapiganii kuundwa katika mpya wala kuwa na tume huru ya Uchaguzi.

  Wito wangu kwa viongozi wa CCM ni huu ufuatao.
  Kwanza, kuna ushahidi wa kutosha kwamba hivi sasa duniani, mabadiriko yanatokea kwa kasi ambayo haijawahi kutokea huko nyuma katika kila nyanja ya maisha.

  Pili na mwisho, Muda si mrefu watanzania watagundua kwamba wanachokihitaji sio katiba mpya na wala sio tume huru ya uchaguzi wala sio maridhiano ya kitaifa ya namna yoyote ile wala sio ushindi wa wagombea wao.

  Narudia tena, Punde kidogo, upepo wa mabadiriko utabidiri mkondo wake, watu watakapoamua kuweka magwanda na kuachana na ustaarabu wa kuonyeshana alama ya V sijui mtawaambia nini.
   
 2. N

  NTABWENKE Senior Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kiukweli nami naungoja kwa hamu kubwa wakati huo kama mlinzi angojeavyo asubuhi, siku inakuja tena inafanya upesi sana machop hayataambiwa tazama wala masikio sikia. Tuombe uzima.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kiongozi hebu nifafanulie kidogo. Hivi mti ukikauka unaangalia majani peke yake bila kujua kama mti wote una athari?

  Mkuu wa mkoa akitumia vibaya mali ya umma (na wanafanya sana) wananchi watamfanya nini wakati ni mteule wa rais? Mkurugenzi wilaya akiboronga mambo watu watanyaje wakati ni mteule wa rais? Mbunge akiamua kuchapa usingizi bungeni kwa miaka yote mitano wapiga kura wake watamfanya nini wakati katiba inasema kilichoenda kwa mganga hakirudi? Jaji mkuu akinyamaza wakati haki za binadamu zinakiukwa mtanfanya nini wakati kapewa TOR na rais?

  Wananchi wafanye nini wakati nchi inayoendeshwa kama ofisi moja itakavyoona 'inafaa'?
   
 4. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu CCM wameishiwa hoja ndo maana wanaongea pumba, tena wanamuogopa Slaa kuliko hata wakwe zao waulize watakwambia. kimsing Dr Slaa ndiye Rais wa Tanzania kwa sasa nadhani umeona Arusha need more
   
 5. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  huitaki wewe na ndugu zako
   
 6. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno ya namna hii huwa yanapatikana kwa akina mama waimba taarabu! majungu, majungu! Huwezi kutetea CCM kama unajua hali ya nchi hii ilivyo mbaya!
   
 7. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kwenye Msafara wa Mamba na kenge wamo
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  KWI KWI KWI KWII, teh teh teh. Wishful thinking!
   
 9. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Soma kabla ya ku-comment wewe mtanzania usiyependa kusumbua akili yako.
   
 10. R

  Real Masai Senior Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza ningetaka kujua ww ni nani ila kwa ufupi ningesema ww ni Mipasho ya MAGAMBA.Nikuulize kuwa ww nani alikwambia kuwa Watz hawaitaki CDM.Na ni nani kasema CDM ni ya Wachaga.Acha kuwa na fikra potofu.Watz tushajanjaruka na hatutaki Propaganda.Kati ya CDM na CCM ni nani chama cha Familia.Obvious ni CCM.Kwa ufupi angalia Arumeru, Eti mpeni SIOI ubunge ana majukumu ya kifamilia.Kwa ni mtanzania yupi asiekuwa na majukumu ya kifamilia.Ningekushauri uwe na fikra endelevu, kwanza noi bora ukafanya Research. WITHOUT RESEARCH,NO RIGHT TO SPEAK. CCM ndio chama cha familia,na kurithishana au ww Huoni.ACHA KUWA NA MAWAZO MGANDO YA KCCM.
   
 11. v

  valid statement JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Sipati shida kujua umesoma kichwa cha habari pekee na kisha ukakimbilia kujibu.
   
 12. v

  valid statement JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  umetoa povu kabla hujelewa dhima ya mtoa mada mdau.
   
 13. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Title inapotofautiana na maudhui tarajia kuwa-mislead wasomaji!
   
 14. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mkuu! naapa kwa jina la mungu wangu. ilibaki kidogo tu niminye kitufe cha Log out halafu nijiregist kwa ID mpya .Halafu ningeporosha tusi kubwa la nguoni na tena...............! bahati nimekuelewa
   
 15. mchadema

  mchadema JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  mkuu u r among wise people, the only challenge is the title of ur thread which many wouldn't want to hear. Unajua katika kila jambo kuna kisababish whether obvious or hidden. Kwa watz CDM inaonekana kama a means to achive the change we want. Tukianza individual mvnt kushndwa ni tarajio, Ila Though CDM WE CAN! Together we CAN. MUNGU MBARIKI DR SLAA NA WANACDM WOTE, CCM ILAANIWE MILELE!
   
 16. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hiki Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kufanya mapinduzi yoyote ya kimaendeleo kwa miaka zaidi ya 50 kikiwa kimeshika nchi,kilichofanya na kinachoendelea kufanya ni kuendelea kuziba viraka vya kiuchumi,kijamii na kiutawala bila kuwa na njia zozote za kuleta mapinduzi ya kweli.
  Hayati Mwl. Nyerere na Karume na mashujaa wengine walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanzania ya sasa hawakuweka vyama mbele halafu wakakaa nyuma yake wakitegemea uhuru uletwe na kikundi kidogo cha watu wanaofanya vikao na mikutano ya mara kwa mara.
  Tukumbuke Nyerere hakupenda kubweteka kama wanasiasa wa leo bali aliendelea kupenda aitwe Mwalimu akifanya kazi kuleta uhuru na maendeleo kwa kadri ya hali za kipindi hiko na uwezo wake.Sio hawa maafande wanaopenda kuitwa Dr bila kuusomea wala kuwa na taaluma.
  Leo CCM inaendelea kuimba wimbo ule ule wa Uhuru kikijitahidi kutumia gharama nyingi kuwashawishi wananchi kwamba bado wanakihitaji na kuweka msisitizo kwamba kilimletea mtanzania uhuru huku ikionekana wazi kimeshindwa kuendeleza mafanikio yaliyopatikana miaka 50 iliyopita.Hata misingi aliyoweka Nyerere ya mapinduzi ya kweli ya kumkwamua mtanzania na wale maadui wa3 ujinga,umasikini na maradhi bado haijatekelezwa.
  Mapinduzi ya kweli hayataletwa na vyama vya siasa pekee bali mtanzania wa kawaida anapaswa kuchukua hatua na kubadilisha mfumo huu mzee mambo ili kuyaleta mapinduzi ya kweli.
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Heading yako haina correspondence na content. Iedit.
   
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nakomaza watu akili mkuu. watu wanatakuwa kuwa na uwezo wa kusimamia wanachokiamini kuanzia kichwani kwanza sio matumboni na mifukoni. Na ni lazima tuitahadhirishe CCM ili ijue ukubwa wa mashtaka yetu.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nakuhakikishia kwamba kabla ya 2015 utakuwa umeikana CHADEMA mara tatu.
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  King xvi, nashukuru mods wameipiga ID yako ya zamani LIFE BAN.
   
Loading...