Wanahitajika vijana wawili haraka!

Wanahitajika vijana wawili haraka!

Niliwahi kufanya kibarua wakati wa ujenzi Udom aisee per day ilikiwa 3000

Chakula nauli chai maji utajua wewe

Nilifanya siku moja tu
Mkuu nilikuwepo kipindi hicho na kilichofanyika pale ni kasumba ya sisi watu weusi kudhulumiana.
Malipo halali kwa kibarua ilikuwa ni elfu 7 kwa maelekezo ya mkandarasi na serikali lakini kwakuwa tumezoea kufanyana fursa wajanja wakaanza kutulipa nusu ya kile tulichostahili.

Ila mwisho wa siku issue ilibumbuluka na wakapandisha mshiko,hata hawa huyo mwekezaji lazima atakuwa katoa fungu kubwa ila kwa kuwa wabongo janjajanga mingi na wabajua ufukara wa wabongo wenzao wanawapiga kama hivyo.
 
...declare interest kwanza!
..ama ndo walewale

Mimi sihusiani na mleta mada na wala simfahamu na pia sijuhusishi na shughuli za IT

Ni mchangia mada tu ila ninaeujua mtaa vizuri na najua kazi za kitaa zilivyo
 
Habari!
Wanahitajika vijana wawili kwa ajili ya kufanya kazi ya masoko ya muda mfupi wa siku saba na malipo ni kwa siku
Elimu
Kuanzia kidato cha nne na kuendelea. Kujua kuongea Kiingereza kwa Ufasaha ni lazima
Majukumu
Kuitangaza bidhaa kwa kugawa vipeperushi na kuwapa maelezo wateja juu ya huduma ya fiber internet.
Eneo
Ni katika majengo yaliyokuwa tayari yameunganishwa na mfumo wa fiber internet. Maeneo hayo ni Upanga, Masaki, City center na Kariakoo.
Utekelezwaji wake
Watapangiwa jengo kutokana na ratiba ya siku hiyo katika eneo husika
Muda
Inatakiwa kufika mapema eneo/jengo lililopangwa kwa siku hiyo kuanzia saa moja asbh hadi saa nne unapumzika. Unarudi saa sita mchana hadi saa tisa unapumzika. Unakuja kuendelea saa kumi na moja jioni hadi saa mbili. Target ni kuwapata wateja wanaofanya kazi na kuishi katika majengo
Malipo
Shilingi 12,000 kwa siku. Gharama za chakula na nauli ofisi haihusiki nazo
Kuanza lini?
Kuanzia Jumatano ya tarehe 24.01.2018
Mawasiliano
Ofisi: Mariam tower, ghorofa ya nne, makutano ya mitaa ya Shaurimoyo na Lindi, Ilala, Dar es Salaam
email: iconsultbuzness@gmail.com
Simu:0659211222/0777777766/0755411455
hata 20 sifanyi
 
Niliwahi kufanya kibarua wakati wa ujenzi Udom aisee per day ilikiwa 3000

Chakula nauli chai maji utajua wewe

Nilifanya siku moja tu
Vipi hakukuwa na nafasi ya kuiba?
Mi nishawahi kumsaidia fundi siku 2 nikawa narudi nyumbani na buku 2, ikabidi nimchombeze fundi kiaina, akanambia mi mwenyewe nilikuwa nakuogopa wewe.
Kuanzia ile siku nilipenda kazi isiishe.
 
Jua lote la utosi juu yko, vumbi lote la town juu yako, nauli kwa mizunguko yote hyo from saa moja morning mpk saa mbili usiku juu yako, chakula juu yako, alafu umlipe mtu buku kumi na mbili?????? Tuwe na huruma, ata kama vyuma vimekaza sio kwa staili hii ya kumtesa binadamu mwenzio. Sote ni wa Mungu.
 
Jua lote la utosi juu yko, vumbi lote la town juu yako, nauli kwa mizunguko yote hyo from saa moja morning mpk saa mbili usiku juu yako, chakula juu yako, alafu umlipe mtu buku kumi na mbili?????? Tuwe na huruma, ata kama vyuma vimekaza sio kwa staili hii ya kumtesa binadamu mwenzio. Sote ni wa Mungu.
Soma vizuri tangazo
Kazi hy sio ya kuzunguka bali kuna majengo maalum ambayo yameunganishwa na waya za fiber kwa ajili ya internet. Hivyo unakuwa na sehemu kama kibanda ndani ya jengo mahala kama karibu na lift mfano. Hivyo watu wanaoingia au kutoka ktk jengo husika unaongea nao na kuwapa vipeperushi. Na kama anakuwa yupo tayari kukaa kuna kahawa na vitafunwa anaweza akapata hy mteja
Mfano mwepesi upate picha kamili, kama upo Dar nenda pale City Mall utaona ndani mule ground floor kuna dizaini ya vibanda ambapo wanauza na kutangaza bidhaa
Mambo yanayotusumbua sana Watz ni kutosima maelezo ya jambo, tunakimbilia tu kutoa comments
 
Acheni uvivu hii ni fursa mpo kitaa tu kazi kupiga mizinga tuu ,12 per day kwa maisha haya ni fair kabisa
Hatujakataa mkuu, lkn ukipiga hesabu vzr utagundua kuwa hyo hela inaishia kwenye usafiri na chakula.
 
Yaani Bora Nikabet tu kuliko kufanya iyo kazi....Halafu mnataka form 4 anaejua ngeri....Kama mnataka kibarua yoyote si mchukue awa wabeba zege mnaosema wanalipwa buku 3 kwa siku wakafanye iyo kaz yenu ya buku 12 mnayosema ni kubwa!!?
 
Back
Top Bottom