Wanajamvi maneno haya yana ukweli kiasi gani?

Evvy jr

Senior Member
Apr 23, 2017
148
188
Siku ya jana nikiwa sehem yangu ya kazi, nikiwa nimepumzika nilipata nafasi ya kuongea na mdada flani ambae tunafanya nae kazi. Yalikua ni mazungumzo ambayo kwa kiasi flani yalinifungua akili katika kuwaelewa hawa ndugu zetu (wanawake).

Kwanza alianza kwa kuniuliza kwa nn huwa hanioni nikijihusisha na mambo ya mahusiano na hajawahi kuona kama nina mpenzi. Nilichomjibu ni kwamba, "kwa majukum yangu na malengo yangu kama kijana niliyojiwekea nahisi nikiwa kwenye mahusiano/nikiwa na mtu sitamtimizia mahitaji yake mengi kutokana na hali yangu ya kiuchumi navyoiona pamoja na majukum yanayonikabili. Mapenzi ya sasa ni pesa, kama huna pesa ni vigum kupendwa au kuonyeshwa mapenzi ya kweli,, kwa hiyo mpaka pale hali yangu ya kifedha itakapokua sawa na majukumu yangu kupungua ndipo nitaanzisha mahusiano"

Yule dada alicheka sana kisha akazungumza mambo yafuatayo
"Mnakosea sana kuwaza hivo, si kweli kwamba tunahitaji sana hizo pesa zenu. Tunachohitaji ni kututengenezea moments ambazo zitatufanya tuwe tunawawaza kila mda. Mwanamke unaweza kumtoa out tena mkaenda sehem ambayo mtatumia hata 10000 na akaona umemjali na unamthamini. Mwanamke mtengenezee matukio madogomadogo mazuri na hatakusahau milele. Hata kutembea pamoja kwa miguu au kumpigia simu kumjulia hali na kumpigisha story za hapa na pale ni moments ambazo zitamfanya awe anakukumbuka kila siku. Mwanamke hahitaji mambo makubwa ili akupende kama mnavyodhani"

Alinitolea mfano kwa kusema "Ushajiuliza kwa nn akina mama wanapenda vijana wadogowadogo, ni kwa sababu watu wazima wengi wanajisahau, wanakua busy sana wanashindwa kutenga mda kwa ajili ya wapenzi/wake zao. Ni kweli suala la sex linachangia lakin hawa vijana wadogo wanajua kutengeneza hizi moments nazokwambia. Kwa hiyo bro acha uoga, majukumu hayaishi, hali ya uchumi isikufanye ukose mahusiano"

Mada hii iliungwa mkono kwa kiasi kikubwa sana na wadada wengine waliokua pale. Wote walitetea kwamba kumtengenezea moments mpenzi ndio kitu kikubwa kitakachofanya akupende na akukumbuke wakati wote. Na wakaongeza kuwa, hata mkiachana vitu vinavyofanya mwanamke amkumbuke mwanaume ni hizo moments nzuri.

Wanajamvi maneno haya yana ukweli kiasi gani?
 
Mkuu naona shikilia msimamo wako kwanza tafuta hela jiweke stable kiuchumi haya mengine tutayakuta huko.. Sasa we ingia kichwakichwa kwa kufuata hiyo gharama ya buku kumi tu!.. mi mpk leo siamini kuhusu mapenzi tu bila uchumi kila nikipiga hizo hesabu ngoma inagoma jibu linakuja lilelile!.. si maanishi kuwa mpenzi bora utampata kwa hela no bali awe bora asietaka hela au anataka lkn mapenzi mtake msitake yanagharama tu.
Mambo ni mengi muda ni mchache
 
Asilimia 90 ya wadada hawajui hata wanataka nini kwenye mahusiano . achilia mbali suala la ukuaji..watu wana grow differently..

Leo anataka handsome wa kum post..
Kesho anataka wa kumlipia kodi hata kama sura kawaida..
Keshokutwa anataka wa kumtosheleza kitandani..

Baadae anataka wa kumshauri biashara zake na kumsimamia mipango ya maisha..

It never stops with humans especially women

Anachotaka Leo kesho anaweza asikitake tena
 
Kiufupi mwanamke anataka sampuli zote za wanaume awe nazo.
 
Siku ya jana nikiwa sehem yangu ya kazi, nikiwa nimepumzika nilipata nafasi ya kuongea na mdada flani ambae tunafanya nae kazi. Yalikua ni mazungumzo ambayo kwa kiasi flani yalinifungua akili katika kuwaelewa hawa ndugu zetu (wanawake).

Kwanza alianza kwa kuniuliza kwa nn huwa hanioni nikijihusisha na mambo ya mahusiano na hajawahi kuona kama nina mpenzi. Nilichomjibu ni kwamba, "kwa majukum yangu na malengo yangu kama kijana niliyojiwekea nahisi nikiwa kwenye mahusiano/nikiwa na mtu sitamtimizia mahitaji yake mengi kutokana na hali yangu ya kiuchumi navyoiona pamoja na majukum yanayonikabili. Mapenzi ya sasa ni pesa, kama huna pesa ni vigum kupendwa au kuonyeshwa mapenzi ya kweli,, kwa hiyo mpaka pale hali yangu ya kifedha itakapokua sawa na majukumu yangu kupungua ndipo nitaanzisha mahusiano"

Yule dada alicheka sana kisha akazungumza mambo yafuatayo
"Mnakosea sana kuwaza hivo, si kweli kwamba tunahitaji sana hizo pesa zenu. Tunachohitaji ni kututengenezea moments ambazo zitatufanya tuwe tunawawaza kila mda. Mwanamke unaweza kumtoa out tena mkaenda sehem ambayo mtatumia hata 10000 na akaona umemjali na unamthamini. Mwanamke mtengenezee matukio madogomadogo mazuri na hatakusahau milele. Hata kutembea pamoja kwa miguu au kumpigia simu kumjulia hali na kumpigisha story za hapa na pale ni moments ambazo zitamfanya awe anakukumbuka kila siku. Mwanamke hahitaji mambo makubwa ili akupende kama mnavyodhani"

Alinitolea mfano kwa kusema "Ushajiuliza kwa nn akina mama wanapenda vijana wadogowadogo, ni kwa sababu watu wazima wengi wanajisahau, wanakua busy sana wanashindwa kutenga mda kwa ajili ya wapenzi/wake zao. Ni kweli suala la sex linachangia lakin hawa vijana wadogo wanajua kutengeneza hizi moments nazokwambia. Kwa hiyo bro acha uoga, majukumu hayaishi, hali ya uchumi isikufanye ukose mahusiano"

Mada hii iliungwa mkono kwa kiasi kikubwa sana na wadada wengine waliokua pale. Wote walitetea kwamba kumtengenezea moments mpenzi ndio kitu kikubwa kitakachofanya akupende na akukumbuke wakati wote. Na wakaongeza kuwa, hata mkiachana vitu vinavyofanya mwanamke amkumbuke mwanaume ni hizo moments nzuri.

Wanajamvi maneno haya yana ukweli kiasi gani?
Bila hela hakuna mapenzi we boya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom