WanaHipHop wote tukutane hapa Fid q Vs Nash Emcee (2)

Kitabu chako binafsi naona hakina tija kabisa kwa jamii nzima ya vichwa wa Hip Hop. Sikukatishi tamaa, la hasha! Maudhui ya kitabu chako hayawezi kuamsha hisia za ndani, itikadi na imani kwa wachemkaji ama wale wanaojinasibu kuwa wanajamii ya Hip Hop. Hisia zako ndugu mwandishi zinaongozwa zaidi na mihemko ya hapa na pale pamoja na matukio flani flani yaliyotokea punde kuhusiana na fani ya hapa nyumbani Bongo. Nasema tena maudhui hayana mashiko ya kuitwa kitabu cha Hip Hop. Makusanyo ya mtandaoni na kutoka mitandao ya kijamii ndio muongozo wako hasa. Ingekuwa rahisi namna hii, kungekuwepo na hazina kubwa sana ya kutosha ya hivi vitabu. Binafsi sikufahamu wewe na ada/mchango wako uliolipa/unaolipa katika hii fani hivyo inaweka ukungu sana katika taswira ninayotazama toka kwako na hiki kitabu. Nilitazama mada zote za hiki kitabu, binafsi hakuna jipya la kuingiza zaidi ya tungeketi wana kadhaa kisha tukaanza kusimuliana haya yote na kupeana tano, kisha tusikikize ngoma kadhaa tutawanyike. Sina chuki, wivu au majungu. Naheshimu muda na nguvu pamoja na akili unazotumia kuandaa hii kitu. Baadhi ya jamii zimepinga sana juhudi zako za kuandaa kitabu cha Hip Hop hapa Bongo kikiwa na maudhui mepesi namna hiyo. Fuatilia namna Gospel Of Hip Hop kilivoandaliwa, The Tao of Wu cha RZA, There Is A God On The Mic cha Kool Moe Dee, How To Rap(part 1&2) pamoja na makala kibao zakina Davey D na vichwa wengine wanaotunza historia adhimu ya huu Utamaduni wa Hip Hop na watu wake kwa ujumla. Mfano simulizi za mahusiano/majibizano ya huyo Fid Q na Nash, ningeweza kufuatilia huko mtandaoni na vijiweni kote wanakokaa ama kuzungumziwa hawa watu. Hip Hop ni zaidi ya hao vichwa wawili ndugu. Kuna mengi ya dhati kuyaandika zaidi ya hayo kuhusiana na fani yetu hapa nyumbani. Kurasa zinazosherehesha suala la hawa wandugu ni uchafu katika kitabu chako. Kama wanawania kuwa kinara kwa mtindo huo, hawajengi fani. Bado nafunguka... Kuna mada za kina Assata Shakur na kina Jadakiss wa The Lox, kaka, kitabu si kirahisi namna hii. Kama kuna wana wamekupa gwara kuandaa hii kitu, sio mbaya, ila kuandaa kitabu hasa cha Hip Hop, au makala, ni kitu ingine. Sema kishkaji shkaji tu zile za maskani mbona hapo umetishaaaa sana kaka. Hakuna kitu rahisi ndani ya Hip Hop. Hata kimoja. Hii inatokana na kuwa mtindo wa maisha wa watu flani flani. Watu hao wanaamini katika namna mbali mbali ndani ya hiyo Hip Hop. Machafuko ni mengi. Amani hutoweka muda mwingi na kurejeshwa kwa namna kadhaa kama vile kufanya ngoma/onesho kwa pamoja kutembeleana maskani na kuwa na Session za pamoja..namna hiyo. Watu wote waliotofautiana kunako Hip Hop wanatakiwa warejeane kwa pamoja na kufuta tofauti zao na kushirikiana katika kujenga fani hii kwa pamoja. Na sio majibizano katika mitandao ya kijamii tu huku uchechezi ukizidi kutoka kwa watu wao wanaowakubali.
 
Ni angalau ulichokianfika kinaweza kuuzika, kwa sababu umejitahidi kutumia upeo wako kuchambua jambo, sio mtu anatoa tweet mtandaoni alafu anaandika kitabu.
 
NASH MC MZUZU MAALIM

MASWALI YA KIWAKI

MKONGWE

MITIHANI

TABIA

SHUJAA

nk hyu mtu ni hatare sana aiseeh... msikikizeni
 
Et Fid na Chindo haziivi? sasa walifanyaje ile torati ya mtaa? Tatizo la Nash anajifanyaga HIPHOP Anaijua yeye peke yake na Nguzo zote anazo yeye tu. hilo ndo tatizo lake tuu akifanikiwa kuachana na upuuzi huo huenda akawa mwanahiphop mzuri tu.
Sijawahi kujua huyo Nash kama kuna msanii wa hiphop anamkubali hapa bongo, maana anajikuta yeye tu ndio anafanya hiphop. By the way Nash huwezi mfananisha na FID hata kidogo, Nash yuko kawaida sana
 
Acha kumfananisha Fid q na vitu vya kipuuzi.
Baada ya hizo tweets na mistari ya huyo Nash, Je Fid alishawahi kujibu chochote..?
 
UTATA BAINA YA NASH EMCEE & FID Q
Miaka kadhaa iliyopita FID Q alikua akiwaalika wasanii wanaorap hasa wale ma emcee kutoka katika utamaduni wa HipHop katika kipindi chake cha Fidstyle Friday ambapo ma emcee walionyesha uwezo wao, walitoa elimu pamoja na kujadili changamoto mbalimbali kata kiwanda cha muziki.Binafsi nilishtuka kidogo baada ya kutomuona Nash mc kwenye kipindi kile,unaweza ukauliza kwa nini sikushtuka kutokuwepo kwa Chindo Man,lakini ukweli ni kwamba Chindo alikua ughaibuni kwa kipindi kile.. kwa mujibu wa Maelezo ya mtengwa mwenzie JCB alipofanya mahojiano na Fid q katika Fidstyle friday.

Lakini pia kuna tetesi kwamba kuna sintofahamu inaendelea kati ya Chindo man na Fid q baada ya Chindo kukomenti kwamba Fid q ni wack katika post moja hivi Facebook kipindi kile cha matokeo ya uchaguzi mkuu.OK tuachane na Chindo turud kwa Nash mc.

Movie ilianza rasmi pale Fid q alipoulizwa na shabiki mtandaoni kuhusu sanaa ya Nash mc ambapo shabiki aliuliza "Unaamini Nash mc ana sifa kamilifu za kuitwa emcee?" Fid q akajibu " Honestly... Sijawahi kumsikiliza so sina jibu la swali lako".Kauli hii iliwashtusha wengi na ikapelekea baadhi ya watu kuhisi kwamba hakuna mawasiliano mazuri kati ya Nash mc na Fid q.

Inaonekana wazi kabisa Nash hakupendezwa na kauli ya Fid q na katika mixtape yake ya "CHIZI" Nash ameiongelea hii issue kama Mara mbili hivi.Kwenye wimbo wake wa asiyehusika na hiphop kuna sehemu amesikika akisema "Uwezo wenu inaonekana bila media mnapwaya/wanaosema hawanijui ni wazi wananigwaya".

Pia katika wimbo wake wa mwisho " maswali ya kiwaki" katika orodha ya nyimbo zake kwenye mixtape ya CHIZI kuna mstari amesikika akisema " ambao hawanijui ni wa kuja na hawanisumbui".Ikumbukwe pia Fid q aliwahi kunukuliwa akisema ameinspire asilimia 98 (98%) ya wasanii wa hiphop bongo,takwimu ambazo Binafsi sidhani kama zina ukweli ndani yake na sijui Fid q hizi takwimu alizitoa wapi.

Nash pia aliendeleza mashambulizi ambapo mwanzon mwa mwaka 2014 aliandika "tweets" ambazo zilishtusha watu wengi akiwemo mtangazaji Jabir Saleh kipindi yupo Times FM katika kipindi cha the Jump off alinukuliwa akisema " Leo Nash mc ameandika tweets za moto, ameandika mambo flan ya kushtusha hiv .... ". Nash aliandika tweets nyingi sana nyingine inasemakana zilikuwa zikimlenga rapper wakazi.Tweet mojawapo ni Hii

" Nimeanza sanaa muzik kurecord kwa Hendrico sound crafters elfu 37,fala wako unaemuaminia hajagusa Dar!"

Wana utamaduni wa hiphop wanadai hiyo kauli ilikua ikimlenga Fid q pamoja na wakazi,hapa Nash anamwambia wakazi kwamba huyo emcee Fid q unaemuaminia ni fala tu! ambapo tunaona Nash akijitamba kuwa yeye ni "born town" akimaanisha yeye ni mtoto wa mjini toka kitambo.

Na Hii yote ilikuja Baada ya wakazi kupost picha alizopiga na KRS ONE pamoja na RAKIM ughaibuni Marekani ambapo Nash mc aka comment kwa kusema kupiga picha na hao Hiphop giants / legends(KRS ONE & RAKIM) haimaniishi kuwa wewe ni emcee kwa sabab hata shilole anaweza akapiga nao picha ingawa sio emcee .

Tweets zilikua nyingi unaweza kuzitafuta katika mtandao,lakini mwisho wa siku Nash mc alikanusha kwamba hizo tweets haziashirii ugomvi wowote na kwamba yeye hana ugomvi na msanii yeyote Tanzania.
Nash pia amewahi kuandika katika Twitter " msanii wa hiphop unalewa mpaka unashindwa kufanya show,unazomewa kwenu?????? Pumbavu!". Na Hii ilikua ikimlenga Fid q kipindi kile alipopanda stejini akiwa amelewa jijini Mwanza lakin baadae Fid q katika mahojiano kwenye kipindi cha Mkasi pale EATV alieleza kwamba hakulewa kwa makusudi bali kuna mtu alimwekea kilevi bila yeye kujua alipokua back stage.

Pia juzi juzi tu katika wimbo wake wa hasi 15 Nash alisikika akisema " lipstick,shedo ndo mnakua hivi rasta?/ ww ulikua wapi nilivyokua hapa?/Pale jite ute kila wiki matamasha........Hapo tunaona Nash akimdiss Fid q kuwa alijipaka lipstick kwenye video yake ya Bongo Hiphop,Lakini Fid alipoulizwa kuhusu hili alijibu hivi namnukuu " Sijapaka lipstick zile ni lips zangu baada ya kufanya editing"...kwa hiyo...Pia tunaona Nash mc akijigamba kwamba yeye ni born town yaani mtoto wa mjini kutoka kitambo na.....itaendelea

Muendelezo utakuwepo katika kitabu cha HipHop na Maisha ambacho kitatoka hivi karibuni na kitauzwa kwa shilingi za kitanzania elfu tano tu.Unaweza ukaweka oda yako mapema kupitia namba 0713560346 / 0743959819

Asanteni ...

Naomba kuwasilisha
Hiphop inajibiwa kwa nyimbo...huwezi msifia msanii kwa ku tweet..toa reference ya nyimbo zake...album ngap...nyimbo zake kali ni zipi...hivi ndo vigezo vya msanii...sio kukaa kwny computer ku tweet hizo mambo wanafanya wakina trump daily
 
Nash ni mpuuzi kuna siku nikaskia anasema Nash EMCEE Uandishi kama wa shaban robert nikasema huyu mpuuzi hana anachokijua zaidi ya kufuga mandevu uchizi tuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom