Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamchoma moto mwanajeshi wa Korea Kusini

Miki123

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
288
502
Wanajeshi wa korea kaskazini wameonyesha mfano wa kutovumilia yoyote anayehatalisha hali ya usalama ya taifa hilo.
Wanajeshi wa kim jong un jumanne ya wiki hii wamemchoma moto na kumpiga risasi mwanajeshi wa korea kusini kwenye eneo lenye ulinzi wa hatari DMZ.

Mwanajeshi wa korea kusini alikuwa yupo rindoni baharini upande magharibi wa rasi ya korea. Akiwa na boti yake ya dolia mjeshi huyo alizama kwenye maji ya bahari na kuogelea kuelekea upande wa Korea kaskazini. Wakati akiwa kwenye chombo kilichomsaidia kuelea wanajeshi wa korea kaskazini waliokuwa kwenye doria walimuona.

Wakaanza kumuhoji, inashukiwa mwanajeshi wa korea kusini alieleza nia yake ya kukimbilia korea kaskazini lakini wanajeshi wa korea kaskazini hawakulizishwa na maelezo.

Baada ya masaa sita walimpiga risasi na kuutia moto mwili wake.

Hivi karibuni kim jong un alitoa amri watu wanaotorokea korea kaskazini kwenye mipaka wapigwe risasi kama njia ya kuzuia kuingiza corona toka nje ya nchi, hilo lilisemwa baada ya mkorea kaskazini aliyetorokea kusini kuamua kurudi kwao kwa kuvuka mpaka wa korea kaskazini na kusini na kisha kukutwa na corona.

Shooting of official puts inter-Korean relations in tangle
 
Something fish, hii ishu lengo lake ni kuongeza mzozo, baada Moon jae-in wa South korea kuinishiate juhudi za ushirikiano na North na pia kusign defence agreement na Mchina
 
Back
Top Bottom