Wanajaribu kuzuia gharika la UKAWA

Wanajaribu kuzuia gharika la UKAWA

Mimi mwana CCM Kindakindaki naapa kuwa nitampigia kura Edward Ngoyai Lowassa anayeiwakilisha CHADEMA kupitia mwamvuli wa Muungano wa vyama vya UKAWA. Kama kunawakati ambapo CCM inahitaji kujipanga vyema na kurekebisha mapungufu yaliyopo wakati huo ndio sasa.Kwa yeyote anayeipenda CCM kama mimi,naomba kwa Moyo Mkunjufu tuiweke CCM pembeni ili ikajikague,ikajitafakari na kisha ijipange kwa ajili ya 2020 - 2025.Gari ama mashine yeyote ile hata iwe tingatinga ikiharibika sharti iwekwe pembeni ili ifanyiwe marekebisho.Ukiilazimisha iendelee na kazi ama iendelee na safari madhara yake ni makubwa sana kwa abiria,mazingira na hata watu waliokaribu na mashine hiyo!!Kataa vitisho,kataa kununuliwa kama bidhaa,kataa uchochezi,kataa michezo michafu ya Kisiasa...Jiandae kupiga kura yako kwa Diwani,Mbunge na Rais wa UKAWA.....MUNGU ibariki TANZANIA na watu wake wote!!

Hata wewe bosi wangu hr wangu hee
 
Lowasa ataingia ikulu ya magogoni dar. Pombe labda ikulu ndogo ya dodoma coz atakuwa mwenyekiti wa maviccm
 
Samahani mtoa mada hivi yale maneno waliyosema wale NCCR kuwa Chadema inauwa vyama vingine ni uwongo? Kweli chama kilichosimamisha wagonbea 67 mwaka 2010 leo 2015 kina wagombea ubunge 12 na 6 kati yao wanapingwa na wana Ukawa wenzao hakidhoofiki kweli na kufa. Tafakari.
Umuhimu Wa mfumo Wa vyama vyingi sio uwepo wa vyama kumi au zaidi. Bali ni namna gani chama au uwepo Wa vyama viwili au vitatu vinaweza kuleta mabadiliko ili kuleta mabadiliko yenye tija Kwa taifa letu la Tanzania na sio uwepo Wa utitiri Wa vyama visivyokuwa na malengo madhubuti Kwa ajili ya ukombozi Wa kweli, kumbuka ndugu yangu vyama pinzani Maslahi yaani vipo kimaslahi zaidi. kwahiyo kama vyama pinzani vina malengo yanayoshabiana hawana kushirikiana katika kuleta mabadiliko ya kweli na ubabaishaji unaoendelea hapa kwetu kumbuka shida yetu sio uwepo Wa vyama 21 au zaidi shida yetu ni maendeleo ya nchi, sasa swali chama gani kinatufaa Kwa kuangalia Sera na Ilani zao.
 
Katika kile ambacho kinaelezwa ni kubanwa kwa CCM, chama hicho kikongwe sasa kimekuwa kikijaribu kila mbinu kujinasua katika kibano cha UKAWA.Kuna taarifa kwamba CCM inawanunua baadhi ya viongozi wa UKAWA kwa kuwarubuni na kuwapa propaganda za uongo kuhusu UKAWA. Huku kikiwa kinayatumia mapungufu yalipo ndani ya UKAWA.

Moja ya propaganda ni kuhusu taarifa za kwamba Edward Lowassa amewanunua viongozi wa UKAWA kwa maslahi binafsi.Taarifa hizi zinaeleza kwamba kuna viongozi watajitoa kutoka miongoni mwa UKAWA na kudai kwamba viongozi wa juu hawawatendei haki. Tayari hilo limefanyika NCCR Mageuzi ingawa linaonekana halina nguvu.Mtoa taarifa kutoka ndani ya CCM katika timu ya kampeni anayemuunga mkono Lowassa anasema,''huu mkakati ni kama utashindikana kwa sababu ukiangalia wananchi tayari wameshaamua''.

Mtoa taarifa wa habari hizi ni kiongozi mwandamizi wa CCM ambaye huzunguka na mgombea urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli na hakutaka kutajwa jina lake kuhofia usalama wake.Tayari baadhi ya viongozi wa NCCR Mageuzi wamejiondoa kutoka miongoni mwa UKAWA, kwa madai kwamba, mwenyekiti wa chama hicho hawasikilizi. Mtoa taarifa kutoka ndani ya CCM anasema, ''suala la NCCR Mageuzi linahitaji busara sana, tayari walishakaa na wakaamua kuhusu majimbo leo wanajitokeza walikuwa wapi?'' akongeza, ''Hii ni kuwaumiza wananchi ambao wapo tayari kwa ajili ya mabadiliko''. Huku akiongea kwa kujiamini anaongeza, ''mimi niko huku(yaani CCM) kwa sababu nahofia usalama wangu ila namuunga mkono Lowassa na wananchi walio wengi''.Akaongeza kwamba mbinu za Lowassa zinabadilika sana na hatabiriki ndiyo maana CCM wanashindwa na kila wanapojaribu inajulikana.

Huku akisisitiza kwa njia ya simu, alisema, hakuna sababu ya wananchi na wapenda mabadiliko kukata tamaa', unapoona haya na kusikia haya ujue mwisho wa adui unakaribia''. Akaongeza kwamba ni muhimu sana kwa wakati kama huu kuwa wamoja.Chama cha NCCR Mageuzi kimetoa tamko kutotambua waliojiengua kwa kusema kwamba hawakufuata taraibu ndani ya chama na kwamba wanatumika, na kimewataka wananchi kujitokeza kumpigia kura Edward Lowassa.

Aidha kutakuwa na umoja utakao undwa kutokana na wanaojiengua na umoja huo utakaoitwa UKAWA utakuwa na baadhi ya wanaUKAWA waliojiengua kutoka UKAWA na utahamasisha ili kuungwa mkono na wananchi huku ukiratibiwa kwa karibu na vituo vya habari vya STARTV na TBC. Miongoni mwa watu watakao unga mkono umoja huo ni Dr Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA. Maneno ya kimkakati ni Mbeya, Dar Es Salaam na mengine watakayoona yanafaa.Anaongeza, ''tafadhi nyinyi waandishi waambieni wananchi na wapenda mabadiliko wasitetereke kabisa, haya yote yatapita na ndiyo misuko suko ya mabadiliko''. ''Sasa hivi wamemwachia January Makamba, ndiyo kila kitu sasa unaona tunavyoyumba''(wao CCM), alisema.

Iwapo hilo litashindikana wataunda umoja wa vyama vingine vya upinzani vikihusisha ACT Wazalendo, UDP na vyama vingine ikiwa ni mkakati wa kuiokoa CCM, kwa kugawa kura na kuwachanganya wananchi ili wakate tamaa ya kupiga kura.Mlinzi mmoja wa timu ya Magufuli aliyejulikana kwa jina moja la Juma amemwambia mwandishi wa habari hizi kwamba hali ya chama hicho kikongwe ni mbaya na hasa katika masuala ya kifedha na kusababisha kuomba msaada kwa marafiki zake wa nje(hakutaja ni nchi gani).''Nakuambia hivi hatushindi waandishi pengine mmeshajua hili kwamba hatushindi, tunalazimisha tu''. Alisema kwamba wingi wa watu katika mikutano ya CCM ni kwakuwa wanasomba watu na Malori na kuwapa hongo(baadhi) kuanzia shilingi 5,000-10,000.

Acha yafe na udhalimu wao
 
Watasubili sana Ukawa kuisambalatisha,zama hizi ni za sayansi na teknolojia,wao wamebaki na mbinu za kizamani.
 
25 October mapema sana na kichinjio changu
 
Kanyaga twende,nimeipenda sana slogan ya hata "Mbowe akijitoa UKAWA sisi tunaendelea
kuunga mkono mabadiliko kupitia ukawa."
 
wasichokijua ccm ni kuwa kwasasa ushindi wa Lowasa upo mikononi mwa wananchi na sio mikononi mwa viongozi wa Ukawa,kwa kifupi Lowasa yupo katika mioyo ya Watanzania wengi
 
Back
Top Bottom