Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wanabodi,
Ni masikitiko yangu makubwa kwa mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii, hasa baadhi ya watu ambao wameamua kuitumia kwa maslahi yao binafsi.
Mh. Rais nakumbuka aliwahi kusema kuwa serikali yake itakuwa pia ikizifanyia kazi taarifa za mitandaoni, ilikuwa ni jambo jema sana kwa kuwa ingekuwa ni sehemu ya kupata habari ambazo zinatoka moja kwa moja kwenye jamii hata kwa level ya chini kabisa.
Lakini sasa hii mitandao ya kijamii imekuwa ndiyo sehemu ya uzushi, fitina, uchonganishi husuda na mambo mengine mengi ambayo yanaweza kuhatarisha amani na usalama wa taifa letu kutokana na mijadala mingine inayokuwa na chembechembe za udini.
Nasema haya si kwa mawazo yangu tu bali kuna ushahidi uliodhahiri kuwa sasa mitandao ya kijamii inatumika vibaya hasa humu jamii forum ambapo watu wana majina ya bandia. Kwa mfano kuna uzi mmoja umeanzishwa jana unasema "Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi za juu kuulinda mkataba wa Lugumi". Huu ni uzushi mkubwa kwa sababu mtu huyu kabadili maneno yaliyosemwa na Rwegasira wakati anahojiwa kwa simu na mwandishi wa The Guardian. Alijibu "I have special directives from the Public Accounts Committee. So far I have not submitted the contract to any authority". Je, haya maneno tafsiri yake katika ile "thread" ni sahihi? Je, alibadilisha maneno kwa faida gani?
Kwenye jukwaa la siasa kumekuwa na ushabiki utadhani wa Simba na Yanga hata katika mambo ambayo ni maslahi ya Taifa.