Golden Age
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 203
- 45
UTATA BAINA YA NASH EMCEE & FID Q
Miaka kadhaa iliyopita FID Q alikua akiwaalika wasanii wanaorap hasa wale ma emcee kutoka katika utamaduni wa HipHop katika kipindi chake cha Fidstyle Friday ambapo ma emcee walionyesha uwezo wao, walitoa elimu pamoja na kujadili changamoto mbalimbali kata kiwanda cha muziki.
Binafsi nilishtuka kidogo baada ya kutomuona Nash mc kwenye kipindi kile,unaweza ukauliza kwa nini sikushtuka kutokuwepo kwa Chindo Man,lakini ukweli ni kwamba Chindo alikua ughaibuni kwa kipindi kile.. kwa mujibu wa Maelezo ya mtengwa mwenzie JCB alipofanya mahojiano na Fid q katika Fidstyle friday.
Lakini pia kuna tetesi kwamba kuna sintofahamu inaendelea kati ya Chindo man na Fid q baada ya Chindo kukomenti kwamba Fid q ni wack katika post moja hivi Facebook kipindi kile cha matokeo ya uchaguzi mkuu.OK tuachane na Chindo turud kwa Nash mc.
Movie ilianza rasmi pale Fid q alipoulizwa na shabiki mtandaoni kuhusu sanaa ya Nash mc ambapo shabiki aliuliza "Unaamini Nash mc ana sifa kamilifu za kuitwa emcee?" Fid q akajibu " Honestly... Sijawahi kumsikiliza so sina jibu la swali lako".Kauli hii iliwashtusha wengi na ikapelekea baadhi ya watu kuhisi kwamba hakuna mawasiliano mazuri kati ya Nash mc na Fid q.
Inaonekana wazi kabisa Nash hakupendezwa na kauli ya Fid q na katika mixtape yake ya "CHIZI" Nash ameiongelea hii issue kama Mara mbili hivi.Kwenye wimbo wake wa asiyehusika na hiphop kuna sehemu amesikika akisema "Uwezo wenu inaonekana bila media mnapwaya/wanaosema hawanijui ni wazi wananigwaya".
Pia katika wimbo wake wa mwisho " maswali ya kiwaki" katika orodha ya nyimbo zake kwenye mixtape ya CHIZI kuna mstari amesikika akisema " ambao hawanijui ni wa kuja na hawanisumbui".Ikumbukwe pia Fid q aliwahi kunukuliwa akisema ameinspire asilimia 98 (98%) ya wasanii wa hiphop bongo,takwimu ambazo Binafsi sidhani kama zina ukweli ndani yake na sijui Fid q hizi takwimu alizitoa wapi.
Nash pia aliendeleza mashambulizi ambapo mwanzon mwa mwaka 2014 aliandika "tweets" ambazo zilishtusha watu wengi akiwemo mtangazaji Jabir Saleh kipindi yupo Times FM katika kipindi cha the Jump off alinukuliwa akisema " Leo Nash mc ameandika tweets za moto, ameandika mambo flan ya kushtusha hiv .... ". Nash aliandika tweets nyingi sana nyingine inasemakana zilikuwa zikimlenga rapper wakazi.Tweet mojawapo ni Hii
" Nimeanza sanaa muzik kurecord kwa Hendrico sound crafters elfu 37,fala wako unaemuaminia hajagusa Dar!"
Wana utamaduni wa hiphop wanadai hiyo kauli ilikua ikimlenga Fid q pamoja na wakazi,hapa Nash anamwambia wakazi kwamba huyo emcee Fid q unaemuaminia ni fala tu! ambapo tunaona Nash akijitamba kuwa yeye ni "born town" akimaanisha yeye ni mtoto wa mjini toka kitambo.
Na Hii yote ilikuja Baada ya wakazi kupost picha alizopiga na KRS ONE pamoja na RAKIM ughaibuni Marekani ambapo Nash mc aka comment kwa kusema kupiga picha na hao Hiphop giants / legends(KRS ONE & RAKIM) haimaniishi kuwa wewe ni emcee kwa sabab hata shilole anaweza akapiga nao picha ingawa sio emcee .
Tweets zilikua nyingi unaweza kuzitafuta katika mtandao,lakini mwisho wa siku Nash mc alikanusha kwamba hizo tweets haziashirii ugomvi wowote na kwamba yeye hana ugomvi na msanii yeyote Tanzania.
Nash pia amewahi kuandika katika Twitter " msanii wa hiphop unalewa mpaka unashindwa kufanya show,unazomewa kwenu??????!". Na Hii ilikua ikimlenga Fid q kipindi kile alipopanda stejini akiwa amelewa jijini Mwanza lakin baadae Fid q katika mahojiano kwenye kipindi cha Mkasi pale EATV alieleza kwamba hakulewa kwa makusudi bali kuna mtu alimwekea kilevi bila yeye kujua alipokua back stage.
Pia juzi juzi tu katika wimbo wake wa hasi 15 Nash alisikika akisema " lipstick,shedo ndo mnakua hivi rasta?/ ww ulikua wapi nilivyokua hapa?/Pale jite ute kila wiki matamasha........Hapo tunaona Nash akimdiss Fid q kuwa alijipaka lipstick kwenye video yake ya Bongo Hiphop,Lakini Fid alipoulizwa kuhusu hili alijibu hivi namnukuu " Sijapaka lipstick zile ni lips zangu baada ya kufanya editing"...kwa hiyo...Pia tunaona Nash mc akijigamba kwamba yeye ni born town yaani mtoto wa mjini kutoka kitambo na.....itaendelea
Muendelezo utakuwepo katika kitabu cha HipHop na Maisha ambacho kitatoka hivi karibuni na kitauzwa kwa shilingi za kitanzania elfu tano tu.Unaweza ukaweka oda yako mapema kupitia namba 0713560346 / 0743959819
Asanteni ...
Naomba kuwasilisha