Wanamgambo 800 Boko Haram wajisalimisha Nigeria

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Wapiganaji 800 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wamejisalimisha kwa jeshi la Nigeria.
Hatua hiyo inafuatia mpango mahsusi wa 'Operation Safe Corridor' unaolenga kuwapokea wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.

Chini ya mpango huo wapiganaji wanaojisalimisha wanachukuliwa na kufunzwa upya njia mbadala ya kujitafutia riziki.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa wanania ya kuwasamehe wapiganaji wa Boko Haram watakaotubu makosa yao.
Kwa sasa wamewekwa kwenye makazi maalum ambapo wanaendelea kupata mafunzo ya msimamo wastani wa kidini.

Baadaye watafunzwa mbinu mpya za kujitafutia riziki kabla ya kupewa mtaji wa kuanza upya maisha yao.
Hata hivyo kuna hofu iwapo jamii itakuwa tayari kuwapokea wapiganaji waliotekeleza maasi dhidi yao.

Wahanga wa maasi yao ndio wanaotarajiwa kuwa na wakati mgumu zaidi kuwapokea ama hata kuwasamehe wapiganaji hao wa zamani.
Eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ndilo lililoathirika sana na mashambulizi ya Boko Haram.

Zaidi ya watu 10,000 waliuawa huku takriban wakaazi milioni moja wakitoroka makwao tangu uasi huo uanze yapata miaka 7 iliyopita.


Chanzo: BBC
 
Hata kama watajisalimisha bado haitosaidia kupunguza machungu ya wale waliopoteza wapendwa wao,.
Kikubwa wafikishwe mbele ya sheria na waadhibiwe kwa mujibu wa sheria ya nchi yao.
 
Isije ikawa njia ya kuingia uraiani na kufanya mabaya zaidi. Wawaweke muda mrefu kambini ili kuwabadilisha msimamo, sio kitu rahisi ila with patience kinawezekana
 
Back
Top Bottom