ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,264
- 4,702
Kuna tetesi za ndani kabisa nimezisikia kutoka soko la hisa la dar es salaam (DSE) kwamba wanahisa wake hawatapata gawio mwishoni mwa mwaka wa kiserikali unaoisha mwezi wa sita tarehe 30. Hii ni kutokana na mauzo kidogo ya hisa katika soko hilo, kutopata gawio itakuwa pigo kubwa sana kwa wanahisa. Tukumbuke kuwa ni mwaka jana tu dse waliingia katika soko la hisa na hatujui undani kabisa. Sasa kama uliwekeza basi utatoka kappa. Sababu nyingine inayochangia kutopata gawio ni kufanya vibaya kwa hisa za voda ambapo mpaka sasa wanashindwa kuziweka sokoni kwani ziliuzwa kwa asilimia 40 tu huku 60 zikikosa mnunuaji. Kwakweli hisa c eneo la kuwekeza hasa katika nchi ya KIMAKANIKIA kama Tanzania.