Wanaijeria watatu wanaokabiliwa na kesi ya kukutwa na dawa za kulevya wamwandikia barua DPP na kukiri makosa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Raia watatu wa Nigeria akiwemo mchungaji wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kukiri kosa la uhujumu uchumi linalowakabili.

Washtakiwa hao, Henry Ozoemana Ogwuanyi (mchungaji), Onyebuchi Ogbu na Lucy Oding
wanakabiliwa na kesi ya kukutwa na kilo 15.8 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Wakili wa Serikali, Elia Athanas ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Oktoba 24, 2019 kuwa washtakiwa hao wameandika barua kwa DPP kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayowakabili.

"Washtakiwa wameandika barua ya kukiri makosa yao lakini DPP bado hajajibu barua hiyo, naiomba mahakama ipange tarehe nyingine,” amedai Athanas.

Baada ya maelezo hayo wakili wa utetezi, Hassan Kiangio amedai suala la kuandika barua kwa washtakiwa hao isiwe kikwazo cha kutoendelea na kesi hiyo, kuuomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi ili shauri hilo liende mbele.

Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 6, 2019 itakapotajwa.
Katika kesi ya msingi inadaiwa Aprili 21, 2019 eneo la Msimbazi wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa walikutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 15.8.


Chanzo: Mwananchi
 
Tuwagonge shaba, shenzitaipu kabisa hao igwe wa Buhari;
Yaani; mchungaji na heroin, waliwe vichwa kabisa.

Eti barua ya kuomba msamaha , DPP sukuma ndani hao miaka 60 au waliwe shaba ya vichwa.
 
Ninasubiri kwa hamu kuona maamuzi yatakuwaje kwa kesi kama hii - umekiri kuwa au kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
 
Msamaha hauwahusu

Wauwaji
Wabakaji
Robbery
Madawa ya kulevya
Wasilete Masihara hapa tena Mchungaji hata aibu hana
 
Hawa wakiachiwa basi waliokamatwa na madawa miaka ya nyuma pia waachiwe, inakuaje mtu anaandika barua anaachiwa huku kuna watu wapo jela kwa kosa hilo hilo wanakula miaka mingi
 
Hiyo jamii ya kinageria sijui wanashida gani,kila sehemu wao wanajihusisha na biashara haramu
 
Hawa wanaigeria ni mimi kabisa!
Screenshot_20191025-065132-picsay.jpeg
 
Back
Top Bottom