Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Serikali ya Ivory Coast inaendelea kufanya mashauriano na wanajeshi nchini humo, ambao walifanya maandamano katika miji mbalimbali nchini humo.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalimalizika miaka kadhaa iliyopita lakini Serikali ingali ina changamoto kubwa kuuunganisha taifa hilo ambalo lingali lina dalili za utengano baada ya mapigano ya muda mrefu.
Waasi walishambulia mwanzo katika mji wa katikati mwa nchi wa Bouake. Mbunge wa aneo hilo anasema kuwa wanajeshi hao wanataka wapewe Dola 8,000 na nyumba kwa kila mmoja wao.
Wanajeshi pia walifanya maandamano katika Korhogo, Daloa, Daoukro na Odienne.
Karibu wote walioasi ni wale waliokuwa waasi wa kundi la Forces Nouvell, lililosimamia Kaskazini mwa nchi hadi mwisho wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.
Walishirikishwa katika jeshi lakini wanasema kuwa wangali wanaidai Serikali kiwango fulani cha pesa cha ule muda waliokuwa waasi.
Serikali ililazimika kulipa pesa chini ya mpango kama huu na kwa sasa imejikuta katika hali ya kutafuta pesa zingine kama hizi ili kuwalipa wahusika.
Chanzo: BBC