Wanajeshi wa Marekani Wanaojiua Wazidi Kuongezeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wa Marekani Wanaojiua Wazidi Kuongezeka

Discussion in 'International Forum' started by Dr. Chapa Kiuno, Nov 19, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  </SPAN>


  Wanajeshi wa Marekani Wanaojiua Wazidi Kuongezeka

  Idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaojiua baada ya kurudi kutoka kwenye vita vya Iraq na Afghanistan imezidi kuongezeka kwa kasi kiasi cha kwamba wanajeshi 140 wa Marekani walijiua mwaka jana na idadi kama hiyo tayari wameishajiua mwaka huu.


  Jumla ya wanajeshi 140 wa Marekani walijiua mwaka jana na kufanya idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaojiua kila mwaka kuzidi kulitishia amani jeshi la Marekani.

  Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Marekani zilizotolewa hivi karibuni, idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaojiua wenyewe baada ya kurudi toka kwenye vita vya Afghanistan na Iraq imezidi kuongezeka kwa kasi na katika mwaka 2008 idadi ya wanajeshi waliojiua ilikuwa kubwa zaidi kuliko idadi ya raia wa kawaida wa Marekani waliojiua.

  Idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaojiua ilianza kuongezeka tangia mwaka 2004 na hali hiyo imezidi kuendelea hadi mwaka huu ambapo kuanzia mwanzoni mwa huu hadi sasa idadi ya wanajeshi waliojiua wenyewe imefikia 140 na inatarajiwa kuwa mpaka mwishoni mwa mwaka huu idadi hiyo itaongezeka zaidi.

  Hivi karibuni mwanajeshi wa Marekani katika kambi ya Fort Hood iliyopo nchini Marekani aliyekuwa kwenye maandalizi ya kupelekwa kulitumikia jeshi la Marekani nchini Afghanistan aliwaua kwa kuwapiga risasi wanajeshi wenzake 13 kabla ya kutiwa mbaroni baada ya kujeruhiwa kwa risasi.

  Katika mahojiano na CNN, jenerali George Casey alisema kwamba jeshi la Marekani linafanya jitihada zote ziwezekanazo kupunguza idadi ya wanajeshi wanaojiua kwa kuanzisha programu mbali mbali za kuwapa matibabu ya kisaikolojia wanajeshi wanaorudi toka vitani.

  Jenerali Casey alisema kwamba mwanajeshi anayetumia mwaka mmoja vitani, huhitaji zaidi ya miaka miwili kuweza kurudia maisha yake ya kawaida.

  Sababu kubwa inayosemekana kusababisha wanajeshi wengi wa Marekani kujiua ni stress wanazokuwa nazo baada ya kurudi toka vitani, unywaji wa pombe uliokithiri na utumiaji wa madawa ya kulevya.  Source: NIFAHAMISHE
   
 2. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,875
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa vyema kwani nani aliwatuma huko?
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Natamani wangewalipua na wengine mtaani kama alivyofanya yule hassani...laana ya kuua watu iraq na afghanistani bila haki haitawaacha
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuingia jeshini ni kujiua, kinachofuatia ni mmomonyoko kuendelea tu. trust me, I have seen them.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Tena itawaandama mpaka makaburini mwao!
   
Loading...