WanaJamiiForums nakuja kwenu kukiri maisha ni magumu, naomba mnisaidie nipate kazi

Naunga mkono hoja.
Sisi huku kwetu tunaitumia elimu kuonekana watanashati na kuchanganya maneno ya kiswahili na english mbele za watu.
Siyo kweli. Sema tu kuwa elimu hii tangu tuletewe na wenyewe hatujajua malengo yake ni yapi. Sisi tumeigeuza kuwa nyenzo ya kutupatia utajiri wakati hilo siyo lengo lake mama. Mbona ilikotoka imeweza kuwakomboa? Sisi tunakwama wapi?
 
Mkuu Da'Vinci nakuunga mkono!

Tanzania elimu kama elimu kumsaidia mtu moja kwa moja kwa wakati huu hakuna hiko kitu maana hata akipata ajira mshahara wenyewe mdogo haukidhi mahitaji kumtoa mtu kwenye umasikini,kama upo uwezekano kukikwepa hiki kipengele kwenye maisha,bora muhusika afanye hivyo mapema.

Ndiyo elimu ni muhimu sana ila tukubali tukatae kwenye maisha asili na halisi ya Mtanzania haina tena msaada,maana bora nisisome then nikutane na kiboko cha maisha sitakuwa na cha kulaumu sana ila nitakaza kiubishi kupambana na uzembe wangu ila nimepoteza miaka minne ndani ya kuta nne kisha nirudi mtaani nikidhani kuna maisha nijikute ndani ya hali hiyo....huwezi kuwa sawa kiakili utachizika na wengi mtaani wapo ktk hali hiyo ni kwa vile wanajikaza tu!!!

Naomba nikuelimishe kidogo mkuu Sir_Mimi halafu nawewe utawaelimisha wenzio kama yule mjingamimi.

JAMII inamhukumu vibaya mtu aliyesoma na kufeli maisha tofauti na yule ambae amefeli na hakusoma kabisa. Ila kuna kitu kimoja ambacho jamii haijakielewa.

KUSOMA ni njia moja wapo ya kutafuta maisha, njia zingine ni kama BIASHARA, MZIKI, UIGIZAJI, MPIRA na fani zingine..Yaani ni kama vile unapoutafuta ufalme wa mbingu kuna njia nyingi, unaweza ukawa mkristu, muislamu, mhindu au budha..kila mtu kwa imani yake ana lengo la kumtafuta Mungu.

ILA inabidi uelewe, sio wote waliosoma wamefanikiwa, sio wote wasanii wamefanikiwa, sio wote wachezaji wamefanikiwa na sio wajasiriamali wote katika fani tofauti wamefanikiwa. Lengo la anaesoma na anaefanya mziki au utangazaji ni kufanikiwa (na zote ni njia sahihi kabisa). Sasa, Ukiona plan A yako imefeli (labda umesoma au nimfanya biashara), badilika na ingia kwenye plan B.. Mbona ni kitu cha kawaida.

Tatizo linakuja pale ambapo jamii inawaona watu wote ambao plan A zao zilikuwa ni shule kama watu ambao hawatakiwi kufeli katika maisha..Ikitokea wamefeli basi hupuuzwa na kuonekana kuwa walipoteza muda huko mashuleni/vyuoni.

Jamii inasahau kuwa kijana aliyefeli kimaisha kupitia plan A ya elimu hana tofauti na kijana aliyefeli kimaisha kupitia plan A ya mziki/mpira au biashara.

Wakuu badilisheni mitazamo, mnawaweka kwenye presha kubwa sana vijana na mnawafanya wawe na failure mentality.


FOHADI: Focus Hardwork Discpline
 
mwanao akiwa anasoma sekondari, jitahidi ajifunze kimoja katika hivi kwenye muda wa ziada.

1. Motorvehicle mechanics.
2. Welding and fabrication.
3. fitter and turner.
4. jitahidi awe na leseni ya udereva na cheti cha
NIT.
5. Computer and cell technician.
6. Constr and mining equipment operator.

Pia huko shule ajifunze kuongea kiingereza kifupi kuwasiliana kwa kikristo, msidanganywe na wanasiasa muandae watoto kadili inavyofaa..
Mwanao akimaster kimoja kwenye hivyo hata amalize chuo kikuu atajua namna ya kuishi huku anaangalia mambo mengine..
Mwanangu mimi nina leseni C lakini kazi Sipati,... Kila kitu kina wakati wake broo hata mimi napitia changamoto.. Ila naamini One day yes

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Msomi mbona sheria fani nzuri tu unakwama wapi learned Bro?

Anyway, vipi unazijua procedure na practical ya system nzima ya BRELA? Yaani unaweza kufanya kazi zinazohusu hao jamaa?

Kama ndio, anza kutembelea watu mbali mbali wanaofanya biashara washawishi wa comply na requirements za sheria kwa Dar huwezi kosa hata 5 kwa mwezi angalau utapata kitu but don't undercut or over charge its an ethical msomi.

Vipi unaijua vizuri NIS JAMII SYSTEM? na unaweza kuitumia vizuri? Basi tafuta kazi zake hizi ni za ma NGO kusajili sana sana.

Vipi unazijua procedure za kusahili hivi vikundi vya Halmashauri?, vipi kuandika mikataba maana bida boda wengi sana hawana mikataba vipi hao boda boda mtaani hapo ulipo wana kikundi cha kuelimushana? Vipi kwanini usiwashawishi wasajili na kuwaonesha fursa ya kuchukua mkopo Halmashauri? Msomi mbona fani yako nzuri tu!?.

Hizi ni chache nimekuambia sababu na mimi nimezifanya na baadhi bado nazifanya ila msomi nenda Law School kuna vitu utajifunza vingi sana.
 
Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 25,

Nimemaliza chuo mwaka jana na degree ya sheria kutoka Chuo Kikuu kimoja huko Arusha, lakini tangu nimalize chuo niliamua kuhamia Dar es Salaam na kujichanganya kwa vibiashara vya hapa na pale kama mnavyojua tatizo la ajira kwa sasa, kweli nimejaribu sana kuuza hiki na kile kama viatu, nguo, vyakula, ila kila ninachofanya kinafeli mahitaji yanazidi kipato, mpaka muda huu ninavyo andika hapa hata ule mtaji kidogo nao nimelipa kodi.

Nimeuza karibia assets zote nilizonunua kipindi nipo chuo, nimebaki na kitanda na godoro tu na jiko navyo kama maisha yataendelea kuwa hivi nitauza navo nirudi nyumbani tu

Sioni thamani yakusoma kabisa, najuta muda niliopoteza nisingeishi maisha mabaya kama haya, naomba mwenye connections ya kazi zifuatazo anisaidie japo nijiokoe nisiuze kitanda na godoro.
  1. Usaidizi wa kwenye magari ya mzigo,
  2. Saidia fundi, kubeba zege,
  3. Viwandani,
  4. Pia hata udereva naweza ingawa sina leseni ila naweza uza simu nikaipata, nisaidieni ndugu zangu
Vyeti vyote na ushahidi ninavyo.

Nawashukuru sana mungu awabariki ndugu zangu.
Pole sana mkuu, usijate tamaa Mungu yupo utafanikiwa tu.
 
Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 25,

Nimemaliza chuo mwaka jana na degree ya sheria kutoka Chuo Kikuu kimoja huko Arusha, lakini tangu nimalize chuo niliamua kuhamia Dar es Salaam na kujichanganya kwa vibiashara vya hapa na pale kama mnavyojua tatizo la ajira kwa sasa, kweli nimejaribu sana kuuza hiki na kile kama viatu, nguo, vyakula, ila kila ninachofanya kinafeli mahitaji yanazidi kipato, mpaka muda huu ninavyo andika hapa hata ule mtaji kidogo nao nimelipa kodi.

Nimeuza karibia assets zote nilizonunua kipindi nipo chuo, nimebaki na kitanda na godoro tu na jiko navyo kama maisha yataendelea kuwa hivi nitauza navo nirudi nyumbani tu

Sioni thamani yakusoma kabisa, najuta muda niliopoteza nisingeishi maisha mabaya kama haya, naomba mwenye connections ya kazi zifuatazo anisaidie japo nijiokoe nisiuze kitanda na godoro.
  1. Usaidizi wa kwenye magari ya mzigo,
  2. Saidia fundi, kubeba zege,
  3. Viwandani,
  4. Pia hata udereva naweza ingawa sina leseni ila naweza uza simu nikaipata, nisaidieni ndugu zangu
Vyeti vyote na ushahidi ninavyo.

Nawashukuru sana mungu awabariki ndugu zangu.
Hii post inasubiri kupitiwa na Moderators ili iende kwa umma! huku nako sio salama tena
 
Back
Top Bottom