kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,940
- 7,849
Kampuni ya TOL ilikua ya kwanza kuuza hisa kwenye soko la hisa la Dar-es-Salaam, lakini cha ajabu tangu kampuni hiyo kutoa hisa zake karibu miaka 20 sasa haijawahi kutoa gawio kwa wanahisa wake hata mara moja.
Kampuni hiyo ilijitangaza kwenye waraka wa kuuza hisa kama yenye ufanisi na matarajio mazuri na kufanya wananchi kumiminika kununua hisa. Walichofanya waliokua wanabodi na menejiment kinaonekana leo katika utajiri mkubwa waliokua nao. Waliwadanganya wananchi.
Hivi sasa wapo wanahisa wachache wameunganisa hisa zao kinyume na taratibu na wanapokezana nafasi za ukurugenzi katika bodi ya kampuni. Hao jamaa kwa kushirikiana na menejimenti wanafanya biashara binafsi na kampuni kwa kupeana zabuni bila utaratibu wa tenda hivyo kula mapato yote ya kampuni.
Kila mkutano mkuu wa wanahisa wanatangaziwa hasara kwa hivyo hakuna gawio. Cha ajabu kila mkutano mkuu bodi inaomba kuongezewa posho na kuongezwa muda kwa wakaguzi wa nje wa hesabu za kampuni.
Kutokana na hali ya hasara bandia hisa za kampuni hiyo zimeshuka toka sh 500 ya toleo la mwanzo la hisa hadi shs kama 250 tu, kwa hivyo ukiuza hisa unapata hasara.
Mambo ya kujiuliza, kama kampuni inapata hasara miaka yote kwa nini haifilisiki? Tunajua bidhaa za kampuni hiyo zina soko kubwa tu nchini na hakuna ushindani mkubwa.
Kama mdau nashauri kuliko kubariki unyang'anyi huu kampuni iuzwe kwa wawekezaji wengine tuone kama kila mwanahisa hakuondoka na kitita cha kuridhisha