Wananchi eneo la mkimbizi iringa waua kibaka........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi eneo la mkimbizi iringa waua kibaka........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 10, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  WANANCHI wakazi wa Mkimbizi katika Manispaa ya Iringa wanaodaiwa kuwa na hasira kali wamemuua kijana mmoja ambaye jila lake halijafahamika kwa tuhuma za wizi.

  Wakielezea undani wa tukio hilo katika mahojiano na mtandao huu mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kijana huyo akiwa na wenzake zaidi ya wanne walivamia nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo la Mkimbizi huku wakiwa na silaha mbali mbali kwa lengo la kupora mali .

  Alisema Salum Kalinga ambaye ni mmoja kati ya wananchi waliopata kushuhudia tukio hilo kuwa baada ya kuvamia mwenye nyumba alifanikiwa kutoa taarifa kwa majirani zake ambao waliweza kuamushana na kufanikiwa kuizingira nyumba hiyo huku vibaka hao wakiwa ndani ya nyumba.

  "Kama si ushirikiano wa wananchi wa eneo hili la Mkimbizi hawa majambazi walikuwa wamejiandaa vya kutosha wakiwa na silaha mbali mbali kama bunduki na mapanga na virungu ....ila huyo alikuwa na bunduki alishindwa kuitumia baada ya kubanwa na wananchi hao"

  Hivyo baada ya kuona wananchi wamefanikiwa kuwavamia huku baadhi ya wananchi wakiwa na silaha za jadi na baadhi yao wakiwa wametoka na bunduki zao ndipo majambazi hao walipoamua kutimua mbio na kumwacha mwenzao mmoja ambaye tayari alikuwa amezungukwa na wananchi.

  Alisema kuwa katika purukushani hiyo kati ya wananchi na majambazi hao mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye ni dereva wa gari la wagonjwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa aliyetambuliwa kwa jina la Mashaka alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na jambazi hilo lililouwawa kwa kipigo.

  Hata hivyo alisema sababu za wananchi kuamua kuua jambazi hilo ni kutokana na kuonyesha jeuri kwa wananchi baada ya kukamatwa.

  " Huu mtaa tumekumekuwa na utaratibu wa kujilinda wenyewe kwa kuweka umoja pale mkazi wa eneo hili anaposikia kelele za mwizi lazima anatoka akiwa kamili ndio sasa majambazi wakiingia Mkimbizi hawatoki hata kama mtu atalala mlango wazi hakuna jambazi ama kibaka atakayejaribu kuingia ndani...."

  Pia alisema hivi sasa kazi kubwa inayofanywa na wananchi wa eneo hilo ni kuendelea kuwasaka vibaka wenzake zaidi ya watatu ambao majina yao na sura zao zilitambuliwa na wananchi waliofika katika tukio hilo la kupambana nao usiku wa kuamkia jana.

  Hata hivyo alisema kibaka huyo aliyeuwawa bado halijafahamika pamoja na kupelekwa katika hospitali ya mkoa kwa ajili ya wananchi kutambua ila sehemu kubwa ya wananchi wa mji wa Iringa wameshindwa kuutambua mwili wa jambazi huyo ambao umeharibiwa vibaya kwa kucharangwa mapanga .

  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mwili huo ukiwa umekatwa miguu ,mikono na kichwa kikiwa kimekatwa katwa mapanga kiasi cha sura yake kushindwa kujulikana.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa (ACP) Evarist Mangalla alimthibitishia mwandishi wa habari hizi kuwepo kwa tukio hilo la wananchi kuua kuua kibaka huyo .
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...