Hii website ya kenyans.org inaonyesha kazi za vijana wote wa East africa,kama ambavyo TV au website za kibongo zinavyoweza kuwaonyesha vijana wa kenya au Uganda lakini si dhani kama kuna mahali wanawatambulisha vijana wetu km ni wakenya.
Sasa kwanini mnakuwa na tabia za wizi? Halafu mnataka EAC, lengo lenu ni kuendelea kuziibia nchi nyingine kirahisi kwa mwamvuli wa hiyo jumuiya sio?Nimefurahi kuona hili jibu kwani nilikua nimeanza kujiuliza maswali kadhaa.
Hamtashangaa kujua kwamba mimi ni mkenya na niko Kenya.
Sikujua kwamba hii forum sana ni ya wa Tanzania lakini sidhani mta ni
fukuza.
Ha ha ha ati tuliwaibia mlima kilimanjaro, aje?
Madini, hiyo inawezekana kwani yalikua yakipitishwa mpakani hadi Kenya
hata hivi sasa nafikiri bado jambo hili la endelea.
Hii website ya kenyans.org inaonyesha kazi za vijana wote wa East africa,kama ambavyo TV au website za kibongo zinavyoweza kuwaonyesha vijana wa kenya au Uganda lakini si dhani kama kuna mahali wanawatambulisha vijana wetu km ni wakenya.
mimi nadhani wabongo tuna tabia ya uoga, au niseme paranoia. hivi ni wapi waliposema marlaw ni mwanamuziki kutoka kenya?
ina maana ukienda eastafricantube.co ukakuta nyimbo za burundi au rwanda, basi automatically watanzania tumeiba wasanii wa nchi hizo mbili - kwa mfano.
isitoshe hapo wa kulalamikiwa ni youtube ambao wana-host hizo video, in a way hata wewe ukiwa na website unaweza ku-link directly - zipo you tube za kumwaga.
nadhani wakati mwingine wajumbe tunakosa uelewa wa mambo, tuwe wadadisi na kutafuta majibu kabla ku-rush kubandika post. we're exposing ourselves. yapo mambo yanayofanywa na wakenya ambayo hayakubaliki, but this one sioni issue hapa.