Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 972
- 1,150
Imetokea katika kijiji kimoja wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe. Nyanda za juu kusini. Mmiliki wa Mbwa alitoa malamiko yake kwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji kwa madai kuwa kapotelewa na Mbwa wake, baada ya kufanya msako, walimshuku mkazi huyo mtuhumiwa, mwanzoni alikana kuhusika, baadae akakubali na maelezo yake ya utetezi ilikuwa kama ifuatavyo.
"Mbwa wamekuwa wakila mifugo yangu mara kwa mara nyumbani kwangu kama kuku n.k, ndiyo nikachukua hatua ya kuweka mtego na kubahatika kumnasa mbwa huyo,kisha kumfanya kitoweo".
Mmiliki wa Mbwa huyo amelalamikia hatua hiyo, na kudai alipwe kwa mbwa wake huyo kuuwawa na kufanywa kitoweo. Aidha Mwenyekiti wa kijiji hicho amewataka Wananchi kutokujichukulia sheria mikononi.
Chanzo: Best FM Radio.