Wanakula kondoo wachanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanakula kondoo wachanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gozigumu, Mar 13, 2009.

 1. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mchungaji wa Pentekoste mbaroni kwa tuhuma za kubaka wanafunzi

  Na Shija Felician,Kahama

  RAIA mmoja wa Rwanda anayedaiwa kuwa ni Mchungaji wa makanisa ya Pentekoste Tanzania, anashikiliwa na Polisi wilayani Kahama,kwa tuhuma za kuwabaka kwa zamu, wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi Nyahanga.

  Mchungaji huyo (Jina linahifadhiwa) anadaiwa kufanya vitendo hivyo kati ya Septemba mwaka jana na mwaka huu alipokamtwa.

  Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mchunganji huyo alikuwa akifanya ubakaji huo nyumbani kwake Nyahanga, karibu na shule wanayosoma watoto hao wa darasa la sita.

  Inadaiwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wanakwenda nyumbani kwa mchungaji huyo ambaye inasemekana alikuwa anawafungia chumbani kwake na kuwabaka kwa zamu.

  Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akiwashawishi watoto hao kwa kuwapa kalamu, soksi za shule na fedha zisizozidi Sh 1,000, kama kifunga mdomo, baada ya kuwabaka.

  Hata hivyo uongozi wa Kanisa la hilo wilayani Kahama, linalodaiwa kuwa ni mwajiri wa Basongela, lilimkana.

  Badala yake, kanisa hilo limemtambua mtuhumiwa kuwa ni muumini na msharika wa kawaida na kwamba lilimpokea kutoka makanisa ya T.A.G na E.A.G.T ya wilayani hapa.

  Habari za awali zilidai kuwa mtuhumiwa alikuwa amefukuza kutoka katika makanisa hayo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga,Shaibu Ibrahimu, alithibitisha habari kuhusu kushikiliwa kwa mchungaji huyo na kwamba polisi wanakamilisha taratibu za kumpima afya yake ili kuona usalama wa afya za watoto hao.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  I wonder... what`s people eating these days... that seems to corrupt their heads...!
   
 3. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi ndizo nyakati za mwisho na ishara zake ndo hizi,kwa hiyo tunapaswa kumuomba mungu sana,wachungaji wachungaji napata shida kidogo kulitamka,maana siku hizi mtu akiweza kukariri mstari miwili tu ya bibilia anajiita mchungaji!zamani mchungaji lazima uende chuo sio kuibuka tu hovyo hoyo mtaani,sasa hivi tuna kila aina ya wachungaji na hawishii hapo wamefikia mahali wanajiita manabii huu ni wizi mtupu! nabii gani wanapatikana mjini tu?nabii gani hana ishara yeyote aliyo ifanya?au kudanganya watu na kujaza kanisa ndo unabii huo? mi naomba haya makanisa ya TAG waanzishe chuo cha uchugaji ili waweze kuwasajili wachungaji watakao pitia hapo na hii itawsadia kuepusha kila wakati kukanusha mchungaji siyo wao na kuingiliwa na matapeli wanao haribu jina uchungaji.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Anakula kondoo wachanga :D ,nafikiri amewafanya mateka na kuwageuza as wake zake si unajua wanapata mafundisho kutoka katika Deuteronomy 21:10-14 .
   
Loading...